007...
tulifika horohoro sa6 usiku na kukutana na mtu atakaye nisaidia kufuka mpaka. Nilimlipa dereva pesa yake kiasi cha sh10,000 kama tulivyokubaliana na yeye akaondoka na kuniacha na mwenyeji wangu wa hapo horohoro. Alikua ni kijana wa miaka kati ya 30-35 alionyesha ni mtu mtulivu asiyependa maneno mengi.
Baada ya nusu saa tulikua tumekubaliana kwamba nitamlipa kiasi cha sh20,000 bada ya kuvuka mpaka na kuingia kenya. Safari yetu ilianza sa8 usiku baada ya kumaliza kupata chakula hapo nyumbani kwa kijana atakaye nivusha mpaka. Tulipita njia ya mapori kwa pori ajabu nilishangaa kukutana na watu wanavuka kwa njia ya panya hawakuwa wachache ni mpishano wa watu eidha wanamizigo ama wako tupu lakini njia ile ilikua imechangamka kama vile ni mchana na watu wale wanafanya shughuli halali.
Tulitembea kwa mwendo wa lisaa na nusu mpaka kutokea kwenye kamji kadogo. Mwenyeji wangu aliniambia hapo ndo utakuwa mwisho wa yeye kua pamoja nami
............,