Satoh Hirosh
JF-Expert Member
- Mar 30, 2021
- 6,432
- 25,646
Leo asubuhi nimepishana na mabasi mengi sana ya mikoa ya Kusini pamoja na basi ndogo za Mkuranga na Kibiti yakielekea stendi ya Kijichi. Nikamuuliza mtu mmoja imekuwaje leo haya magari yanaenda Kijichi badala ya Mbagala rangi 3? akajibu magari yote ya mikoani yanayoanzia Mbagala Sasa hivi stendi yao ni Kijichi.
Kwa hiyo hata Ester ya Arusha na Tashirifu ya Tanga zitaanzia Kijichi, hapo Mbagala panabomolewa.
Majibu yalikuwa mengi maana kila mtu akawa anasema yake, mara mtu kanunua lile eneo la Rangi Tatu, mara halikuwa eneo la serikali, mara serikali inataka kuliendeleza eneo. Sikutoka na jibu moja la uhakika.
Ila serikali imeruhusu vipi kuhamishia stendi Kijichi au ni dharura?
Nimefika njia ya ng'ombe nimekutana na tashirifu ya ya Tanga inastrugle kukata Kona, gari linaenda mbele taratibu Kisha linarudi nyuma ili likae vizuri kwenye lane yake kisha iendelee na safari. Barabara nyembamba na gari ni refi, nina uhakika hata njia panda ya Neruka Kuna kitu Kama hiko kinatokea.
Zile barababra za mtaani kule Kijichi, kuanzia Neruka hadi kufika stendi ilipo ni nyembamba nazo, ukipishana tu na roli za mchanga mwenye gari ndogo lazima asimame kwanza Kisha roli lipite maana linajaa Barabara yote.
Kama stendi imehamia Kijichi moja kwa moja sijui itakuwaje na ile mibasi ya mkoani kwenye zile Barabara nyembamba!
Alafu Kijichi naona Kama imekaa kushoto kwa abiria wa sehemu zingine maana ipo ndani. Ni kama uitoe stendi ya Magufuli pale Mbezi Kisha uihamishie Goba kwa ndani, lazima kutatokea usumbufu sana.
Mpaka Sasa hivi sijui kwanini stendi imehamishwa rangi tatu. Mtu mmoja nilimsikia anasema ni heri wangejenga stendi mpya Kongowe au Mwandege karibu na kiwanda cha bahresa kuna eneo kubwa.
Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app