pinno
JF-Expert Member
- Jan 17, 2013
- 1,213
- 1,229
Wandugu,
Mimi sio mpenzi sana wa soka, ila huwa nafuatilia timu yangu ya Taifa, Timu yangu ya Mkoa naotoka, na timu mbili tatu ambazo zinanifutia ligi za mbele, ila sio yule shabiki ambae ni shabiki kindaki ndaki,
Sasa nafahamu kuhusu yule kipa, kipenzi cha rais wa Jiji la Dar es salaam, ambae amesifiwa kutwa kucha na mkuu huyo, hadi ilifika mahali, mkuu akamtunuku kitita cha hela, Kipa Aishi Manula.
Japo kulikuwa na makelele mengi ya wadau kuwa kipa huyo sio lolote, na kuwa anabahatisha, lakini inaonekana Kocha aliekuwepo Bwana Amunike, pamoja na viongozi wa TFF walikuwa wanamuelewa,
Kaja kocha mpya, akataka kumchezesha Bwana Juma Kaseja kwenye mechi dhidi ya Kenya, kwa kuwa kutokana na kocha huyo, alikuwa anaamini kuwa Bwana Juma kaseja, bado ni kipa bora kabisa, na hakuna mfano wake TZ, Na alikuwa anajua hili kwa sababu yeye ndo kocha wake kwenye timu anayochezea sasa, TFF na wadau wakahamaki, na wakahisi kuna wadau watamind, akiwemo raisi wa Dar, kuwa kipa wake anaemkubali hajapangwa,
Ila kwa kuwa walikubaliana kutoingilia maamuzi ya makocha, wakakubali,Juma Kaseja ajaribishwe ile mechi, ila sasa wakiamini kuwa atavurunda tu, na mechi zijazo Manula ataendela, basi ikabidi waje na ka press release ili kumanage hamaki ya wadau wa soka, endapo kutatokea watu kupaniki kwa kutoona Aishi Manula anacheza,
Wakasema Manula hachezi kwa kuwa ni majeruwi, Siku ikapita, Kaseja akaingia uwanjani, akaonesha uwezo mkubwa ajabu, mechi ya marudiano, akaonesha uwezo mkubwa ajabu, kadaka penalty tatu, tukawatoa Wakenya, Watu wakakumbuka mechi yetu dhidi ya Kenya kule Misri, ambapo Bwana Manula alishindwa kupangua mikwaju ile ya Wakenya ila leo hii Bwana Kaseja kaipangua yote, Mtaani wakasema "Laiti kama Kaseja angekuwepo kule Misri, pengine story ingebadilika" na ndipo hata wale waliokua wanabeza uchaguzi wa wachezaji wa kocha aliepita Bwana Amunike, wakasikika sauti zao wakisema "Ndio maana sisi tulisema huyu kocha alikuwa hajui kuchagua wachezaji wa kuwapanga"
Now, Kaseja is back, Je Manula bado ana lake pale? Je Bwana DAB Bado ataendelea kusapoti timu kwa mapenzi yote, maana naona tangu alipozila kwenye maandalizi dhidi ya Kenya baada ya kujua kipa wake kipenzi hayupo, naona ameendelea kuji weka mbali na timu had leo hii. Utadhani si timu ile aliyekuwa anaifungia safari hadi Misri.
The future is exciting kwa Juma Kaseja ,Taifa Stars na Tanzania ya Michezo.