Stephen Wasira amtembelea na kumjulia hali Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati Baba wa Taifa, Februari 18, 2026

Stephen Wasira amtembelea na kumjulia hali Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati Baba wa Taifa, Februari 18, 2026

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg. Stephen Wasira, amemtembelea na kumjulia hali Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2026.
WhatsApp Image 2026-02-18 at 15.38.30 (1).jpeg

WhatsApp Image 2026-02-18 at 15.38.29.jpeg

WhatsApp Image 2026-02-18 at 15.38.30.jpeg
 
Well done makamu mwenyekiti wa CCM Taifa, mh.Stephen Masatu Wasria,
Unafanya kazi nzuri sana baba, :KasugaYeah:
 
Sijui kama alifika kaburini alipolala Mwalimu kutoa heshima. Nakumbuka Polepole alisema na nukuu '' ... sijawahi kuona Mzee mpumbavu kama huyu! alipogeuka nyuma akakuta Mwalimu ana mtazama, akaondoka bila kuaga. Tangu hapo hakuwahi kuonana na Mwalimu hadi anafariki' mwisho wa nukuu
 
Makongoro alisema tangu anatoka shuleni Tabora school, likizo Wasira yupo.

Hadi hapo alipo Makongoro ,bado Wasira yupo.

Hivi sijui kuna watu hawana kupumzika ndio maana hata juzi anaongea kwa fikra zake anafikiri anaongelesha watanzania waliopo 1970.
 
Huyu Wasira sasa amekuwa balaa nyingine wakati huu.

Huyu mama huenda huu mwaka hauishi!
 
Hivi sijui kuna watu hawana kupumzika ndio maana hata juzi anaongea kwa fikra zake anafikiri anaongelesha watanzania waliopo 1970.
Hapana. WaTanzania waliokuwepo 1970 hawakuwahi kuwa na fikra za aina hizi zilizopo sasa, hata kwa kipimo cha aina yoyote ile.
Pamoja na umaskini wake mkubwa sana, Tanzania ilikuwa na heshima na fikra za hali ya juu sana.

Sasa sijui kwa nini watu huwa wanapenda kufanya rejea hii potofu kabisa!

Au kwa vile hapakuwepo na internet na mitandao ya kijamii; jambo ambalo ni tofauti kabisa.

Tafuta gazeti lolote la wakati huo, na usome yaliyokuwa yanajadiliwa kwa akili kubwa kabisa!
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg. Stephen Wasira, amemtembelea na kumjulia hali Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2026.
halafu ipite sku mbili bibi wa watu akate moto ili muandae mazishi ya kitaifa kula hela zetu! koma we mzee muache bibi yetu
 
Back
Top Bottom