Stephen Hawking's Final Book Says There's 'No Possibility' of God in Our Universe

Wapi naaminisha watu? Na inakuwaje mtu mmoja akamuaminisha mwingine?

Aanayeaminisha inakuwaje asisitize uchunguzi na uthibitisho badala ya imani?
Huwa tunaomba uthibitisho ila tunajibiwa kuwa kisichokuwepo hakithibitishiki,ndio maana nakwambia unachofanya ni kuwaaminisha watu kuwa hakuna Mungu na wapo wengine huamini.
 
Thibitisha Mungu yupo.

Thibitisha roho ipo.

Thibitisha pepo ipo.

Nijue unasema kweli, na si uongo.
Nasikiaga watu wanasema huwa wakilala wanaota ndoto..Mimi sjawahi kuota ndoto..kiranga ushawahi ? Kama umewahi kuota ndondo nidhibitishie.
Ukithibitisha hili naamini utapata majibu ya maswali yako ya kudhibitisha uwepo wa mungu(extra dimensional being)
 
Ni uchunguzi gani uliyofanyika wa kwenda kumsaka Mungu na majibu yakawa hayupo? Maana huku kusema Mungu angekuwepo ingekuwa hivi sijui isingekuwa vile haiwezi kuwa fact.

Sasa wewe umetumia nini kusema hayupo?
Eti kaona kwa sababu tunakunya baasi mungu hayupo
 
Howking ni mtu nyuma ya mtu mwengine ambae ni mpotoshaji(illuminati)..wanatuaminisha Yale asemayo ni yake kumbe sio.
 
Yeye katoa hoja zake juu ya utetezi wa anachokiwaza.... Ukitaka kupinga basi na wewe toa zako ili uende sambamba na unachokiamini.


Usiwe km nyumbu... Kukubar kubari kila kitu bila hoja au ushahid wowote.... Utadanganywa na kufanywa vibaya saana.

Binafsi niko upande wa hawking muda saana..... Ila nina maswali mawili yanayonifanya nisiame mazima......

Nikiyapatia tu ufumbuzi... Nitakuwa kwa hawking 100%
 
Nimemuumba binadamu kutoka kutowepo hadi kuwepo
 
Sidhani kama elimu ya dunia hii inaweza kuelezea uwepo au kutokuwepo kwa Muumba wa dunia hii.

Kwa maaana wote tumekuja katika dunia hii tukaikuta kama ilivyo. Hakuna aliyeshuhudia uwekwaji wa misingi ya dunia hii.

Kwa kuwa hakuna wenye physical evidence, wote tunaishia kwa theoretical evidence, basi ni vyema ile inayo suppotiwa na watu wengi ipewe kipaumbele zaidi ambayo ni imani inayofundishwa zaidi kwa mifumo ya kidini.

Kwa uelewa wangu sidhani kitu kilichopo ndani ya dunia hii kilikuwepo by coincidence, no there must be an engineer. Sasa huyu engineer wa huu kwa mafundisho ya kidini tuna amini kuwa alikuwa ni MUNGU.
 
Ni uchunguzi gani uliyofanyika wa kwenda kumsaka Mungu na majibu yakawa hayupo? Maana huku kusema Mungu angekuwepo ingekuwa hivi sijui isingekuwa vile haiwezi kuwa fact.

Sasa wewe umetumia nini kusema hayupo?
Logical consistency.

The same thing that makes your question demand an answer.

Without logical consistency, a question does not need an answer.

If you need an answer to your question, you uphold logical consistency.

You uphold the logic that disputes the existence of God.
 
Nimeuliza kuna uchunguzi uliyofanyika wa kumsaka Mungu na majibu yakawa hayupo? kinyume na hapo tutaendelea kubishana kwa kila mmoja kutetea msimamo wake.
 
Kama Mshana Jr
Yule mchaw
 
Huyu Mungu hatakiwi awe wa kutetewa na watu kuhusu uwepo wake. Ni jukumulake kujithibitisha kwamba yupo.
Nilishawahi kuandika hapakwamba hata wale tunaoiamini Biblia, kuna mtu anaitwa Thomaso, aliambiwa Yesu kafukuka, akasema haamini, hadi akaambiwa aende amshike Yesu kwenye makovu ya misumari, akajiridhisha, lakini bado hakuambiwa amekosea licha ya Yesu kusema heri watakaoamini bila kuona. Namaanisha kuna vitu lazima mtu ajihakikishie mwenyewe kama alivyofanya Thomao.

