Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

Mwanadamu sio Mungu ni jambo jema kuhamishia kituo cha mwendokasi ubungo ili stendi ya ubungo iende mbezi luis
Uko tumamu kweli mkuu?

Kwahiyo na hapo unasema "mwanadamu sio Mungu"
as if hawakujua kwamba maji hutuama hapo jangwani, kwani walihitaji mtabiri kujua jangwani huwa kunajaa maji?

Miaka yote walikuwa kipaumbele kuwafukuza wananchi then wakajenga wao, wamepoteza fedha za wanachi kiasi gani? Nani aliyepitisha jambo hili? amewajibishwa au ndio mnalindana?

leo wakajenge sehemu nyingine kwa fedha za nani? tukisema ccm ni mazwazwa mnasema wananchi wanawatukana
Huo si unakaribia utindio wa ubongo??
 
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT).

Hatua hiyo inatokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo.

Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa ili kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika.

Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo ili waweze kufikia mwafaka.

“Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,”alisema Mwita.

Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mto Msimbazi uweze kuwa na nafasi kubwa ya kusafirisha maji hadi baharini.

Meya alisema jambo hilo linaweza kupunguza mafuriko katika eneo la Jangwani na maeneo karibu na mto huo.

Alisema fedha za upanuzi huo zimekwisha kutolewa, kilichobaki ni utekelezaji wa mradi kuanzia daraja la Salendar hadi Pugu.

“Awamu ya kwanza ya mradi itaanzia Salendar hadi Kigogo, jambo ambalo linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo la mafuriko kwa wakazi wa Jangwani na maeneo jirani ya mto Msimbazi,” alisema.

Vilevile, Meya Mwita alisema Serikali Kuu imetoa shilingi bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa çha mabasi yaendayo mikoani, kitakachojengwa Mbezi Mwisho.

Alisema licha ya kutolewa kiasi hicho cha fedha, jiji limetoa shilingi bilioni nane kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi ambao maeneo yao yatachukuliwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

“Tunatarajia kupata ekari 24 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha Mbezi Mwisho, ujenzi ambao utaanza wakati wowote kuanzia sasa. Mkakati uliopo ni kuwalipa fidia wananchi wa eneo lile tuweze kuendeleza mradi,” alisema.

Alisema mradi huo utachukua miaka miwili kukamilika na ndani yake kutakua na maduka na nyumba za kulala wageni, jambo ambalo linaweza kuwasaidia kuongeza mapato.

Alisema mwaka huu katika makusanyo yake ya kila mwaka, halmashauri imeingiza shilingi bilioni 22 ambazo zitatumika kwa mambo mbalimbali yakiwamo uendelezaji wa miradi.

Chanzo: Swahili Times
========

Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kupeleka kwenye kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo UBT, kutokana na eneo hilo la Jangwani kujaa maji kila mara wakati mvua zinaponyesha.

Picha ya chini ni mchoro wa kituo kipya cha mabasi ya mikoani kitakachojengwa Mbezi Luois jijini Dar es salaam.View attachment 771061View attachment 771062
JK alishawi kusema kuwa ule mradi uonolewe pale, mijitu ikapotezea.
Si kwa matumizi haya mabaya ya fedha zetu. Ubungo si ni juzi tu imekarabatiwa?
Duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu.

Open-space Jangwani: Kikwete adanganywa tena!?
 
Uko tumamu kweli mkuu?

Kwahiyo na hapo unasema "mwanadamu sio Mungu"
as if hawakujua kwamba maji hutuama hapo jangwani, kwani walihitaji mtabiri kujua jangwani huwa kunajaa maji?

Miaka yote walikuwa kipaumbele kuwafukuza wananchi then wakajenga wao, wamepoteza fedha za wanachi kiasi gani? Nani aliyepitisha jambo hili? amewajibishwa au ndio mnalindana?

leo wakajenge sehemu nyingine kwa fedha za nani? tukisema ccm ni mazwazwa mnasema wananchi wanawatukana
Huo si unakaribia utindio wa ubongo??
Tatizo hujui maana ya mjadala huru unachowaza wewe sio lazima kiwe sawa hadi unachapia chapia maana ya forum huru kila mmoja anakuja na mawazo tofauti hadi kufikia hitimisho kwa mfano kila mmoja angekuwa anawaza sawasawa na mwenzie anachowaza jamii forum na mijadala vingekuwepo?

Shida moja ya ngozi nyeusi pakitokea mmoja akawa tofaut na wazo lake basi akili yako inawaza unafikiria kwa utimamu mjinga wewe kila mmoja anakuja na wazo lake then hitimisho linapatikana jawabu moja
 
Watu wanaotetea ufirauni kama wewe ndio sababu mwafaka ya kuwepo kwa adhabu ya kifo
Chaajabu imekuwa vice versa.
Elimu yetu haitufunzi maana ya mijadala tunachofikiria wote tuwaze kitu kimoja rudi shule hapa utakutana na mawazo toafut kwa asiejua atapata elimu ila ukitaka kila mmoja awaze vile unataka fungua forum yako halafu contro mawazo ya kila member fala wewe
 
Asante mkuu!
 
