Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

Pia ingekuwa vizuri sana mwendokasi ndo ziende mbezi ,Ubungo ibaki ya mabus pale ni centa kwa wengi,maana mwendokasi hata yard iwe mjini lazima aende mbezi akafate watu.Hivo ni bora yard yao iwe mbezi iamkie na kulalia huko huko mwisho wa ruti yake.Hii iko poa sana kama planner wakiizingatia.
Mwendo kasi ni kwa ajili ya inner city movements hivyo kimkakati ni vizuri wawepo katikati wao na ofisi zao.

By the way, gazeti la Mtanzania la juzi juzi naibu waziri wa tamisemi aliongea kuwa kuna mwekezaji mwingine ataleta mabasi yake (Emiratea toka dubai), je nae ataweka mabasi yake hapo ubungo??
 
Nafikiri magari ya kwenda Kaskazini kituo kipelekwe kule Tegeta dawasco na mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi kipelekwe Kibaha. Then magari ya kusini yabakie Temeke


Ushauri mzuri pia, lakini kama nguvu ya kujenga hizo stand Temeke, Kibaha na Tegeta zikiunganishwa na kuweka barabara za uhakika kutokea hapo Mbezi itakuwa imetatua kero nyingi kwa wakati mmoja
 
Kweli mkuu. Ni Bora wangetumia elimu yao ya utaalamu angalau pale jangwani Wangeweza hata kujenga mtambo wa kuchakata yale maji taka yawe safi nyakati za mvua ila badala yake wamejenga maofisi kwenye mkondo wa maji tena maji yanayotuama , maji machafu yanayoelekea baharini . Yaani kwenye njia kuu kabisa ya maji .

Hii akili au tope. Shame on you wote mliotumia kodi yangu vibaya. [emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]

Na huo mradi wenyewe utadhani daladala za mlala hoi mradi unanyong'onyea kama container lililosimamishwa juu ya vijiti vya chelewa. Hasara tupu
Kutumia elimu yao positively si rahisi mkuu. Wako kimaslahi binafsi zaidi, jambo ambalo linatuumiza sisi walipa kodi.
 
Ni ajabu sana ata baada ya miaka 50 ya uhuru bado tunawaza stand za mabasi ..
Aliyeturoga sijui ni nani..

Haya ni matumizi mabaya ya ofisi..

Hasara ishatokea pale jangwani kodi ya Mwananchi imetumika vibaya..nani awajibike..??
 
Unaweza kujenga kitu sehemu sahihi lakin natural calamities huwez kuzikwepa kama ikitokea zikaja tofaut hata huko ma mbele wanahangaika na haya majanga
Jangwani panajulikana tokea Taifa la Tanzania linanzishwa, ni sehemu korofi kwa kujaa maji.
 
Kosa ndo limeshafanyika,pale Jagwani wageuze tu kuwa mradi wa viboko maana tukiweka samaki watabebwa na mafuriko.hahah
 
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT).

Hatua hiyo inatokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo.

Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa ili kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika.

Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo ili waweze kufikia mwafaka.

“Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,”alisema Mwita.

Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mto Msimbazi uweze kuwa na nafasi kubwa ya kusafirisha maji hadi baharini.

Meya alisema jambo hilo linaweza kupunguza mafuriko katika eneo la Jangwani na maeneo karibu na mto huo.

Alisema fedha za upanuzi huo zimekwisha kutolewa, kilichobaki ni utekelezaji wa mradi kuanzia daraja la Salendar hadi Pugu.

“Awamu ya kwanza ya mradi itaanzia Salendar hadi Kigogo, jambo ambalo linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo la mafuriko kwa wakazi wa Jangwani na maeneo jirani ya mto Msimbazi,” alisema.

Vilevile, Meya Mwita alisema Serikali Kuu imetoa shilingi bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa çha mabasi yaendayo mikoani, kitakachojengwa Mbezi Mwisho.

Alisema licha ya kutolewa kiasi hicho cha fedha, jiji limetoa shilingi bilioni nane kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi ambao maeneo yao yatachukuliwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

“Tunatarajia kupata ekari 24 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha Mbezi Mwisho, ujenzi ambao utaanza wakati wowote kuanzia sasa. Mkakati uliopo ni kuwalipa fidia wananchi wa eneo lile tuweze kuendeleza mradi,” alisema.

Alisema mradi huo utachukua miaka miwili kukamilika na ndani yake kutakua na maduka na nyumba za kulala wageni, jambo ambalo linaweza kuwasaidia kuongeza mapato.

Alisema mwaka huu katika makusanyo yake ya kila mwaka, halmashauri imeingiza shilingi bilioni 22 ambazo zitatumika kwa mambo mbalimbali yakiwamo uendelezaji wa miradi.

Chanzo: Swahili Times
========

Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kupeleka kwenye kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo UBT, kutokana na eneo hilo la Jangwani kujaa maji kila mara wakati mvua zinaponyesha.

