BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Wasira ameyasema hayo Agosti 31, 2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa Chama hicho wakati wa kikao cha ndani ambapo ametumia kikao hicho kuelezea mchakato wa kura za maoni hadi kupatikana walioteuliwa kugombea ubunge na udiwani,
"Kazi yetu ni kuhakikisha mtu ashinde... kwahiyo muache kugawanyika kwasababu kura za maoni zimeshapita hivyo tugawanyike kwa ajili ya zile.
"Hakuna hoja hapo bali kwa sasa hoja ni CCM kupata dola na hayo mengine yote tunayoyafanya yote ni mchakato wa kufikia lengo la kupata dola.Hivyo msipoteze lengo kwasababu ya mchakato wa ndani, huo ujumbe wangu wa leo,"amesem Wasira
Amefafanua uongozi huo na kazi ya kusema nani anakuwa na nani hawi ni kazi mbaya na ngumu na amewaambia kutokana na nguvu ya ubinadamu maana wao sio malaika na mpaka hapo walipofikia ni vema wakapongezwa maana kazi yenyewe ngumu.
"Sasa wewe unanung'unikia nini? Ni kazi ngumu lakini nataka niwaambie walioteuliwa sio kwamba wao ni bora kuliko wasioteuliwa, sio kweli ila hili chama lina watu wengi halafu wanauwezo.Hata ukiondoa walioteuliwa ukaamua kupata wwngine tena watakuja wengi na wenye uwezo zaidi ya hawa."