The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Stephen Wasira amezungumza na wanachana na viongozi wa Chama wilayani ileje mkoani Songwe akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani humo.
Akizungumza na wana CCM hao katika Ukumbi wa Seselembe, Ileje leo, Machi 16, 2025, Wasira amesema Chama kinaingia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kikiwa hakina wasiwasi wa kushinda kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Pia soma Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Chama Cha Mapinduzi kinaingia katika uchaguzi kikiwa na hakika ya ushindi kutokana na kazi kubwa ya kuleta maendeleo iliyofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, tunavisihi vyama vingine vya siasa viingie katika uchaguzi huu na wananchi endeleeni kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura," amesema Wasira.
Awali baada ya kuwasili wilayani humo akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake kwa Mkoa wa Songwe, Wasira alipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na hali ya siasa ya wilaya hiyo, kisha kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la kitega uchumi cha Chama wilaya ya Ileje na kuongoza uchangiaji wa ujenzi wa jengo hilo.
Chanzo Jambo TV