Story za maajabu na kustaajabisha Duniani

Story za maajabu na kustaajabisha Duniani

KUTANA NA JEAN BEDEL BOKASSA, RAIS ALIYEPENDA STAREHE KULIKO WOTE AFRIKA KATIKA UTAWALA WAKE.

Miongoni mwa watawala waliokuwa na visa na vituko vingi katika bara hili la Afrika ni mfalme wa kujipachika wa Afrika ya Kati, Jean-Bedel Bokassa.

Jean Bedel Bokassa akiwa anaongoza nchi masikini kabisa duniani, alifanya sherehe ya kujisimika kama mfalme mwaka 1977 kwa kutumia kiasi cha sawa na shilingi bilioni 32 za Kitanzania za wakati huu. Lile taji lake la Ufalme peke yake liligharimu kiasi cha shilingi bilioni tatu!.

Jean Bedel Bokassa alikuwa dikteta wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Alikuwa na wake kumi na saba (17) na watoto hamsini (50).

Alifanywa yatima wafaransa walipomuua baba yake akiwa na miaka sita (6) baada ya baba yake kufa mama yake naye alijiua.

Alipata kupigana vita ya pili ya dunia chini ya Wafaransa. Baadaye alikuja kumpindua rais aliyekuwa ndugu yake mwaka 1965. Alijipa cheo cha field marshall na kutengeneza uniform maalumu sababu ya wingi wa medals alizojipa. Akienda kutembelea nchi alikuwa anagawa almasi.

Alikuwa ana majumba zaidi ya sita Ufaransa. Pia alikuwa na majumba mengine nchi mwake, katika majumba yake mengine yaliyokuwa nchini mwake, Jumba lake mojawapo lilikuwa na bwawa la mamba na simba wa kufugwa, alitumia mamba hao na simba kuulia wapinzani wake.

Wake zake walikuwa Mchina, Mjerumani, Msweden, Mtunisia na Mromania. Aliwaweka nyumba tofauti na alikuwa akiwatembelea kila siku na kusababisha foleni kubwa barabarani kutoka na wingi wa safari hizo huku akiambatana na misafara.

Alipinduliwa na wafaransa baada ya kuua wanafunzi waliokua wanaandamana. Alifungia wanafunzi 30 kwenye jela ya mtu mmoja.

Walipompindua kwenye friji yake walikuta nyama za watu.

Mwishoni mwa maisha yake alitumia kusoma bible na huku akiwa anajiita mtume wa yesu. Hatimae alifariki mnamo mwaka 1996 kutokana na ugonjwa wa moyo.

View attachment 802286
hahahaha..mamaee....Africa kumbe imerogwa muda mrefu mnoooo"".
 
UJUE MGOGORO WA ARDHI KATI YA ISRAEL NA PALESTINA NA SULUHISHO LAKE

Israel ni taifa pekee la kiyahudi Duniani. Taifa hili linapatikana Mashariki ya bahari ya Mediterrania, ni taifa dogo kwa eneo, likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 20,770. ( Imezidiwa ukubwa wa eneo na Wilaya ya Sikonge nchini Tanzania kwa tofauti ya kilomita za Mraba 7103 ). Israel inapakana na nchi za Syria na Lebanon kwa upande wa kaskazini, Jordan na eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi (West bank) kwa upande wa Mashariki na kusini inapakana na Misri na eneo la Palestina la Ukanda wa Gaza ( Gaza strip ).Taifa hili lina idadi ya watu Milion 8,680,000 kwa takwimu za mwaka 2017. Idadi ya Wayahudi ni Milioni 6,484,000 sawa na 74.7% (Idadi hii inajumuisha Walowezi wa Kiyahudi wanaoishi ukingo wa Magharibi (West bank) na eneo la Milima ya Golan). Waisrael Waarabu ni Milioni 1,808,000 sawa na 20.8% ya raia wote wa Israel. Idadi ya Wakristo ambao sio Waarabu pamoja na watu wa jamii ya bahai ni 388,000 sawa na 4.5% ya raia wote wa Israel. Lugha rasmi za Taifa la Israel ni Kiebrania (Hebrew) na Kiarabu (Arabic)

