Makundi mbalimbali ikiwemo vyama vya siasa ndani na nje ya nchi, wasanii, taasisi za dini, mabazi na wanamichezo ni kati ya wanaohudhuria mkutano huu wa CCM unaofanyika Dododom.
Rais Samia amefungua mkutano huo kwa kuanza na hotuba ya ufunguzi, ambapo mbali na kuongelea maendeleo ya chama kwa ufupi ametoa onyo kwa wanachama wanaeonda majimboni kwa lengo la kufanya kampeni waache kufanya hivyo mara moja.
Pia awaonya CCM kuwa na makundi wakati wa kuteua wagombea.
Rais Samia awahimiza CCM kuhimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na wale ambao wanahitaji kuboresha taarifa zao kufanya hivyo.
====
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar amesoma azimio la kikao cha NEC kilichofanyika 18/1/2025 Dodoma ilipokea na kujadili mapendekezo na kamati kuu ya ccm taifa kuhusu mrithi wa Kinana, baada ya kujadili mapendekezo hayo Halamshauri kuu ya CCM imemteua Steven Wassira kuwa ndiye mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara ili kupigiwa kura.
===
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichoketi leo tarehe 18 Januari 2025, Dodoma, kuelekea Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Leo tarehe 18 na 19 Januari, jijini Dodoma.
#KaziIendelee