Stiegler Dam, Taasisi za Kimataifa Vs. Magufuli

Stiegler Dam, Taasisi za Kimataifa Vs. Magufuli

Kwa hili ,kwa hili, kwa hili Jua liwake au Mbala mwezi, au nyota mvua inyesha ,au mawingu au barafu zianguke ; Bwawa la Stiglers gorge lazima lazima lijengwe ili tupate umeme wa uhakika.

Mazimgira ni ya kwetu na Watanzania ni Sisi pia tunao bitaji umeme kwa kiwango kikubwa sana ili kuleta maendeleo yetu wenyewe.

Hatutawasikiliza wanamazingira nje ya miopango ya serikali.

Wana mazingira wanatumiwa sana na makampuni ya nje kuhujumu maisha ya watanzania.
Mfano Suala la Barabara ya lami kupitia mbuga ya Serengeti limeturudisha nyuma sana na kuifanya nchi yetu iwe imeparalize upande ule wa mpakani na Kenya wakati upande wa Kenya uko active sana kimaisha ya wananchi. Hii yote ni janja ya wakenya kufanya eneo letu kuwa la maajabu wakati la kwao likiwa lakuingiza kipato na mzunguko mkubwa wa fedha kwa wananchi wao. Pia wamekomalia sana ujenzi wa kiwanda kikubwa cha magadi.
Mfano mwingine ni suala la kupamabana na mazalia ya mbu wa malaria .Hawa watu wa mazingira wanafadhiliwa na wamiliki wakubwa wa viwanda vya madawa ya malaria ili malaria zisiishe waendelee kupata soko la dawa zao za kuharibu mazingira ya miili yetu kwa kwa unafiki ya kulinda mazingira. Mbu miaka nenda rudi wamebaki kwa ajili ya kuwanufaisha watu wa mazingira na watu wa miradi ya malaria huku malaria zikizidi kuathiri jamii.
Hapa napo pana hitaji maamuzi magumu ya kuangamiza mazalia ya mbu " jua liwake" au "mvua inyeshe."

Huko Stiglers gorge Kwa akili ya kawaida unapoweka reserve kubwa ya maji kwa kujenga bwawa kubwa unaongeza mvuke hewani na hatimaye ongezeko la mvua.
Pia tunaweza kufuga samaki wengi na baadae kuwa na uvuvi mkubwa na kuanzisha kiwanda cha samaki. Wanyama tunaweza tukaamua kuwafuga hata majumbani kwetu hakuna shida.
Na ukweli ni kuwa miaka mia mbili ijayo wanyama wa porini watakuwa wanapatikana kwenye mazoo na sio huko porini kwa kuwa ninadamu atakua ameendelea zaidi kiviwanda na teknolojia. Hivyo hatuna haja ya kubakia na umaskini kwa kisingizio cha kulinda mazingira ya wanyama huko porini zaidi tujenge uwezo wa kiuchumi ili hao wanyama tuwafuge majumbani kwetu kama ilivyo mbwa ,kanga na Tausi n.k. Hata india wanafuga tembo na tiger.

Magufuli songa mbele.
Kwa hili nakuunga mkono 100%.
Ukimaliza hapo hamia kwenye kilimo. Hatutaiki njaa.
 
Lengo lao sio mazingira bali wanapenda sana kutuletea ma iptl
 
Wazungu hawana shida ya umeme... Now wanakuja na their conservanist theories. Never.. !

Iwe jua, iwe mvua lazima mradi ufanyike
 
Hata Trump amekataa kuwaamini wana mazingira kaamua makaa ya mawe lazima yachimbwe tu, kwanini Magufuli ashindwe? Acha tujenge bana ikileta athari haitatumika kwani sh. ngapi!!!!!!!!
Ni wapuuzi tu. Hawataki tujenge make wa naelewa fika tutajitosheleza kwa umeme na hatutawategemea tena kutuletea mitambo ya kipuuzi ya kutuuzia umeme kama zile ishu za IPTL.

Kama hawataki wanywe sumu, tunachimba na tunazalisha umeme kwa ajiri ya nchi yetu. Nchi ni yetu na Selous ipo kwetu.
 