Wapalestina ni jamii ya Kiarabu inayopatikana kwa wingi katika ardhi yao inayokaliwa kimabavu na Israel, kwenye ukingo wa Magharibi wa mto Jordan (West bank) na eneo la Ukanda wa Gaza lililowekewa mzingiro na Taifa la Israel. (Besieged Gaza strip). Idadi ya watu Wanaoishi katika ardhi ya Palestina ni milioni 4,543,126 kwa takwimu za mwaka 2017 ambapo Wapalestina ni 3,950,926 na Walowezi wa kiyahudi wanaunda idadi ya watu 5,92,200. Eneo la Ukingo wa Magharibi (West bank) lina ukubwa wa kilomita za Mraba 5,860 na Idadi ya Watu milioni 2,747,943 kwa takwimu za mwaka 2017. Eneo lililozingirwa la Gaza (Besieged Gaza strip) lina ukubwa wa kilomita za Mraba 360 na idadi ya watu 1,795,183 kwa takwimu za mwaka 2017. (Ukubwa wa ukanda wa Gaza umetofautiana kidogo na ukubwa wa Wilaya ya Ilala inayopatikana mkoa wa Dar es salaam nchini Tanzania kwa kilomita tano za mraba). Lugha rasmi za Wapalestina ni Kiarabu (Arabic) na Kiebrania(Hebrew).

UZAYUNI (ZIONISM) NA KUTAWANYIKA KWA WAYAHUDI
Uzayuni (Zionism) ni Itikadi ya taifa la Israel. Mazayuni (Zionists) wanaamini kuwa Uyahudi (Judaism) ni utaifa na pia ni dini. Na kwamba Wayahudi wanastahili kuwa na nchi yao katika ardhi ya mababu zao kama ambavyo Wachina wanavyostahili kuishi China au Wahindi wanavyostahili kuishi India. Itikadi hii ndiyo iliyosababisha Wayahudi kuanza harakati za kurudi tena katika ardhi ya Palestina na kuunda taifa la Israel mnamo mwaka 1948. Na hiki ndicho chanzo cha mgogoro wa sasa kati ya Wapalestina na Waisrael.

Wayahudi wanapozungumzia Historia ya utaifa wao, huanzia kwenye ufalme wa Daudi (David) ambaye ndiye muasisi wa Ufalme wa Israel uliojulikana kama United Monarch mnamo mwaka 1004- 960BC. Baada ya kifo cha Daudi, mwanaye Suleiman (Solomon) alishika hatamu ya uongozi kuanzia mwaka 961-922BC. Baada ya kifo cha mfalme Suleiman mwaka 922BC Makabila kumi ya upande wa Kaskazini yalikataa kuwa chini ya Utawala wa mfalme Rehoboam ambaye alikuwa ni mtoto wa Mfalme Suleiman, hivyo makabila haya yalifanya uasi na kuanzisha ufalme wao walioupa jina la Ufalme wa Israel-Samaria, mji mkuu wa Ufalme huu uliitwa Samaria, baadae walihamishia makao makuu kwenda mji wa Wacaanan wa Sichem ambao kwa sasa unajulikana kama Nablus. Ufalme huu ulisambaratika baada ya kuangukia mikononi mwa dola ya Assyria ( Assyrian Empire) mnamo mwaka 720BC.

Hali hii ilipelekea kuwepo kwa falme mbili za Kiebrania za upande wa Kaskazini na upande wa kusini ambayo hii ya upande wa kusini ilibaki kuwa chini ya Mfalme Rehoboam ilijulikana kama nchi ya Yuda (Judah), makao yake Makuu yalibaki katika mji wa Jerusalem na baadae yalihamishiwa katika mji wa Hebron. Ufalme huu ulisambaratika baada ya kushindwa vita na kuangukia mikononi mwa mfalme Nebuchadnezzar wa Babeli mnamo mwaka 587BC.

Mwaka 63BC nchi ya Yuda iliwekwa chini ya uangalizi wa dola ya Kirumi na mwaka wa 6CE iliunganishwa na kuwa jimbo la Warumi. Mnamo kwaka 135CE Wayahudi waliasi na kupelekea vita baina yao na Warumi ambapo walishindwa vibaya, walipoteza uhuru wao na mji wa Jerusalem uligeuzwa kuwa mji wa kipagani.Wayahudi walipigwa marufuku kuishi Jerusalem na Warumi waliibadili jina nchi ya Yuda na kuiita Syria Palestina.

