Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ki ukweli inatia mashaka sana kiusalama. Kama mtu anaweza kutolewa ndani ya bus lililojaa abiria mchana kweupe na kesho yake anapatikana kauwawa tena kikatili sana.mgeni gani akisikia hivyo atakuwa na amani.
Huyo mwandishi wa the guardian naye atatekwa hivi karibuni 😒🥺,wasiojulikana watamfuata London. TCRA nao watatoa amri gazeti liombe radhi,kisha litapigwa ban ya siku 30 kupost maudhui mtandaoni . Hawa mabeberu waache kuichafua nchi yetu😒.
Na nchi inayo ongozwa na wanaoruhusu utekaji itoe fidia kwa wanaotekwa??!Gazeti hilo linaweza kudaiwa fidia kwa kuchafua haiba ya viongozi na nchi
Tusilalamike kwa mikuki ya kujichoma.Haya mambo yanawaharibia sana mkuu
Tumetumia mabilioni kuandaa Royal Tour then mambo kama haya yanatokea na kuchafua nchi.
Umuhimu wa Royal Tour uko wapi?
Mbongo hapo huenda alishaokotwa katobolewa macho na kaoza ama haonekani popote pengine ana kesi ya uhujumu uchumi.Nimewaza pia ndo maana wabongo hatuna international journalists wanaofanya kazi kwenye vyombo vikubwa duniani.
Imagine hiyo article angeandika mwandishi wa kibongo.
Wakuu,
Inaonekana kama Sativa is here to stay.
Siku ya leo, Gazeti la The Guardian kutoka Uingeereza limetoa bandiko linalohusu masuala ya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini
Edgar Mwakalebela maarufu alitajwa kama muhanga wa matukio ya utekaji yanayoendelea nchini ambapo pia alipata nafasi ya kuzungumza jinsi watu aliowatambua kama Polisi walivyomteka.
View attachment 3173374
Katika bandiko hilo la The Guardian, waathirika wengine wa utekaji pia walitajwa kama Mzee Ali Kibao, Abdul Nondo na baadhi ya makada wa CHADEMA waliouwawa kipindi cha Uchaguzi wa Serikali za mitaa.
View attachment 3173377
View attachment 3173376
===============
Kama tulitumia mabilioni kuandaa ili filamu ya Royal KUSAFISHA sura ya nchi yetu na sasa hivi vyombo vya kimataifa vinaturipoti kuwa Tanzania sio sehemu salama ya kuishi, ile Royal Tour ilikuwa na umuhimu gani?📌🔨
Wamelewa visungura wamelala subiri kukuche matusi utakayooga maana huwa wanaamka nazo.Sijaona matusi ya UVCCM au wamelala?
Gazeti hilo linaweza kudaiwa fidia kwa kuchafua haiba ya viongozi na nchi
Edga mwakabelaSATIVA ndo nani?
Kwani limeandika uwongo? Sativa mwenyewe amethibitisha ni sahihi alitekwa na polisiGazeti hilo linaweza kudaiwa fidia kwa kuchafua haiba ya viongozi na nchi
Mwenyekiti wa ccm wilaya ya namtumboSATIVA ndo nani?
Tufungue kesi kesho mahakamaniGazeti hilo linaweza kudaiwa fidia kwa kuchafua haiba ya viongozi na nchi
Ni yule kijana Mwakalebela ambaye CCM ikiwatuma polisi na TISS iliyotaka kumuua kwa kuikosoa serikali!SATIVA ndo nani?