Japo inauma sana kuona kodi zetu zinachezewa kwa kiwango hiki
 
G
Ingefaa injinia wa jiji wakati wa upanuzi wa MTO msimbazi abuni mchoro kama wa Suez canal..

ili huo mfereji ubaki kuwa njia ya usafiri kwa boti na..

moja kwa moja uchafuzi wake utakoma kwa wananchi kuutunza na utalipendezesha zaidi jiji [emoji89]
ingekua bonge LA kivutio kama ujeruman na MTO wao
 
Kwa nini hao mwendo kasi wasipelekwe huko Mbezi! Wabongo bwana ni shida, yote hii ni kumuongezea shida mlalahoi, nitoke Kigoma, nilale Morogoro, nifike Mbezi nianze safari nyingine ya kwenda Mbagala viongozi hamlioni hili?
Kweli kabisa, mwendokasi waende mbezi. Kituo cha mikoani kibaki palepale.
 
Mwanadamu sio Mungu ni jambo jema kuhamishia kituo cha mwendokasi ubungo ili stendi ya ubungo iende mbezi luis
Acheni kumsingizia mungu mambo ya kijinga, nani ambaye hajui jangwani ni bonde la mpunga? Kama wananchi walihamishwa kwa nguvu why serikali wao walijenga? Mbona UDA enzi za mabasi ya Icarus kituo chao kilikuwa Ubungo hapo terminal? Walikuwa wajinga? Ni kipindi cha Keenja ndipo stend ilihamishwa from Kisutu kuja hapo terminal Ubungo.
 
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT).

Hatua hiyo inatokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo.

Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa ili kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika.

Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo ili waweze kufikia mwafaka.

“Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,”alisema Mwita.

Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mto Msimbazi uweze kuwa na nafasi kubwa ya kusafirisha maji hadi baharini.

Meya alisema jambo hilo linaweza kupunguza mafuriko katika eneo la Jangwani na maeneo karibu na mto huo.

Alisema fedha za upanuzi huo zimekwisha kutolewa, kilichobaki ni utekelezaji wa mradi kuanzia daraja la Salendar hadi Pugu.

“Awamu ya kwanza ya mradi itaanzia Salendar hadi Kigogo, jambo ambalo linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo la mafuriko kwa wakazi wa Jangwani na maeneo jirani ya mto Msimbazi,” alisema.

Vilevile, Meya Mwita alisema Serikali Kuu imetoa shilingi bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa çha mabasi yaendayo mikoani, kitakachojengwa Mbezi Mwisho.

Alisema licha ya kutolewa kiasi hicho cha fedha, jiji limetoa shilingi bilioni nane kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi ambao maeneo yao yatachukuliwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

“Tunatarajia kupata ekari 24 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha Mbezi Mwisho, ujenzi ambao utaanza wakati wowote kuanzia sasa. Mkakati uliopo ni kuwalipa fidia wananchi wa eneo lile tuweze kuendeleza mradi,” alisema.

Alisema mradi huo utachukua miaka miwili kukamilika na ndani yake kutakua na maduka na nyumba za kulala wageni, jambo ambalo linaweza kuwasaidia kuongeza mapato.

Alisema mwaka huu katika makusanyo yake ya kila mwaka, halmashauri imeingiza shilingi bilioni 22 ambazo zitatumika kwa mambo mbalimbali yakiwamo uendelezaji wa miradi.

Chanzo: Swahili Times
========

Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kupeleka kwenye kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo UBT, kutokana na eneo hilo la Jangwani kujaa maji kila mara wakati mvua zinaponyesha.

Picha ya chini ni mchoro wa kituo kipya cha mabasi ya mikoani kitakachojengwa Mbezi Luois jijini Dar es salaam.View attachment 771061View attachment 771062
Hicho kituo Mbezi kingekuwa gereji na ofisi za kampuni, UBT ibaki hapo ila iboreshwe (multilevel & multi functional), satellite cities ziwe na terminals zao. Vinginevyo muda si mrefu mtakujahamia Kibaha.
 
Unaweza kujenga kitu sehemu sahihi lakin natural calamities huwez kuzikwepa kama ikitokea zikaja tofaut hata huko ma mbele wanahangaika na haya majanga
Watu wasomi na taaluma zao wamewekeza na kujenga yard ya multi-million ktk natural drainage ya jangwani halafu unasema vipi natural calamities hazikwepeki?
 
Mwanadamu sio Mungu ni jambo jema kuhamishia kituo cha mwendokasi ubungo ili stendi ya ubungo iende mbezi luis
Tatizo halipo kwenye kuhamisha tatizo lipo kwenye hizo hela walizotumia kujenga pale Jangwani kwanini wasingejenga hapo Ubungo mapema?

Ni uwendawazimu watu wanapelekwa shule na baba zao halafu wanamaliza wanaingia mtaani wakiwa hawajui kama kujenga pembeni mwa mkondo wa maji kuna madhara kisha useme binadam sio Mungu.

Huu ni utoto!!!
 
Back
Top Bottom