Kusambaratika kwa falme hizi mbili za kiyahudi na kutawaliwa na madola makubwa kuanza Assyria empire, Babylonian empire, Persian Empire (Iran), Greek empire, Roman Empire, Rashidun Caliphate, Ummayad Caliphate, Ayyubid Dynasty, Mamluk Sultanate, Ottoman Empire na British Empire (United Kingdom) kulipelekea Wayahudi kutawanyika katika maeneo mbali mbali Duniani. Kutawanyika huku kuliwagawa Wayahudi kwa majina kutegemea na maeneo waliyotawanyikia. Makundi haya ya Wayahudi ni Ashkenazi (Ashkenazi Jews) kundi hili ni lile lililohamia katikati na Mashariki ya bara la Ulaya. Sephard (Sephardic Jews ) ni kundi lililohamia maeneo ya kusini ya bara la Ulaya na Kaskazini ya Afrika na Mizrahi (Mizrahi Jews) ambao walibaki mashariki ya kati, Asia ya Kusini na Asia ya kati.

JE WAYAHUDI WALIIKUTA ISRAEL IKIWA TUPU BILA WATU?
Ardhi ya Israel (Palestina) ilikuwa na wenyeji ambao ni makabila ya mwanzo kuja kuweka makazi yao katika nchi ya Palestina. Makabila haya yalihamia huko kutoka kusini na Kaskazini mwa Bara Arabu takriban mwaka 3000 BC. Makabila hayo ni Wayebusi (Jebusites), Waamori (Amorites), Wahiti (Hittites) Wakanaani (Canaanites) na Waperizi(Perizzites). Makabila haya yalikaa katika maeneo tofauti ya nchi hiyo: Wakanaani waliweka makazi yao katika eneo la Gaza na Wayebusi walibuni mji wa Yebus, ambao kwa sasa unajulikana kama mji wa Jerusalem. Wayebusi walipokonywa mji huo na Wayahudi baada ya kutoka Utumwani nchini Misri mwaka 1003BC chini ya utawala wa mfalme Daudi ambaye aliufanya kuwa makao makuu ya ufalme wake.

Ibrahim ambaye uzao wake ndio unaounda jamii ya wana wa Israel alihamia Palestina wakati huo ikiitwa nchi ya Wacaanan mwaka 1900BC akitokea Kusini mwa Iraq katika eneo lilijulikana kama Uru ya Wakaldayo (Ur of Chaldeans). Ibrahim aliishi kwa amani na jamii za eneo hilo ambapo alizaa watoto wawili Ismail na Issaack. Ismail na Mama yake walihama Canaan na kuweka makazi yao katika mji wa Makka wakati Issack alibaki Caanan na baba yake Mzee Ibrahim na makazi yao yalikuwa katika mji wa Hebron( Halil). Issack alimzaa Jacob (Yakubu) ambaye naye alifanikiwa kuzaa Watoto kumi na mbili.Kutokana na nchi ya Canaan kukumbwa na baa kali la njaa, Jacob ambaye baadae alibadili jina na kuitwa Israel na watoto zake walihamia Misri.

Wakiwa Misri walizaliana kwa wingi na kuishi kama watumwa kwa muda wa miaka mia nne (400) hadi Mwaka 1190BC waliporudi katika nchi ya Caanan wakiongozwa na Viongozi wao walioitwa Mussa(Moses) na Joshua Nun (Yusha bin Nuun). Mussa (Mosses) alifariki wakati wakiwa safarini hivyo Joshua ndiye aliyefanikiwa kuwafikisha katika nchi ya Caanan ambapo walifanikiwa kuteka maeneo kadhaa baada ya kuingia kwenye mapigano na wenyeji wao Wacaanan na makabila mengine. Hapo ndipo Joshua alifanikiwa kuanzisha na kuongoza dola ya Wana wa Israel.

Dola hii haikuweza kudumu muda mrefu kwani Ilisambaratika baada ya kufa Joshua (Yusha bin Nuun) hivyo Wana wa Israel waliangukia kwenye mateso ya Wafilisti ambao ni jamii ya Wacaanan waliokuwa wakielekea upande wa Kaskazini kutokea kwenye miji yao ya pwani ya kusini ambayo ni Gaza, Ekron, Gath, Ashdod, na Ashkelon. Wana wa Israel wakiongozwa na Sauli (ambaye kwa kiarabu anatajwa kwa jina la Twaaluti) walifanikiwa kuwashinda Wafilisti na kuanzisha tena Dola ya Wana wa Israel mnamo mwaka 1025BC.

