The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Baadhi ya dini zina miungu tofauti tofauti, ila Mungu wa kweli ni mmoja tu. Kinachopelekea watu waamini miungu ni kukosa ufahamu sahihi sasa baada ya kuwa wame-detect uwepo wa Mungu yule ambaye ni mmoja tu. Lakini at least hata yule anayeabudu miungu, anasignify kwa kiwango kikubwa sana kwamba kuna Mungu wa kweli ila ameshindwa tu kwa namna moja ama nyingine, ku-capture the right signal!
Ndio hapo sasa matatizo yanapoanzia, huyo Mungu wa kweli ni yupi, kwanini inakua shida au vigumu kumjua hadi watu watangetange kwenda kwa miungu wengine? Nilitegemea Mungu wa kweli ajulikane na wote kisha waamue kumsadiki au kutokumsadiki.
Kwa hali ilivyo sasa, unaweza kutumia tool gani au mfumo upi kuthibitisha kwamba Mungu anaeabudiwa na hawa jamaa ndio Mungu wa kweli? Hauoni kwamba hii hali ikiendelea inafanya kila anaemwabudu Mungu wake aseme kwamba ndio Mungu wa kweli na wengine ni wa uongo?
Nimeshaweka wazi, sipo kwenye kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu japo mjadala ndio umejikita hapo. Tumefikia hapo kwenye kujua huyo Mungu wa kweli ni yupi na namna gani ya ku-capture the right signal!
Ahsante