Picha ya chini ni mchoro wa kituo kipya cha mabasi ya mikoani kitakachojengwa Mbezi Luois jijini Dar es salaam.View attachment 771061View attachment 771062
Mpaka sasa, Kitua cha mabasi ya mikoani pale Ubungo, kwa abiria wengine kama wataondoka Mbagala, Kigamboni, Kongowe nk ni mateso hasa kwa wale wa kipato cha chini.
Abiria wa tabaka hili hupata shida sana ikizingatiwa kwamba hushindwa kumudu gharama za kukodi vyumba vya kulala karibu na stendi ya Ubungo.

Leo Halmashauri ya Jiji inafikiria kuzidisha umbali tena hadi Mbezi, inawafikiriaje abiria hawa wa Kipato cha chini?

Kwa mtazamo wangu, badala ya Halmashauri ya Jiji kuihamisha Ubungo Bus Stand kupisha Dart, DART ndio wahamishiwe Mbezi baada ya kufanya ujenzi mdogo wa dharula wa ofisi na gereji na kuiacha Ubungo Stand ikiendelea kuhudumia abiria wa mikoani.

Kama ni makosa yalikwishafanyika ya kuliingizia hasara Taifa. Na ikumbukwe kuwa moto hauzimwi kwa moto bali maji. Hivyo hatua za haraka zinazokusudiwa katika utatuzi wa suala la DART halitakuwa na afya kwa watumiaji wengine.

Nashauri DART wahamie Mbezi na Ubungo Stand ibaki kwa ajili ya mabasi ya mikoani, ila ifanyiwe ukarabati mkubwa wa kuiboresha.
NAWASILISHA.
 
kwahiyo zile pesa zilzio tumika kujengea ule mradi pale. jangwani " tuhesabu kuwa ni hasara ...""aiseee Hawa viongozi wangekuwa ni raia wa China wangeshanyongwa

period "" wanatumia pesa za wananchi hovyo sijui huwa wanatumia makalio kufikiri
 
Mkuu wwe huoni kuna mianya inatengenezwa hapo watu waishi
Jiulize ujenzi wa huu mradi ulianza lini
Hawakuwa na uchambuz yakinifu juu ya eneo la jangwani
Nani aliizinisha ujengaji wa yard bila kufata ushauri

Hizi ni janja janja za upotevu wa pesa
hatari sana "" haya majizi ya taifa ..yaani mradi umedumu miaka miwili na nusu tu "" Tayari umeshalipatia taifa hasara...hiiiiiii
 
"....kabla hawajaanza ujenzi, walinletea Ombi, wakitaka ruhusa ya kujenga pale Jangwani. Nikawakatalia kwa maelezo kuwa pale hapafai na si salama...... siku moja nikawa napita pale (Jangwani)..... nikakuta kuna pilikapilika nyingi..... nikauliza, kuna nini pale? Nikajibiwa: Kituo cha Mwendokasi, nikashangaa sana, nikasema ngoja ninyamaze Mswahili Mimi"
Nani alitamka haya maneno mkuu?
 
Si kama mkubwa anavyosema mimi ni rais wa wanyonge.
Ila kiuhalisia anamanisha kuwanyonga.

-load board 15%
-kama umesoma privte no loan. Ila yy alisoma private na kasomeshwa tena elimu ya watu wazima na mshahara juu kwa kuunga unga.
- alijaribu kuwaombea wakina jesica mkopo pia.


— rais wa vyana vyote. Hapo hapo lisu kwachuu. Sugu ndani
tuache siasa tuijenge nchi ...huku yeye na pole pole wanapita mikoani nakufanya mikutano ya kichama tena sometimes katika msafara wa kiserikali....

huyu mzee iko namna
 
Je jangwani patabomolewa?? VERY POOR PLANNING!
Na pia daraja la wavuka kwa miguu pale Ubungo bus terminal litakuwa linatumika kwa madereva ma staff wa udart kuvuka??
Tetesi za stendi kuhamia Mbezi ni za muda sasa, labla hata mwendokasi haujakamilika, sielewi kwa nini waliweka lile daraja uelekeo wa ndani ya syendi ya mkoa. Pesa hiyo ingejenga zahanati mahali kuliko ilivyotupwa pale maana ni wazi upande huo wa daraja hautakuwa na tija.
daaahh ukiona hadi wew unalalamika means kweli hii serikali nimtihani "" yaani mpka mtoto umeamua kumkosoa mzazi "" hii ndio nchi Yetu bwana ..mazingaombwe ndio kwao
 
Acha tu waendelee kuchezea pesa, ila mm nawalaum wale wa mwanzo. Serikali iliwafukuza raia maeneo karibu na pale kuwa ni hatarishi. Iweje wao wajenge pale,?????
Sipati picha garama zake mana kuhama tu sio suluhisho, pale Jangwani maji yanapita juu. Huo ni mziki mwingine .
 
Watanzania hatunaga mipango endelevu siku zote.......

Ova
 
Ingefaa injinia wa jiji wakati wa upanuzi wa MTO msimbazi abuni mchoro kama wa Suez canal..

ili huo mfereji ubaki kuwa njia ya usafiri kwa boti na..

moja kwa moja uchafuzi wake utakoma kwa wananchi kuutunza na utalipendezesha zaidi jiji [emoji89]
 
Back
Top Bottom