Steve Nyerere: Mchungaji Peter Msigwa nimemchukulia mwanamke ndio maana anaendekeza ugomvi na wasanii kutangaza utalii nchini

Wasanii ni vikaragosi vya CCM, kwanini walipwe kwa hela zetu wakati hawaajiriwa kihalali.
Hivi huyu Steve amepata wapi Ujasiri wa kumsema hadharani Mchungaji, Baba, Mume na Mbunge wa Wananchi Kwa kasfa mzito kama hii. Msigwa ni Waziri Kivuli utaliii alikuwa anatia Mawazo yake Bungeni.
 
Mwelezeni Huyo msanii steve mangele (sio sahihi kutumia jina Nyerere kwa huyu kwani ni kulidhalilisha) kuwa Mchungaji Msigwa Peter anayo kinga ya kibunge kwa kila anachoongea akiwa ndani ya Bunge, hivyo achunge kauli zake zisijesababisha akachukuliwa hatua na Mchungaji Msigwa kwa haya anayoropoka mitaani
 
Labda hukumuelewa mchungaji msigwa au hukubahatika kuona huo mchango wake. Alichokuwa anashauri ndugu msigwa ni kwa waziri badala ya kuhangaika na wasanii wa ndani tu atumie na wasanii wa nje (celebrities) kama wanavyofanya Rwanda ili kutangaza utalii kwa mataifa ya nje ambayo ndiyo kazi yake ili kuongeza idadi ya watalii wa nje.
 


!
!
kwa speech hii tu anaonekana hafai kuwa balozi wa utalii huyu
 
Hapo kanuni inatakiwa ifanye kazi mbunge analindwa na kanuni Kwa yote anayosema ndani ya Bunge.
 
Msigwa alikua sahihi, Steve Nyerere hata aposti mara 700 kuleta mtalii hataweza..
 
Ila kwakweli tumefika pabaya sana.yani kila mtu anaongea tu kumtukana mwenzake? Sasa kosa la msigwa lilikuwa nn pale? Si alishauri tu jamani?
Nahuyu Steve anamtukana mbungwe kwann

Sent using Jamii Forums mobile app
Wabunge wa Upinzani Awamu hii wameondolewa Heshima na hakuna wa kuwatetea. Yeyote Tu anaweza kuwatukana hadharani akijinadi anaisapoti Serikali. Si haki Mbunge ana title Mheshimiwa tena aliopewa na Wananchi Nobody Anatolka kuwakashifu for Fame. Mhe Msigwa pole Sana.
 
Ila Tanzania raha sana ukiwa na jina kidogo tu unaweza kufanya press conference ukaongea upupu wako bila tatizo lolote kabisa
 

Huyu na ni mpuuzi tu.
Aende bungeni bungeni akapinge hiyo hoja.

NB:
Kutokana na tabia yake iwe kweli au kazuga, hili la kugombea wanawake linamuondolea heshima yeye na wasanii wengine. \inaonesha wasanii ni wahuni na wanaenndekeza mambo ya ngono/uzinzi na ukahaba
 

katika hili Msigwa hoja yake ilikuwa inasimama katika utaratibu na kama ilivyokuwa huko nyuma, kabla ya awamu ya 5, na alikuwa yuko sahihi; kitu ambacho si lazima kifanyike hivyo hata kwenye awamu hii. Kwa kipindi hiki cha JPM, ukiamua kutumia utaratibu wa zamani kwamba wewe ni Waziri unasimamia Sera, hivyo ukawa unakaa ofisini hufanyi hata ziara wakati Tandahimba watu wanalalamika hawana maji, anakutumbua within seconds.

Mawaziri kutatua kero za wanachi LIVE haimaanishi kuwa wameacha kusimamia sera, au kwamba wanafanya kazi kwa operation. Kwani mimi kama ni Waziri, kutatua kero za wananchi nikiwa niko kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo, KUNANIZUIAJE KUSIMAMIA SERA? Je, sera inasimamiwa tu kwa kukaa kwenye dawati nikiwa ofisini? Aache kuwachangaya mawaziri na mimi ninachelea kusema kuwa atakayefuata ushauri wa Msigwa anaweza akapoteza nafasi yake kirahisi tu kwa sababu kwa kipindi hiki cha JPM, utendaji kazi wa aina hiyo ni kama hauwezekani, ilikuwa huko nyuma! Sera naweza hata nikasimamia hata nikiwa nimekaa ofisini mwaka mzima, isipokuwa sasa MATOKEO ya utekelezaji wake ndiyo utakuwa mgogoro. Ndiyo maana tulikuwa tunapata matatizo huko nyuma ambayo tumeshaanza kuyaondoa sasa, kwa sababu tulikuwa tunastick na kanuni za kwenye maandishi ambazo katika uhalisia, zilikuwa hazitunufaishi na chochote. Huko ndiko Msigwa anataka turudi?
 
Huyu jamaa aliwahi kuwa msanii wa kitu gani?
 
Wazo lako limekaa vema ila tatizo nchi yetu kila kitu kinafanyiwa siasa tu, ifike muda tuache siache uchwara tufanye kazi....yan mpaka Wakenya jirani zetu wana tupiku....
 
Sijawahi kumchukulia serious Stivie Nyerere aka MZEE WA FUTUHI.
 
Yaani wote mnamuatack Steve nyerere.
Msameheni yule ni mgonjwa Wa akili anafahamika,mnachofanya ni unyanyapaa
 
so ametukana wanawake wote ....arudishe pesa za msiba wa mtoto wa muna na kayumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…