Sauli alifariki mwaka 1004BC na hivyo Daudi alishika uongozi na kuwa mfalme wa Dola ya Israel iliyojulikana kama United Monarch. Ni katika utawala wa mfalme Daudi (King David) ndipo dola ya Israel ilipoimarika na kujitanua katika maeneo mengi ikiwa ni pamoja na kuuteka mji wa Jerusalem kutoka mikononi mwa Wayebusi (Jebusites) mnamo mwaka 1003BC. Mfalme Daudi alifariki mwaka 960 na mtoto wake Suleiman ( King Solomon) alishika hatamu ya Uongozi hadi Mwaka 922BC alipofariki. Kufariki kwa Mfalme Suleiman kulipelekea kugawanyika kwa dola Israel (United Monarch) baada ya makabila kumi ya upande wa Kaskazini kukataa kuutambua utawala wa mfalme Rehoboamu ambaye alikuwa mtoto wa Mfalme Suleiman. Hali hii ilipelekea dola hii kuanguka na kutawaliwa na madola mengine makubwa.

Baada ya kipindi kirefu cha wastani wa miaka 1360 ya kutawaliwa na Madola mbali mbali makubwa kama Assyrian empire, Babylonian empire, Persian Empire (Iran), Greek empire na Roman Empire kilichopelekea Wayahudi wengi kupelekwa utumwani na wengine kutawanyika sehemu mbalimbali huku wakiziacha jamii nyingine zikiendelea kubaki katika eneo hilo la Palestine (Israel) hatimaye Mji wa Jerusalem uliingia mikononi mwa dola ya Kiislam (Rashidun Caliphate) mwaka 638CE baada ya kuwashinda Warumi wakati dola hiyo ya Kiislamu ilipokuwa chini ya uongozi wa Caliph Omar Al Khatwab ambaye alifunga safari kwenda Jerusalem kuchukua funguo za mji kutoka kwa kasisi Sophronius wa dola ya Kirumi.

Makabidhiano hayo ya mji wa Jerusalem yalifanyika katika kanisa linajulikana kama the Holy Sepulchre (Church of the Holy Sepulchre ), katika makabidhiano hayo ya mji wa Jerusalem, kasisi Sophronius na Caliph Omar Khatwab walisaini mkataba uliojulikana kama OMAR TREAT, mkataba uliotoa hakikisho kwa Wakristo kuishi na kufanya ibada zao bila kubughudhiwa. Mkataba huo ulisomeka hivi:

"Haya ndiyo ya amani aliyowapa Umar kiongozi wa Waislamu watu wa Jerusalem. Amewapa amani kwa nafsi zao na makanisa yao na misalaba yao, na kuwa hayatakaliwa makanisa yao wala hayatavunjwa, wala hayatapunguzwa kitu katika majenzi yake wala katika nafasi yake, wala hawatalazimishwa kuacha dini yao wala kudhuriwa yeyote katika wao, na ni juu ya watu wa Jerusalem kutoa jizya (tribute) kama wanavyotoa watu wa Madain"

Ni mwaka huo huo ambapo miji mingi ya Palestina (Israel)iliingia katika Dola ya Kiislamu.

Ikumbukwe kuwa Caliph Omar ndiye alijenga msikiti mdogo kwa ajili ya kufanya ibada katika eneo ambalo Waislamu wanaamini ndipo ulipokuwa Msikiti wa Mbali (Al Aqsa) uliotajwa kwenye Kitabu kitukufu cha Quran, Sura ya Kumi Saba (Surat Bani Israil). Kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya kiislam, ni eneo hili ambalo Mtume Muhammad aliwaongoza manabii katika ibada kabla hajapaa kwenda mbinguni katika kisa maarufu kinachojulikana kama MIRAJI. Baadae msikiti huo uliongezwa ukubwa hadi kufikia muonekano wake wa hivi sasa. Na kwa mujibu wa imani ya kiyahudi, katika eneo hilo ndipo Mfalme Suleiman (King Solomon) alipojenga hekalu la kwanza. Pia wanaamini kuwa ni katika eneo hilo ndipo patakapojengwa hekalu la tatu na la mwisho. Eneo hilo ni sehemu takatifu kuliko zote katika imani ya kiyahudi. Nchi ya Palestine pamoja na nchi za Sham zote zilibakia katika utawala wa Kiislamu (Rashidun Caliphate) kwa muda wa miaka 461. Ni katika kipindi hicho ndipo jamii za eneo hilo la Palestina zilipojifunza lugha ya kiarabu, kubadili dini na kuingia katika Uislamu.