Wakatafute soko la gas mamaeeee wanataka tuibia gas wazalishe nayo umeme watuuzie mamaa mke wko unalipa na mahari wazungu hawa mnao wabudu na kutembea na bendera zao kuwa wamebarikiwa wacha watuibie mmpenda wenyewe!!!
 
Kwa Fedha ipi?: Uhamisho Dodoma, Standard Gauge, Flyovers, Stiegle's Gorge Dam, . kila la heri.
Hapa ndio nami napata ukakasi, Ila kwa mambo ya mazingira kwa utawala huu wasahau.
 
Kwa hili ,kwa hili, kwa hili Jua liwake au Mbala mwezi, au nyota mvua inyesha ,au mawingu au barafu zianguke ; Bwawa la Stiglers gorge lazima lazima lijengwe ili tupate umeme wa uhakika.

Mazimgira ni ya kwetu na Watanzania ni Sisi pia tunao bitaji umeme kwa kiwango kikubwa sana ili kuleta maendeleo yetu wenyewe.

Hatutawasikiliza wanamazingira nje ya miopango ya serikali.

Wana mazingira wanatumiwa sana na makampuni ya nje kuhujumu maisha ya watanzania.
Mfano Suala la Barabara ya lami kupitia mbuga ya Serengeti limeturudisha nyuma sana na kuifanya nchi yetu iwe imeparalize upande ule wa mpakani na Kenya wakati upande wa Kenya uko active sana kimaisha ya wananchi. Hii yote ni janja ya wakenya kufanya eneo letu kuwa la maajabu wakati la kwao likiwa lakuingiza kipato na mzunguko mkubwa wa fedha kwa wananchi wao. Pia wamekomalia sana ujenzi wa kiwanda kikubwa cha magadi.
Mfano mwingine ni suala la kupamabana na mazalia ya mbu wa malaria .Hawa watu wa mazingira wanafadhiliwa na wamiliki wakubwa wa viwanda vya madawa ya malaria ili malaria zisiishe waendelee kupata soko la dawa zao za kuharibu mazingira ya miili yetu kwa kwa unafiki ya kulinda mazingira. Mbu miaka nenda rudi wamebaki kwa ajili ya kuwanufaisha watu wa mazingira na watu wa miradi ya malaria huku malaria zikizidi kuathiri jamii.
Hapa napo pana hitaji maamuzi magumu ya kuangamiza mazalia ya mbu " jua liwake" au "mvua inyeshe."

Huko Stiglers gorge Kwa akili ya kawaida unapoweka reserve kubwa ya maji kwa kujenga bwawa kubwa unaongeza mvuke hewani na hatimaye ongezeko la mvua.
Pia tunaweza kufuga samaki wengi na baadae kuwa na uvuvi mkubwa na kuanzisha kiwanda cha samaki. Wanyama tunaweza tukaamua kuwafuga hata majumbani kwetu hakuna shida.
Na ukweli ni kuwa miaka mia mbili ijayo wanyama wa porini watakuwa wanapatikana kwenye mazoo na sio huko porini kwa kuwa ninadamu atakua ameendelea zaidi kiviwanda na teknolojia. Hivyo hatuna haja ya kubakia na umaskini kwa kisingizio cha kulinda mazingira ya wanyama huko porini zaidi tujenge uwezo wa kiuchumi ili hao wanyama tuwafuge majumbani kwetu kama ilivyo mbwa ,kanga na Tausi n.k. Hata india wanafuga tembo na tiger.

Magufuli songa mbele.
Kwa hili nakuunga mkono 100%.
Ukimaliza hapo hamia kwenye kilimo. Hatutaiki njaa.
Mkuu ata Israel waki tukataza!!!
 
Come rain or come shine, the project gonna be implemented.
Amen! let it be! come rain or come shine, the project will be implemented. this is our country and we will only stick to what is beneficial to us
 
Hao wanaojiita wanamazingira waache kuingilia mambo ya nchi yetu, yaani sisi tuishi Giza na tukose uwekezaji mbalimbali kisa hakuna umeme wa uhakika wakati tuna vyanzo vya maji vya uhakika vya kuzalishia umeme wakati huo huo wanatucheka nyuma ya pazia kuwa hatujui kutumia rasilimali zetu.

