Stori gani uliwahi kusimuliwa kuhusu mchezaji wa mpira kumbe 'kamba'?

Stori gani uliwahi kusimuliwa kuhusu mchezaji wa mpira kumbe 'kamba'?

Kuna stori niliwahi kuambiwa na jamaa mmoja kuwa Bekham alikuwa anafanya mazoezi hata siku mbili mfululizo bila kupumzika akiwa nyumbani.

Kipindi hicho nilikuwa mdogo nikamuamini ila sasa nimekuwa nimemfata kumwambia yule jamaa achukue kamba yake sifungiki tena.
Kwamba siku za mechi za Ligi Daraja la Kwanza enzi hizi, eti Frank Kassanga "Bwalya" aliyekuwa beki wa Simba eti alikuwa anafuatwa baa anaingia uwanjani na anakiwasha kweli kweli akiwa amelewa!🤣🤣🤣🤣
 
Kuna stori niliwahi kuambiwa na jamaa mmoja kuwa Bekham alikuwa anafanya mazoezi hata siku mbili mfululizo bila kupumzika akiwa nyumbani.

Kipindi hicho nilikuwa mdogo nikamuamini ila sasa nimekuwa nimemfata kumwambia yule jamaa achukue kamba yake sifungiki tena.
Diego Maradona ndio mchezaji aliechezewa Rafu nyingi kuliko mchezaji mwengine yoyote yule duniani.
 
Kuna siku Diego Maradona aliamua kupiga chenga wachezaji wengine wote 21 waliobaki, wa timu yake na timu pinzani mpaka refa.
 
Aliekua kipa wa Yanga Bwana Juma Pondamali alidakaga mpira akauficha mgongoni ndani ya jezi kisha akatingisha nyavu kwa mkono, refa akaweka kati.

Baadae wanatafuta mpira uanzishwe kati hawauoni, akautoa mgongoni refa ikabidi abadili maamuzi.
 
Hii ya goalkeeper wa Colombia ina ukweli kidogo, huyo kipa alikuja na staili inaitwa butterfly katika kupangua mashuti.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Rene Higuita,
Style Inaitwa SCORPION KICK
images (19).jpeg
images (8).jpeg
 
Nakumbuka niliadisiwaga kwamba RONALDIHNO akikupiga chenga ya kisnake lazima kiuno kivunjike😂😂😂
 
Nilisikia kwamba Ronaldo akipiga shuti lazima ichane nyavu na pia akipiga shuti likakosa goli lazima shabiki 1 wa nyuma ya goli pinzani atakae patwa na mpira lazima avunjwe vidole au mkono kabisa
 
Drogba anakunywa lita 365 za Maziwa na Kuku 21 kwa siku 1 tuu
Mimi niliambiwa jamaa alivyokuja bongo na ivory coast kucheza dhidi ya taifa starz lunch yake alikua anakula kuku watatu. Sijui ni kweli au kamba
 
Kwamba straika wa Simba Fredy eti ni Fredy fungafunga!
 
Back
Top Bottom