Stendi ya Mbagala Rangi Tatu kuhamishiwa Kijichi, sababu ni nini?


17 October 2022
STENDI YA KIJICHI DAR ES SALAAM KUZINDUKIWA

Wadau waongelea wembamba wa barabara
Source : TMC TV

"Nimepokea maoni yenu, timu ya pamoja tuliyoiunda itayafanyia kazi mapungufu yaliyopo na niwahakikishie tu kuwa kabla ya tarehe 17 October 2022 kila kitu kitakuwa sawa". Alisisitiza mkurugenzi wa manispaa ya Temeke ndugu Elihuruma Mabelya.
 

MKURUGENZI TEMEKE AKUTANA NA WAMILIKI WA MABASI​

Posted On: October 7th, 2022
Na:Shalua Mpanda na

Sweetbetter Njige

TMC - Habari.

Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke ndugu Elihuruma Mabelya Oktoba 7,2022 amekutana na TABOA na DARCOBOA ambao ni Wamiliki wa Mabasi, pamoja na Wadau mbalimbali kujadili kuhusu kuanza kutumika kwa Stendi ya Kijichi kwa safari za Mikoani.

Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na katibu tawala wa Wilaya, Bi Bupe Mwakibete , mwakilishi kutoka LATRA na Afisa Usalama Barabarani Wilaya ( DTO) ni muendelezo wa vikao vingine viwili ambapo tarehe 04/10 2022 kikao kama hicho kilifanyika, na kiliwahusisha Wamiliki wa Stendi za Mbagala ambazo ni stendi namba 17,21 na 48.

Na kikao kingine cha tarehe 03/10/2022 kilichohusisha Umoja wa Madereva Usafirishaji na Uchukuzi Tanzania ( UWAMATA,UWASAKUTA NA MUWAKUTA), lengo likiwa ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu suala hilo ambalo ni kwa maslahi mapana ya Manispaa na Wananchi kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkurugenzi Mabelya alieleza dhamira ya Serikali ya kuboresha miundombinu ya usafirishaji na kuwatoa hofu Wamiliki hao wa Mabasi kuwa Manispaa imejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa wa kiasi kikubwa.

Aidha Mkurugenzi Mabelya alipokea maoni, ushauri na mapendekezo juu ya namna bora ya kushughulikia suala hilo na kisha kuteua wajumbe kutoka TABOA na DARCOBOA kuungana na Kamati ya Manispaa inayoshughulikia mchakato wa kuhamia Stendi ya Kijichi ili kwa pamoja waweze kushughulikia changamoto zote na hatimaye kutimiza lengo.

"Nimepokea maoni yenu, timu ya pamoja tuliyoiunda itayafanyia kazi mapungufu yaliyopo na niwahakikishie tu kuwa kabla ya tarehe 17 kila kitu kitakuwa sawa". Alisisitiza Mkurugenzi Mabelya.

Katika hatua nyingine baadhi ya wajumbe wa kikao hicho walitaka kuhakikishiwa juu ya usalama wa Raia na mali zao katika Stendi hiyo mpya ambapo katibu tawala Bi.Bupe Mwakibete alisema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya "imebariki" zoezi hilo na ipo tayari kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa wakati wote katika stendi hiyo ya Kijichi.

Manispaa haikuwa na stendi ya mabasi, sasa imetenga eneo la Kijichi kuwa stendi ya mabasi ya kwenda mikoani, na inatarajiwa kuanza kutumika rasmi Oktoba 17,2022.
Source : MKURUGENZI TEMEKE AKUTANA NA WAMILIKI WA MABASI
 
11 October 2022

DC Jokate Mwengelo - Stendi ya Kijichi wilaya ya Temeke, Dar es Salaam wepesi wa kutoa huduma na kutoathiri huduma uzingatiwe

Jokate Mwegelo wilaya ya Temeke ni kubwa, maamuzi ya kuhamisha stendi Kijichi mradi wake pamoja na soko umegharimu Tshs. 3.9 Bn.

