Bongotunacheza
JF-Expert Member
- Dec 7, 2018
- 1,821
- 3,980
Hao boda washashindikana
Mapepo au uzembe? Nikisema haya ni madhara ya kutawaliwa na viongozi waliojiweka madarakani ili kuponda raha kuna watu hawawezi kuona connection na hiki kifo. Ukweli ni kwamba matokeo ya uongozi mbovu yataikumba kila familia na sisi tutabaki kusingizia mapepo.inasikitisha sana,, pale kimara suka ni kama kuna mapepo wanywa damu sidhani kama miezi miwili inaweza kupita bila kutokea ajali
apumzike kwa amani😔
Mkuu hawajashindikana ila hakuna uongozi nchii hii! Kna watawala waliojiweka kwa nguvu ili waponde maraha wakati wananchi wanakufa. Tusipokubali kuungana na kuwatimua tutaendelea kuishi kama digidigi muda wote.Hao boda washashindikana
Aise
Ova
kuna ajali nyingine huwa zinatokea bila kueleweka nishawahi kushuhudia moja ndo maana nimesemea coz hiyo siku hakukua na uzembe wala nini usinibishieMapepo au uzembe? Nikisema haya ni madhara ya kutawaliwa na viongozi waliojiweka madarakani ili kuponda raha kuna watu hawawezi kuona connection na hiki kifo. Ukweli ni kwamba matokeo ya uongozi mbovu yataikumba kila familia na sisi tutabaki kusingizia mapepo.
Jana niliweka taarifa ya kupotea kwa mtoto Richard Riziki Kiko (15) mwanafunzi wa kidato cha pili, shule ya sekondari Mbwawa Lutheran iliyopo Kibaha. Richard alipotea juzi jumapili, akiwa anarudi nyumbani Magomeni Kagera akitoka kumsalimia bibi yake Mbezi Kibanda cha Mkaa.
Jioni wakati anarudi nyumbani alipelekwa na bodaboda hadi kituo cha Mbezi Kibanda cha Mkaa ili apande daladala za kurudi Magomeni. Dereva boda alimuacha kituoni hapo na kuondoka. Hata hivyo hakufika nyumbani na hakujulikana alipo. Baada ya taarifa hiyo kusambaa, hatimaye Richard amepatikana akiwa amefariki na mwili wake umehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala.
Akiwa kituoni badala ya kupanda daladala, alipanda bodaboda za kuchangia (mshkaki) kutoka Mbezi kurudi Magomeni. Walipofika maeneo ya Kimara Suka bodaboda iligonga "bump" na kutokana na speed kali pamoja na kupakia abiria watatu, Richard alirushwa na kuangukia kwenye lami ambapo alijeruhiwa.
Kwa bahati mbaya akiwa anatapatapa chini, kabla hajaokolewa, gari dogo ilipita muda huohuo na kummalizia. Watu waliokua karibu walipokimbilia ili kutoa msaada, walikuta Richard ameshafariki dunia. Polisi walifika na kuupeleka mwili Mwananyamala. Dereva wa gari dogo alisimama na kutoa ushirikiano lakini bodaboda alikimbia.
Msiba upo nyumbani kwao Magomeni Kagera. Tunatoa pole kwa familia, uongozi wa shule ya sekondari Mbwawa na wananfunzi wenzie. Raha ya milele umpe ee BWANA, na Mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani 🙏🏽
Credit : MALISA GJ FACEBOOK PAGE. View attachment 3619166
Kuna yangu mmoja hukoRIP! Boda zinamaliza watu,hasa mida ya kuanzia jioni kagiza giza hivi mpk muda wa saa mbili usiku ni hatari sana
Hawana time naoUsalama barabarani kazi yao nini!?Yaani pikipiki inaingia highway ikiwa imebeba mishikaki tena kuna mwanafunzi!
Kiasi kikubwa bike ni mauti hasa kwa matumizi ya highway huko kupasuliwa kichwa ni ishu ndogo tuKuna yangu mmoja huko
Alimnunulia chombo boda
Binamu yake awe anapiga kazi imuingizie kipato ndg yake
Kuna siku tumekaa tunapiga vyombo aliponambia nkamwambia kiutani tu
Kikubwa awe makini hilo jeneza linalotembea
Jamaa hakumaliza hata miezi 7 alipata kichwa alikuwa anakipeleka tandika
Pale kwenye mataa ya kiwanda serengeti alichotwa
Dah alipasuliwa hapo hapo na truck
Ova