Dola ya Kiislamu ya Rashidun ilipokonywa eneo la Palestina (Israel) mwaka 1099CE na Wakristo kutoka Ulaya walipokuja kuzivamia ardhi hizo katika vita ya Msalaba iliyoshuhudia mauaji ya Waislamu elfu sabini (70,000) katika eneo la Msikiti wa Aqsa ( Temple Mount). Watu wa Msalaba (Crusaders) waliikalia ardhi ya Palestina wa muda wa miaka 88 kabla ya kutimuliwa na Majeshi ya Waislamu wa Ayyubid Dynasty chini ya Sultan wa Syria na Misri mwenye asili ya Kikurdi Swalaahud-Diyn Hasan al-Ayyuubiy ambaye aliweza kuirudisha Palestina mikononi mwa Dola ya Kiislamu mwaka 1187CE. Makao makuu ya dola hii ya kiislamu yalikuwa Cairo nchini Misri kati ya mwaka 1174CE hadi Mwaka 1250CE, baadae makao makuu ya dola hii yalihamishiwa Allepo nchini Syria mnamo mwaka 1250-1260CE.

Mwaka 1250CE dola ya Kiislamu ya Mamluk ilikamata hatamu ya kuiongoza Palestina na eneo lote la Sham (The Levent) kutoka mikononi mwa utawala wa Swalaahudin al Ayyuubin (Ayyubid Dynasty). Dola hii ya Mamluk ndiyo iliyopigana na kushinda vita dhidi ya wapiganaji shupavu wa jeshi la Mongol tarehe 6 Septemba 1260CE pale walipoivamia na kutaka kuikalia ardhi ya Sham. Ushindi huu wa dola ya Mamluk dhidi ya Wamongol ulikwenda sambamba na safisha safisha ya mabaki ya Wapiganai wa Msalaba (Crusaders) waliokuwa wamebakia katika maeneo ya ardhi ya Sham ( Syria, Jordan na Lebanon)

Baada ya dola ya Mamluk kuishiwa nguvu, hatimaye ardhi ya Palestina na eneo lote la ardhi ya Sham liliangukia Mikononi mwa dola ya Kiislam ya Ottoman (Ottoman empire) mwaka 1516CE. Dola ya Ottoman iliitawala Palestina kwa muda wa miaka 400 hadi ilipoikabidhi mikononi mwa Utawala wa Uingereza (United Kingdom empire) mwishoni mwa vita kuu ya kwanza ya Dunia mwaka 1918CE. (Rejea: kitabu cha The Palestinian Issue kilichoandikwa na Dr. Mohsen M. Saleh)

KUREJEA KWA WAYAHUDI KATIKA NCHI YA PALESTINA NA KUUNDWA KWA TAIFA LA ISRAEL.
Kutokana na manyanyaso, kuteswa na kubaguliwa kwa Wayahudi waliokimbilia barani Ulaya, hali hii ilipelekea Wayahudi kuanza kufuatilia kwa ukaribu zaidi asili yao. Ni wakati huo katika karne ya 19 ndipo Wasomi wa kiyahudi walipoona umuhimu wa kuwa na taifa lao katika ardhi ya asili ya mababu zao. Mwandishi wa Kiyahudi mzaliwa wa Austria Theodor Herzl alikuwa mtu wa kwanza kupaza sauti kuhusiana suala la utaifa wa kiyahudi (Jewish nationalism) katika harakati za kimataifa mnamo mwaka 1896.

