Bongotunacheza
JF-Expert Member
- Dec 7, 2018
- 1,821
- 3,980
Jana niliweka taarifa ya kupotea kwa mtoto Richard Riziki Kiko (15) mwanafunzi wa kidato cha pili, shule ya sekondari Mbwawa Lutheran iliyopo Kibaha. Richard alipotea juzi jumapili, akiwa anarudi nyumbani Magomeni Kagera akitoka kumsalimia bibi yake Mbezi Kibanda cha Mkaa.
Jioni wakati anarudi nyumbani alipelekwa na bodaboda hadi kituo cha Mbezi Kibanda cha Mkaa ili apande daladala za kurudi Magomeni. Dereva boda alimuacha kituoni hapo na kuondoka. Hata hivyo hakufika nyumbani na hakujulikana alipo. Baada ya taarifa hiyo kusambaa, hatimaye Richard amepatikana akiwa amefariki na mwili wake umehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala.
Akiwa kituoni badala ya kupanda daladala, alipanda bodaboda za kuchangia (mshkaki) kutoka Mbezi kurudi Magomeni. Walipofika maeneo ya Kimara Suka bodaboda iligonga "bump" na kutokana na speed kali pamoja na kupakia abiria watatu, Richard alirushwa na kuangukia kwenye lami ambapo alijeruhiwa.
Kwa bahati mbaya akiwa anatapatapa chini, kabla hajaokolewa, gari dogo ilipita muda huohuo na kummalizia. Watu waliokua karibu walipokimbilia ili kutoa msaada, walikuta Richard ameshafariki dunia. Polisi walifika na kuupeleka mwili Mwananyamala. Dereva wa gari dogo alisimama na kutoa ushirikiano lakini bodaboda alikimbia.
Msiba upo nyumbani kwao Magomeni Kagera. Tunatoa pole kwa familia, uongozi wa shule ya sekondari Mbwawa na wananfunzi wenzie. Raha ya milele umpe ee BWANA, na Mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani 🙏🏽
Credit : MALISA GJ FACEBOOK PAGE.