Wapili ni Gideon, na yeye aliambiwa akapigane, akaweka ngozi nje akasema endapo kutakua na umande ngozi isilowane basi atajua kweli Mungu atakua pamoja nae, alifanya kama majaribio mawili kupata ishara kwamba Mungu atakua pamoja nae huko vitani.

Narejea hapa Kiranga amewahi kusema huyo Mungu kama yupo na anaweza kufanya chochote aniondoe kesho nisiwepo, iwe kwa kufa au kwa chochote (sikumbuki vizuri lakini ilikua kitu cha aina hiyo). Sasa kama muhusika mwenyewe amepewa ajidhihirishe kwa mtu anaetaka kuona uwepo wake hajafanya hivyo, kubishana na mtu asiyeamini uwepo wake kwa maneno matupu ni kazi ya ziada ambayo kimsingi nafikiria hakuna mtu anaiweza.

Ndio maana kila mara nasema, kisayansi/logic havikai chungu kimoja na imani (Nashukuru pia Kiranga hana shida kabisa na Imani wala wanaoamini Mungu yupo ila pale unapotaka kuthibitisha kwamba yupo kwa logic ndio tatizo linapoanzia).

Na kwa faida ya wale wanaoamini uwepo wa Mungu, kama hauwezi kuelezea uwepo wa Mungu, jaribu kupitia tena juu ya kile unachokiamini. Hii kwa upande mwingine itasaidia kujenga kujifunza na kufuatilia juu ya unachokiamini.
 
Ukitaka kutopata hitimisho kwa jambo lolote, hata uwepo wako wewe mwenyewe kama ni kweli upo au si kweli, unaweza kutopata hitimisho.

Mimi si kwamba sitaki kutopata hitimisho juu ya hili jambo.

Au contraire! Nataka sana tu.


But the issue of god’s existence or non existence is a bit different, though.

On the one hand, I acknowledge all of the inconsistencies.

On the other, I’m like hmm...how do we know for certain, though?

The whole thing is a big old mystery that I believe no one has figured it out yet.

So until then, I’ll remain open minded....

I wont wholly dismiss it. But neither am I going to fully accept it.
 
Shida n kuwa tunataka kuthibitisha uwepo wa Mungu kama vile Mungu ni kitu.Stephen anasema, Laws of Nature, Laws of Science - If you like,you can say the laws are the work of God,but that is more a definition of God than a proof of his existence.Pia anasema- the only role for an all- powerful deity might be setting the initial conditions of the universe so that those laws could take shape. Naona Mungu ameziunda hizo laws of science na kuziweka chini yake hatuwezi kuthibitisha uwepo wake kwa kutumia hizo laws. Science nayo haijakamilika mpaka Leo kuna vitu vinagundulika na kuna nadharia zinathibitishwa kuwa wrong.Kwanza Stephen ana IMANI na science na proof zake ikiwamo the big bang theory halafu anataka athibitishiwe uwepo wa Mungu kwa kutumia nadharia anazoziamini yeye which is wrong , God the Creator is above what he created hivyo sisi wengine tunathibitisha uwepo wake kwa kutumia nadharia zingine nje ya science laws ambazo tuna IMANI nazo. Stephen anasema ....If you like, you can say the laws are the work of God sasa ubishi ukoje hapa kwani naye amefika mwisho.Ukishasema....the only role.....might be setting the initial conditions of the universe so that those laws could take shape,tunajiuliza tena what role is there for God?Tunadhani Mungu akiwa kazini kunatakiwa kuwe na perfection.Gödel showed us that you really cannot prove anything logically without assumptions. But why assumptions? Wenzetu wanaweza andika hayo mabuku ya kupinga uwepo wa Mungu kutafuta pesa na ujiko lkn moyoni wana mashaka.Atheist na Agnostic hawatakiwi kubishana kuwe na " modus vi- vendi" kwa kutumia imani au principles tofauti za kujenga hoja n dhahiri hakuna mshindi.Mmoja kasema sawa kabisa God exists but not in a comprehensible form. If God becomes comprehensible then he is not God... It is therefore logical to say that human mind has no ability to comprehend the existence of God rather we can only comprehend our own existence to a limited degree. Kuna binaadamu wana hasira na Mungu kutokana na changamoto wanazopitia wanadhani kama yupo alipaswa kuumba na kuuendesha ulimwengu wanavyodhani wao.Ulimwengu ulivyo ndio matakwa ya Mungu na kila kitu na jambo lina makusudi yake.
 