Herz ambaye alishuhudia unyanyasaji mkubwa wa Wayahudi alishawishika kuamini kuwa Wayahudi hawangeweza kuishi kwa usalama wakiwa nje ya taifa lao. Aliandika Insha (essays) na kuandaa mikutano iliyochochea uhamiaji mkubwa wa Wayahudi kutoka Ulaya kwenda katika ardhi ya Palestine (Israel). Kabla ya harakati za Herz, ni Wayahudi elfu ishirini tu (20,000) waliokuwa wakiishi katika ardhi ya Palestina. Lakini hadi Adolf Hitler anafanikiwa kukamata madaraka idadi ya Wayahudi iliongezeka mara nane. Pia harakati za Wayahudi kurudi katika ardhi ya Palestina zilichochewa zaidi na azimio la Balfour (Balfour Declaration) la mwaka 1917, mwishoni mwa vita kuu ya pili ya Dunia ambapo utawala wa Uingereza kupitia Waziri wake wa mambo ya nje Arthur James Balfour ulitangaza kuanzisha Taifa la Wayahudi kwenye ardhi ya Palestina kupitia barua yake aliyoiandika kwenda kwa Lord Rothschild aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Kiyahudi ya Uingereza (British Jewish Community)

Waarabu waliona kumiminika kwa Wayahudi kama ni harakati za ukoloni kutoka Ulaya. Pande hizo mbili za Wayahudi na Waarabu ziliingia katika mapigano makali yaliyoshindwa kudhibitiwa na Utawala wa Uingereza katika Palestina. Mwaka 1947 Umoja wa Mataifa ulipiga kura kuigawa ardhi ya Palestina kuwa nchi mbili. Wayahudi ambao idadi yao ilikuwa 650,000 walikubaliana na uamuzi huo na kutangaza rasmi kuunda Taifa la Israel mnamo 14 May 1948 chini ya David Ben Gurion ambaye alikuwa Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kizayuni Duniani (World Zionist Organization)

Wapalestina (Waarabu) ambao idado yao ilikaribia 1,200,000 waliuchukulia uamuzi huo kama muendelezo wa mkakati wa muda mrefu wa Wayahudi kuwaondoa katika ardhi zao waliukataa mpango huo. Huo ndio ukawa mwanzo wa Mgogoro wa ardhi unaoendelea sasa baina ya Wapalestina na Waisrael. Wanamgambo wa Wapalestina wakisadiwa na mataifa ya kiarabu ya Misri, Jordan, Iraq na Syria walitangaza vita dhidi ya Israel mnamo tarehe 15 May, 1948.Vita vilimalizika tarehe 10 March 1949 kwa Israel kushinda na kunyakua ardhi zaidi kutoka mikononi mwa Wapalestina ambao wengi wao waliuawa na zaidi ya laki saba (700,000) kulazimishwa kuondoka katika ardhi zao hali iliyopelekea waishi katika makambi ya wakimbizi tatizo ambalo hadi sasa bado halijapata ufumbuzi.

Hadi kufikia mwaka 2017 kuna idadi ya Wakimbizi milioni Saba wa Kipalestina sehemu mbali mbali Duniani ambao Israel imewanyima haki ya kurudi katika maeneo yao. Katika vita hiyo Israel iliongeza ukubwa wa ardhi kutoka asilimia 55 hadi 77. Wapalestina walibaki na asilimia 23 tu ya ardhi inayojumuisha eneo la Ukingo wa Magharibi (West bank) na Ukanda wa Gaza (Gaza Strip). Tukio hili linakumbukwa na Wapalestina kama Nakba ( Janga) au catastrophe kwa kiingereza na huko Israel siku ya Nakba husherehekewa kama kumbukumbu ya kuanzishwa kwa Taifa la Israel.

Maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza yalitekwa na Israel mwaka 1967 katika vita ya siku sita (Six day war) kati ya Israel na Mataifa ya Kiarabu ya Misri, Lebanon, Jordan na Syria. Israel iliruhusu Walowezi wa Kiyahudi kujenga makazi katika maeneo hayo ambapo makazi hayo yanachuliwa kuwa sio halali na sehemu kubwa ya Jumuiya ya Kimataifa.

Wapalestina waliendeleza harakati za kujikomboa kwa kuanzisha vyama vya ukombozi vya PLO (Palestine Liberation Organisation) kilichoanzishwa 28 May 1964 chini ya Yasser Arafat, sasa hivi PLO inaongozwa na Mahmoud Abbas (Abuu Mazen). Chama kingine ni HAMAS kilichoanzishwa mwaka 1987 chini ya Ahmed Yasin na Abdel Aziz al Rantiss, kwa sasa Chama hicho kinaongozwa na Ismail Haniya, waziri mkuu wa zamani wa Palestina . Chama cha Hamas kimejizatiti zaidi katika eneo la ukanda wa Gaza wakati chama cha PLO kikiwa na Ushawishi mkubwa katika eneo la ukingo wa Magharibi wa mto Jordan (West bank).

