Story ya mtoto Richard Kiko ( 15) inasikitisha mno

Story ya mtoto Richard Kiko ( 15) inasikitisha mno

Aisee..!Nimekoswa Raha na Siku yangu imeharibika kabisa!!!
Rest Easy Mtoto.Pole kwa Familia na kwa namna ya pekee mno kwa huyo BIBI yake,anapitia kipindi kigumu kuliko.....
Unaweza kusema kwanini asingepanda bus, ila ndiyo ishatokea

Ova
 
inasikitisha sana,, pale kimara suka ni kama kuna mapepo wanywa damu sidhani kama miezi miwili inaweza kupita bila kutokea ajali

apumzike kwa amani😔
Hasa pale kwenye mataa ni hatari
 
Polen sana wafiwa...bodaboda ni usafiri hatari sana
 

Na Shida Nyingine Kubwa Ni Kutozingatia Uvaaji Wa Protective Gears Si Dereva Wala Abiria...​
 
kuna ajali nyingine huwa zinatokea bila kueleweka nishawahi kushuhudia moja ndo maana nimesemea coz hiyo siku hakukua na uzembe wala nini usinibishie
Unabishiwa bana usibishiwe wewe kobe?

Suka hamna mapepo wala nini shida ni uzembe na usenge wa madereva na watumiaji barabara wa miguu pale gari na boda zinapita kwa speed zikiwahi taa unategemea nini nyoko wee
 
Unabishiwa bana usibishiwe wewe kobe?

Suka hamna mapepo wala nini shida ni uzembe na usenge wa madereva na watumiaji barabara wa miguu pale gari na boda zinapita kwa speed zikiwahi taa unategemea nini nyoko wee
nyoko mwenyew
 
Jana niliweka taarifa ya kupotea kwa mtoto Richard Riziki Kiko (15) mwanafunzi wa kidato cha pili, shule ya sekondari Mbwawa Lutheran iliyopo Kibaha. Richard alipotea juzi jumapili, akiwa anarudi nyumbani Magomeni Kagera akitoka kumsalimia bibi yake Mbezi Kibanda cha Mkaa.

Jioni wakati anarudi nyumbani alipelekwa na bodaboda hadi kituo cha Mbezi Kibanda cha Mkaa ili apande daladala za kurudi Magomeni. Dereva boda alimuacha kituoni hapo na kuondoka. Hata hivyo hakufika nyumbani na hakujulikana alipo. Baada ya taarifa hiyo kusambaa, hatimaye Richard amepatikana akiwa amefariki na mwili wake umehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala.

Akiwa kituoni badala ya kupanda daladala, alipanda bodaboda za kuchangia (mshkaki) kutoka Mbezi kurudi Magomeni. Walipofika maeneo ya Kimara Suka bodaboda iligonga "bump" na kutokana na speed kali pamoja na kupakia abiria watatu, Richard alirushwa na kuangukia kwenye lami ambapo alijeruhiwa.

Kwa bahati mbaya akiwa anatapatapa chini, kabla hajaokolewa, gari dogo ilipita muda huohuo na kummalizia. Watu waliokua karibu walipokimbilia ili kutoa msaada, walikuta Richard ameshafariki dunia. Polisi walifika na kuupeleka mwili Mwananyamala. Dereva wa gari dogo alisimama na kutoa ushirikiano lakini bodaboda alikimbia.

Msiba upo nyumbani kwao Magomeni Kagera. Tunatoa pole kwa familia, uongozi wa shule ya sekondari Mbwawa na wananfunzi wenzie. Raha ya milele umpe ee BWANA, na Mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani 🙏🏽

Credit : MALISA GJ FACEBOOK PAGE. View attachment 3619166
Poleni sana.Nadhani hapo tutmwelewa Mh.Mnyonge Songoro
 
kuna ajali nyingine huwa zinatokea bila kueleweka nishawahi kushuhudia moja ndo maana nimesemea coz hiyo siku hakukua na uzembe wala nini usinibishie
Eleza ilitokeaje bila uzembe mimi nikuonyeshe uzembe ulipo.
 
Back
Top Bottom