Aaaamen [emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Sana tu mkuu, wiki mbili zilizopita milikuwa ninasibiri maamuzi is a ajira. Baada ya interview Sauti iliniambia hili swala linahitaji Salamu Maria 50. Nilianza kusali na baada ya siku mbili nilipata email ya hongera. Ni Mungu sana tu mkuu
Ulishinda kwasababu ya uwezo,
Hata wenzio nao walisali lkn hawakushinda.

Kama sivyo basi Mungu ni mbaguzi na mpendeleaji, kwanini akuone we ni bora kuliko wengine?

Mimi sijawahi kosa Interview, huwa tunashindwana mshahara tu, lkn sijawahi sali hata siku moja.

Nimefanya interview ya Sekretarieti ya Ajira, nikashinda ila kufika kwenye taasisi husika mshahara wa mbuzi nikaacha.

Sijawahi muomba mungu zaidi ya kujiamini tu.
 
Nimeuliza kuna uchunguzi uliyofanyika wa kumsaka Mungu na majibu yakawa hayupo? kinyume na hapo tutaendelea kubishana kwa kila mmoja kutetea msimamo wake.
Ngoja nikusaidie kuweka tena kitu ulichouliza hapa, kama umesahau.

Umeuliza hivi

Ni uchunguzi gani uliyofanyika wa kwenda kumsaka Mungu na majibu yakawa hayupo? Maana huku kusema Mungu angekuwepo ingekuwa hivi sijui isingekuwa vile haiwezi kuwa fact.

Sasa wewe umetumia nini kusema hayupo?

Jibu ni ndiyo.

Maelezo yote hayo yanajibu swali lako la mwisho "sasa wewe umetumia nini kusema hayupo?

Nakujibu swali ulilouliza halafu hata kusoma jibu hujui?

Hapo kuna haja gani ya kujadiliana nawe?

Nikikuambia usome "Philosophy of Religion:An Anthology" sehemu inayohusu "The Problem of Evil" utaweza?

Soma kitabu hiki naweka attachment kwa kujielimisha zaidi, hususan "PART IV The Problem of Evil page 276"
 

Attachments

Usomi mtupu.

Kuna mtu mmoja, nafikiri ni Cromwell, alisema, anashukuru wasioamini uwepo wa Mungu, kwa sababu kwa kupitia kuwasoma wao, anaimarisha imani yake.

Wwaamini wa kweli wanatakiwa kunishukuru mimi, kama Mungu wao ni wa kweli na yupo, maana ninaweza kuwaimarishia imani zao na kuwafanya wamuelewe zaidi Mungu.

Umesema vizuri kwamba mimi sina tatizo na wanaoamini Mungu. Najua ustaarabu, najua faragha ambayo imani inapewa, ndiyo maana katiba ya Tanzania inatoa uhuru wa kuabudu, na hili si jambo lililo katika katiba ya Tanzania tu, ni jambo lililo katika katiba nyingi sana, ni jambo lililopo hata katika haki za binadamu kama sehemu ya "The Universal Declaration of Human Rights" ya December 10 1948.

Sina tatizo na wanaoamini Mungu yupo. Hawa mtu akiwabana wasiamini atakuwa anaingilia haki zao za msingi za kuamini wanavyotaka. Juzijuzi hapa Rais Kagame wa Rwanda alianza kusema anataka wachungaji wote Rwanda wawe na degree, nikapinga hili kama kuingilia uhuru wa kuamini.

Tatizo langu ni kama ulivyosema, kwamba watu anasisitiza Mungu yupo as a fact, not as an article of faith.

Hapo ndipo tunaangalia logic ya kuwepo huyo Mungu tunaona hai make sense, in fact ina contradiction inayoonesha kwamba Mungu huyo hawezi kuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…