Kutokana na kuimarika kwa harakati za Mashambulizi ya Hamas kupitia tawi lao la kijeshi la Izzudin al Qassam brigades linaloongozwa na makamanda shupavu Mohammed Deif na Marwan Issa dhidi ya Walowezi wa Kiyahudi huko Gaza, Israel ililazimika kujiondoa Gaza na kubomoa makazi yote ya Walowezi wa Kiyahudi. Hatua hiyo iliipa Hamas hatamu ya uongozi katika Ukanda wa Gaza. Hata hivyo tangu Mwaka 2005 Israel kwa kushirikiana na Misri zimeendelea kuiwekea vikwazo Gaza kwa kuiwekea Mzingiro wenye lengo la kuzuia uingizaji wa silaha na harakati za wapiganaji wanaoingia na kutoka kwenye eneo hilo. Mzingiro huo umeleta madhara makubwa kwa wananchi wa Gaza kwa kulifanya eneo hilo kukosa mahitaji mengi muhimu ya kibinadamu kama mafuta, nishati ya umeme, na uagizaji wa bidhaa za viwandani kutoka nje.

Kujitoa kwa Israel kutoka ukanda wa Gaza (Unilateral Withdrawal) ilikuwa mwanzo wa taifa hilo la Kiyahudi kuanza harakati kubwa za ujenzi wa makazi ya Walowezi wa kiyahudi katika eneo la ukingo wa magharibi (West bank) ukiwemo mji wa Jerusalem Mashariki ambao Wapalestina wanatarajia kuwa ndio utakaokuwa Mji mkuu wa Taifa lao. Hadi mwaka 2017 idadi ya Walowezi wa Kiyahudi katika eneo hilo inafikia laki tano (500,000) ambapo Israel imeshasisitiza kuwa Jerusalem kamwe haitagawanyika na ndio mji wao mkuu wa milele. Ukiondoa Marekani ambayo Mwezi Desemba 2017 kupitia Rais Donald Trump imetangaza rasmi kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel na kuagiza Ofisi za ubalozi wa Marekani zihamishiwe Mjini Jerusalem kutoka jijini Tel Aviv, bado jumuiya ya Kimataifa imeendelea kutotambua msimamo huo wa Israel ambapo nchi nyingi zimefungua balozi zao Mjini Tel Aviv.

Eneo la West bank lina kumbukumbu Muhimu sana kwa dini za Kiyahudi, Kiislamu na Kikristo kutokana na kuwa na urithi wa maeneo matakatifu kwa dini hizo kama vile Misikiti ya Al Aqsa (The dome of the rock) na Haram al sharif (Temple mount) inayopatikana mjini Jerusalem, pia kuna Church of the Holy Sepulchre. Maeneo mengine ni Msikiti wa Ibrahim (Cave of the Patriarchs) mjini Hebron na Church of Nativity mjini Bethlehem ambako ndipo inasemekana alizaliwa Yesu Kristo.

JE WAISRAEL WATAENDELEA KUIKALIA ARDHI YA PALESTINA MILELE?
Ni swali linalosumbua sana Wanasiasa wa Israel kutokana na wingi wa makazi ya Walowezi wa kiyahudi kwenye ardhi ya Palestina huko ukingo wa Magharibi. Vyama vya siasa vya mrengo wa Kushoto, kati na kulia vimekuwa na mitazamo na sera tofauti kuhusiana na hatima ya makazi ya Walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Palestina.

Misimamo ya vyama vya mrengo wa kulia:
Chama cha Likud chenye Wabunge 30 kati ya Wabunge 120 katika bunge la Israel (Kneset) kinachoongozwa na Waziri mkuu Binyamin Netanyahu, Bayit Yehudi (Jewish Home) chenye wabunge 8 kinachoongozwa na Waziri wa Uchumi Naftali Bennett, United Torah Judaism chenye Wabunge Sita kinachoongozwa na waziri wa afya Yaakoov Litzman na SHAS chenye wabunge saba kinachoongozwa na Waziri wa Mambo ya ndani Aryeh Deri vinapinga kuanzishwa kwa taifa la Palestina. Vyama hivi vinavyoongoza serikali ya sasa ya Israel vinaunga mkono ujenzi wa makazi ya Walowezi wa kiyahudi kwenye ardhi ya Palestina. Msimamo wa vyama hivi ni kuwa na Taifa moja la Israel lenye wakazi wa jamii za Kiyahudi na Kiarabu ambao watakuwa na uhuru wa kuishi sehemu yeyote ndani ya Israel.

