Story ya kurejea kwa Sultan wa Zanzibar ni Fake News! JF Tumelishwa Tango Pori!. Asante Kaka Chale kuniwezesha kuupata ukweli

Hapa JF huwa tunapenda kujadiliana kwa facts na ushahidi, ukiisoma story mzima ya Hayati John Okello inajielezea wazi alipotoka Uganda Kenya na kuingia Visiwani ilikuwa ni safari ya kutafuta ajira kubangaiza alipofika Zanzibar alifedheheshwa sana na maisha ya Waafrika yalikuwa maisha duni sana huku wakinyonywa na Wazanzibari wa makabila ya Waarabu.
Okello alikuwa ni Che Guavara wa Kiafrika.
 

Kwa hiyo mkuu story aliyotoa Okello ndio inakamilisha fact ya yaliyotokea? Wewe ni Mfuasi wa Lissu, katafute darasa za Lissu juu ya suala zima la mapinduzi ya Zanzibar utaelewa mengi sana.
 
Kwa hiyo mkuu story aliyotoa Okello ndio inakamilisha fact ya yaliyotokea? Wewe ni Mfuasi wa Lissu, katafute darasa za Lissu juu ya suala zima la mapinduzi ya Zanzibar utaelewa mengi sana.
Usicomplicate mambo na Conspiracy theories, msome kwanza John Okello, Nyerere angetaka kuvivamia Visiwa kwanini amtumie Kijana wa Kiganda wakati alikuwa Askari shupavu kabisa kwenye Jeshi.

Hata kama Nyerere alihusika kumuondoa Sultani wa Kiarabu alifanya jambo la maana sana huwezi kuwa Omani Kingdom katikati ya Afrika Huru.

Mimi kuwa mfuasi wa Lissu haimaanishi kuwa ni Blind Follower wa Lissu.
 

aliekwambia nani kuwa Zanzibar ilikuwa Oman Kingdom? kichwa chako kimejaa chuki za kibaguzi ulizolishwa na propaganda uchwara za CCM ni ngumu sana kuelewa.

Unajifanya unaichukia CCM lakini propaganda zake unaendelea kuzikumbatia.
 
Iwe kweli au uongo huyo chief wenu sijui sultan, hatakiwi kugusa ardhi takatifu ya East Afrika, maana ni pandikizi la washenzi walioharibu maisha ya watu weusi.

Hii itawauma wale waafrika weusi wanaojiona washakua vijukuu vya mtume na waarabu, hao Wahuni waliuza na kuua watu weusi walitumia mgongo wa dini kuwapandikiza uongo ili wajisafishe mauchafu Yao, lkn historia inabaki pale pale utawala wa wageni Afrika haileti maana, mbona sisi hatutawali ktk ardhi zao huko uarabuni?

Mwarabu/mzungu kuzaliwa Afrika haimfanyi yeye kuwa mtu wa ASILI hii na mtawala wa ardhi hii, hapa wazanzibar walipigwa mchana kweupe, maajabu hii mijitu ngozi nyeusi ambayo babu zao walitekwa Tanganyika na wengine kubakwa, kuuliwa na baadhi kuuzwa utumwani, imeibuka masalia ya hii mitoto ya kizanzibar iliyorogwa na dini, haitaki ukweli, imebaki kuutetea utawala wa kishenzi wa mwarabu na masultan, kitu ambacho sidhani mababu waliofanyiwa ukatili wa biashara haramu ya utumwa wangekubali hiki wafanyacho wajukuu zao wapumbavu.
 
Historia ya mapinduzi ya Zanzibar ina mengi yaliyofichwa, Lissu kaongea hoja zenye mashiko.
Lissu angetaja hata Kitabu sio hivi vya Mohammed Said ambaye anavutia upande mmoja kama mwamba ngozi.

Kuna ubaya gani wa kutaja source zako, unazitaja tu, hebu angalia njama za kupigwa risasi na kuuwawa Raisi Kennedy wa US kuna vitabu vingi sana vinavyoliongelea lile tukio,na sio vyote vinavyoongea ukweli.

Au hata unaweza kusema source yangu ni kitabu cha Yericko Nyerere halafu sisi tutasema Yericko?! Huyu huyu mbabaishaji?! Hatutoamini Story zako.tunataka Source zenye kuaminika.
 
 
Lissu angetaja hata Kitabu sio hivi vya Mohammed Said ambaye anavutia upande mmoja kama mwamba ngozi.
Tafuta kitabu cha ' Kwa heri ukoloni kwaheri uhuru Zanzibar na mapinduzi ya Afrabia kilichoandikwa na Harith Ghassany ;

Au tafuta kitabu cha "ukweli ni huu" cha Amani Thani Kuna mengiw yameandikwa humo.

Hata humu JF zipo nyuzi nyingi tu kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.
 
Nimeiuliza Chatgpt kuhusu waliokuwa nyuma ya Mapinduzi ya kumuondoa Sultani wa Zanzibar.

Mapinduzi ya Zanzibar, yaliyofanyika Januari 12, 1964, kimsingi yaliongozwa na Afro-Shirazi Party (ASP) na Zanzibar Nationalist Party (ZNP), pamoja na kuungwa mkono na Tanganyika African National Union (TANU). Mapinduzi hayo yalichochewa kwa kiasi kikubwa na mivutano ya kikabila na kisiasa kati ya Waarabu na Waafrika huko Zanzibar, huku Waafrika walio wengi wakihisi kutengwa na serikali iliyotawaliwa na Waarabu. Wahusika wakuu nyuma ya mapinduzi ni pamoja na: 1. John Okello: Kiongozi wa Afro-Shirazi Party (ASP) na mmoja wa makamanda wakuu wa mapinduzi. Okello alikuwa mhusika mkuu katika kuandaa maasi na kuhamasisha uungwaji mkono kutoka kwa Waafrika walio wengi, hasa katika kisiwa cha Zanzibar. 2. Abeid Karume: Kiongozi wa Afro-Shirazi Party, ambaye baadaye alikua Rais wa kwanza wa Zanzibar baada ya mapinduzi. Ingawa hakuhusika moja kwa moja katika mapambano ya silaha, Karume alikuwa na nafasi kubwa ya kisiasa katika kipindi cha baada ya mapinduzi. 3. Serikali ya Tanzania: Serikali mpya iliyoundwa ya Tanganyika Bara, inayoongozwa na Julius Nyerere na chama chake, TANU, ilichukua jukumu muhimu katika kusaidia mapinduzi. Serikali ya Nyerere ilitoa msaada wa kijeshi na kusaidia katika uimarishaji wa madaraka baada ya mapinduzi. Mapinduzi hayo yalisababisha kupinduliwa kwa Sultani wa Zanzibar na serikali iliyotawaliwa na Waarabu, na kusababisha kuanzishwa kwa jamhuri yenye mwelekeo wa kijamaa. Ilifuatiwa na muungano wa Zanzibar na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Tanzania mnamo Aprili 1964.
 
...Mjini Unguja Jijini Zanzibar...
 
Sultan anakaribishwa akikaa hapo ataanza kuwasaidia mwishoe wanamrudisha kwenye utawala kisha anafuta sheria zote muhimu kama ukomo wa urais, Zanzibar inarudi tena kutawaliwa na Sultani wa Oman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…