Stephen Wassira: Watanzania wamemuelewa na kumuunga mkono Rais Samia; wanasema kiwango chao cha furaha kimeongezeka

Stephen Wassira: Watanzania wamemuelewa na kumuunga mkono Rais Samia; wanasema kiwango chao cha furaha kimeongezeka

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Mzee Wasira ambaye amekuwa waziri katika serikali tangu uhuru mpaka serikali ya awamu ya nne ya JK amesema Kiwango cha furaha kwa Watanzania kimeongezeka. Ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na Azam TV. Aidha amesema baada ya masikitiko ya muda mfupi kufuatia kifo cha Magufuli nchi imerudi kwenye reli baada ya hotuba za Rais Samia Suluhu Hassan.

Kumbe furaha hii pia imetamalaki ndani ya CCM na wapambe wanafiki wa Magufuli!

===

Akizungumza Apr 9, 2021 kwenye kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na Azam TV, Mzee Wassira amesema:

"Namwambia nini Rais? Namtakia heri. Namtakia heri aongoze nchi yetu vizuri. Na kitu kimoja ambacho ningependa Rais ajue ni kwamba: kwa hotuba hizi tu, Watanzania wengi wamemuelewa na wanamuunga mkono. Wanasema kiwango chao cha furaha kimeongezeka; kwasababu tumesikitika [kufuatia kifo cha Rais Magufuli] lakini tumerudi kwenye reli."
 
Title imekaa kichonganishi tofauti na maelezo.

Sijamsikia Wasira lakini maelezo yanaonesha kuwa Watu wamepata matumanini mapya kwa Mama Samia baada ya machungu ya msiba.
 
Mzee Wasira ambaye amekuwa waziri katika serikali tangu uhuru mpaka serikali ya awamu ya nne ya JK amesema Kiwango cha furaha kwa Watanzania kimeongezeka tangu kifo cha Rais Magufuli. Ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na Azam TV. Aidha amesema baada ya masikitiko ya muda mfupi kufuatia kifo cha Magufuli nchi imerudi kwenye reli baada ya hotuba mbili tu za Rais Samia Suluhu Hassan.

Kumbe furaha hii pia imetamalaki ndani ya CCM na wapambe wanafiki wa Magufuli!
Kwa wastani ni kuwa sasa hivi watanzania wameongeza siku za kuishi
 
Watu wanashindwa kujua, kuwa furaha huweza letwa na matumaini. Furaha iliondoka kwa sababu hapakuwa na matumaini. Sasa watu wana furaha kwa sababu Kuna tumaini aidha uwepo wa ajira, kuthaminiwa,kupanda cheo au nafasi si kwa sababu sio wa Kanda,kabisa au dini fulani,kulipwa deni, kupanda mshahara,kuwa huru kueleza maoni yake,kuwa huru bila vitisho,kuwa huru katika kazi yake,kutodhulumiwa Mali au pesa na serikali,kulipwa mafao/pensheni stahiki n.k

Lala salama Mwamba.
 
Mzee Wasira ambaye amekuwa waziri katika serikali tangu uhuru mpaka serikali ya awamu ya nne ya JK amesema Kiwango cha furaha kwa Watanzania kimeongezeka tangu kifo cha Rais Magufuli. Ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na Azam TV. Aidha amesema baada ya masikitiko ya muda mfupi kufuatia kifo cha Magufuli nchi imerudi kwenye reli baada ya hotuba mbili tu za Rais Samia Suluhu Hassan.

Kumbe furaha hii pia imetamalaki ndani ya CCM na wapambe wanafiki wa Magufuli
Duh! Hata huyu sasa ni mtu wa kusema na kusikilizwa! Anaisemea nchi, nasi tunafurahia.
 
Back
Top Bottom