Hivyo juhudi zifanyike miundo-mbinu yote irekebishwe ili kuweza kupokea jukumu jipya bila kuathiri watakaotumia stendi mpya na soko vilivyopo Kijichi anamalizia DC Jokate Mwegelo.
Source : TMC TV
 
Hiyo stendi kuhamishiwa hapo ndani yake kuna siasa nyingi na michongo ndani yake kuna watu wamejiamulia kwa maslahi yao na kuwakomoa watu fulani bila kufanya uchambuzi na tathimini za kutosha kuhusu umuzi kwa kuchambua faida ,hasara na ubora wa stendi kuwa hapo kulinganishwa na eneo lingine.

Juzi nipo mitaa ya Buza ninapoishi katika ofisi yangu ya kubangaiza kujipatia angalau mlo mmoja nilisikia rafiki yangu akijadiliana na jamaa mmoja hivi simjui ambaye anaonekana ni mtu mzito ana uongozi fulani hivi ,alikuwa alipigwa stori kuhusiana na mchongo huo na njama gani zilizopo nyuma ya pazia mimi nilipuuza nikawa naendelea na shughuli zangu nilidhani kuwa ni chai nimeshangaa leo kukuta huu uzi sasa nimepata mzuka kwenda kijiweni nikamchimbe jamaa anipe za ndani nije kufungulia uzi kuhusiana na swala hilo...

Maghayo Satoh Hirosh
 
Nimepishana na hizo bus mitaa ya kigamboni Hadi nimeshangaa jinsi mabus yanavyopata shida kupishana
 
mimi nahisi wanataka kupanuwa mji mana kijichi kupo kiswaz sana hata costa zilikuwa adimu.
 
Tunasubiri kwa hamu mrejesho
 
Hiyo stendi kuhamishiwa hapo ndani yake kuna siasa nyingi na michongo ndani yake kuna watu wamejiamulia kwa maslahi yao na kuwakomoa

Haina mantiki stendi ya magari makubwa kuondolewa toka barabara kuu ya Kilwa Road jijini Dar es Salaam na kupelekwa ktk mazingira ya makaazi ya watu ndanindani kabisa.

Huko wasafiri wanatakiwa kufika alfajiri kukiwa na kiza pia wanawasili jioni hivyo kuvuruga utaratibu wa mipango miji na kusababisha athari za mazingira kwa kelele na pilikapilika nyingi ktk sehemu iliyopangiwa juzi tu kuwa makazi ya mfano ya watu.

28 June 2021

Alichokisema RC Makalla Baada ya kutinga Soko la Mbagala - Kijichi​

 
Sasa mbona leo ni tarehe 17 na bado barabara ni nyembamba vilevile na magari yameanza kupita na shida imeonekana? Marekebisho gani wamefanya?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Inamana serikali haina eneo along kilwa road mpka kupekeka stend ya magari ya kwenda kusini huko kijichi mafichoni.?

Msimu wa korosho umewadia.

#MaendeleoHayanaChama
 
🤔🤔🤔
 
Oya Maghayo mwamba ulimwita na amejibu vizuri kabisa.

Mkuu adriz tunasubiri mrejesho wa za ndaaaaani kbs!!

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
mimi nahisi wanataka kupanuwa mji mana kijichi kupo kiswaz sana hata costa zilikuwa adimu.
Unaongelea kijichi gani hiyo ya kiswazi mkuu?

Do your homework again!! Kijichi ina mtandao mkubwa wa barabara na ni ushuani kuliko sehemu yoyote ya wilaya ya Temeke.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Apewe mara ya pili? Kuna mwarabu wa oman amenunua eneo hilo anataka ajenge kiwanda cha kondom.
Hiyo ni kuimpliment ile kauli ya hangaya ya kupunguza kuzaa sana kwa vitendo.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] lile ni eneo la mtu binafsi tangia zamani jmn.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…