Nadhan wangekuwa kweli ni wapigania mazingira wangeanza na mataifa yao yaliyoendelea ambayo yana tumia nuclear power kuzalisha umeme+kuwa na maviwanda yanayochafua anga na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi duniani
Ndiyo maana Trump hataki kusikia mambo ya mazingira, yeye uchumi kwanza mengine baadae.
 
Tatizo wanamazingira wanaweza kuendesha kampeni chafu ya kususia utalii au kuzilazimisha serikali zao zenye kuchangia bajeti yetu kutubana kwa kuzuia raia wao wanaopanga kuja nchini kwa ajili ya utalii kama njia ya kutupiga presha ili tuachane na mradi, hii imekaa vibaya!

Hata hivyo ni bora tukakomaa likajengwa tu iwe mvua, iwe jua maana mradi huu ni ukombozi!
 
Kama gharama zote tutabeba wenyewe basi itajengwa, lakini kama tunasubiria senti ya mzungu, tusahau huo ujenzi. Au tuombe marafiki zetu wa ukweli "macho madogo" watupe hela!
 
Hao wanaojiita wanamazingira waache kuingilia mambo ya nchi yetu, yaani sisi tuishi Giza na tukose uwekezaji mbalimbali kisa hakuna umeme wa uhakika wakati tuna vyanzo vya maji vya uhakika vya kuzalishia umeme wakati huo huo wanatucheka nyuma ya pazia kuwa hatujui kutumia rasilimali zetu.

Nadhan wangekuwa kweli ni wapigania mazingira wangeanza na mataifa yao yaliyoendelea ambayo yana tumia nuclear power kuzalisha umeme+kuwa na maviwanda yanayochafua anga na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi duniani
Wewe umepatia sana na mi nasema ndo kwanza game limeanza. Nchi zote duniani zina angalia maslahi ya kiuchumi kwanza na mengine baadaye. Hao wazungu wako smart kwenye uhifadhi kwa sababu kwa aina ya uchumi na shughuli zinazofanyika kwa sasa katika nchi zao, hazipelekei kuharibu mazingira.
Lakini mujiulize kipindi wako katika stage ya industrial revolution Karne ya 19 hadi 20 waliiiharibu wao wenyewe dunia kwa kutumia kiwango kikubwa cha makaa ya mawe. Sisi Tanzania ndo kwanza tuna papasa papasa makaa yetu ya Kiwira hatujaanza vyema ya mchuchumaa, halafu watu a bid tunaharibu mazingira?
Nenda eneo la Ruhr Valley North Rhine Westphalia Ujerumani, Donbas Ukraine, Yorkshire UK, Pennsylvania USA, Nord Ufaransa, Wallonia Ubelgiji, Kuzbass USSR na Manchuria China, mtaona wenyewe walivyoharibu nchi zao.
 
Yani tuache chanzo cha umeme cha nne (4) kwa ukubwa barani Afrika, tutakuwa tu wendawazimu.
Wazungu wameshaendelea sana na sasa wanapigania kuachana na nishati ya nyuklia baada ya kuwa naye muda mrefu na kuichoka kwamba inaharibu mazingira, kwa hiyo sisi hatutawahi kupata uhondo wa umeme wa nyuklia? Let's think beyond the box.
 
Mkuu ata Israel waki tukataza!!!

Israel hawana maneno mana nao vile vile wamekatazwa kujenga makazi ukanda wa gaza lakini wameangalia maslahi ya watu wao na wameamua kuendelea na ujenzi.

Kwa hiyo na sisi tunaangalia maslahi ya watu wetu na nchi yetu japo kwenye uhuru wa kidemokrasia na maendeleo wametuzidi.
 
Wakome! Wamezoea kutuibia kupitia capacity charges ya mitambo yao ya kuzalisha umeme! Ni nchi yetu watukome kabisa! Rais Magufuli usirudi nyuma!
 
Wazungu wa ovyo sana! Wakiona mnataka kuinuka wanakereka sana! Kwani wanavyochimba madini na kutuachia mashimo hawaharibu mazingira?
Unajua inaudhi sana!
 
Back
Top Bottom