Huyu Mungu hatakiwi awe wa kutetewa na watu kuhusu uwepo wake. Ni jukumulake kujithibitisha kwamba yupo.
Nilishawahi kuandika hapakwamba hata wale tunaoiamini Biblia, kuna mtu anaitwa Tomaso, aliambiwa Yesu kafukuka, akasema haamini, hadi akaambiwa aende amshike Yesu kwenye makovu ya misumari, akajiridhisha, lakini bado hakuambiwa amekosea licha ya Yesu kusema heri watakaoamini bila kuona. Namaanisha kuna vitu lazima mtu ajihakikishie mwenyewe kama alivyofanya Thomao.
Wapili ni Gideon, na yeye aliambiwa akapigane, akaweka ngozi nje akasema endapo kutakua na umande ngozi isilowane basi atajua kweli Mungu atakua pamoja nae, alifanya kama majaribio mawili kupata ishara kwamba Mungu atakua pamoja nae huko vitani.
Narejea hapa
Kiranga amewahi kusema huyo Mungu kama yupo na anaweza kufanya chochote aniondoe kesho nisiwepo, iwe kwa kufa au kwa chochote (sikumbuki vizuri lakini ilikua kitu cha aina hiyo). Sasa kama muhusika mwenyewe amepewa ajidhihirishe kwa mtu anaetaka kuona uwepo wake hajafanya hivyo, kubishana na mtu asiyeamini uwepo wake kwa maneno matupu ni kazi ya ziada ambayo kimsingi nafikiria hakuna mtu anaiweza.
Ndio maana kila mara nasema, ukilenda kisayansi/logic havikai chungu kimoja na imani (Nashukuru pia Kiranga hana shida kabisa na Imani wala wanaoamini Mungu yupo ila pale unapotaka kuthitisha kwamba yupo kwa logic ndio tatizolinaanza hapo).
Na kwa faida ya wale wanaoamini uwepo wa Mungu, kama hauwezi kuelezea uwepo wa Mungu, jaribu kupitia tena juu ya kile unachokiamini. Hii kwa upande mwingine itasaidia kujenga kujifunza na kufuatilia juu ya unachokiamini.