Kwenye kampeni za uchaguzi za mwaka 2015 Waziri Mkuu Binyamin Netanyahu akihutubia katika makazi ya walowezi wa kiyahudi ya Har Homa (Har Homa Settlements) aliahidi kujenga maelfu ya makazi ya walowezi wa kiyahudi kwenye ardhi ya Palestina na kusisitiza kuwa hatoruhusu kuundwa kwa Taifa la Palestina katika utawala wake. Naftari Bennett mtoto wa Wahamiaji wa kiyahudi kutoka Marekani na Mwanamama Ayelet Shaked (Waziri wa Sheria wa Israel) kutoka chama cha Bayit Yehudi ni wanasiasa wenye msimamo uliofurutu mipaka wanaotaka Wapalestina wote wachukue uraia wa Israel na wale wasiotaka basi waishi Israel kwa vibali maalum kama raia wa kigeni au wakimbizi. Pia wanapinga haki ya kurejea nyumbani kwa wakimbizi wa Kipalestina waliokimbia wakati wa vita vya mwaka 1948 na 1967.

Chama kingine cha Mrengo wa kulia cha Yisrael Beiteinu (Israel nyumbani kwetu) chenye wabunge 5, kinachoongozwa na Waziri wa ulinzi Avigdor Lieberman kinaunga mkono kuundwa kwa Taifa la Palestina. Chama hicho kupitia mpango wake unaojulikana kama Lieberman Plan (Populated Area Exchange Plan) kinataka Miji yote ya mipakani ya Israel yenye wakazi wengi Waarabu kama vile Umm el Fahm, Tayyibe, Ar'ar, Baqa al-Gharbiyye,Kafri Qara,Qalansawe, Kafr Qasim, Tira, Kafr Bara na Jaljulia ihamishiwe Palestina kwa kubadilishana na Makazi makubwa ya walowezi wa kiyahudi yaliyojengwa kwenye ardhi ya Palestina inayopakana na Israel kama vile Beital Illit, Ma'ale Adumin na Modi'in Illit. Kwa mujibu wa mpango huo Israel itajiondoa katika makazi mengine machache yaliyojengwa maeneo ya ndani zaidi kwenye ardhi ya Palestina.

Msimamo wa Vyama vya mrengo wa kati: Vyama vyote vya mrengo wa kati vinavyounda kundi la Zionist Union vya Hatnua chenye Wabunge watano kinachoongozwa na mwanamama Tzipi Livn, Labor cha Avi Gabbay chenye wabunge 19, Green Movement cha Yael Cohen ambacho kina mbunge mmoja na Yesh Atid chenye wabunge 11 kinachoongozwa na Mwandishi wa habari Yair Lapid, pia chama cha Kulanu cha Moshe Kahlon chenye wabunge 10 vinaunga mkono Israel kujiondoa katika maeneo ya Palestina kupitia mpango wa kuanzishwa kwa mataifa mawili (Two state Solution). Isipokuwa msimamo wao kuhusu hatima ya mji wa Jerusalem hautofautiani na ule wa vyama vya mrengo wa kulia ambao unasisitiza kuwa Jerusalem isiyogawanyika ndio mji mkuu wa milele wa Israel. Pia vyama hivyo vinaunga mkono ujenzi wa ukuta (Separation wall ) utakaotenganisha eneo la Palestina la West bank na Israel.Mpango wa kujenga Ukuta ulianzishwa na Waziri mkuu wa zamani hayati Ariel Sharon lakini haukuweza kukamilishwa hadi sasa.

Msimamo wa vyama vya mrengo wa kushoto: Vyama vya mrengo wa kushoto vinavyounda United Arab Joint List vya Hadash (The Democratic Front for Peace and Equality) chenye wabunge watano kinachoongozwa na Ayman Odeh, Balad (National democratic assembly) chenye wabunge watatu kinachoongozwa na Jamal Zahalka, Ta'al (Arab Movement for Renewal) chenye wabunge wawili kinachoongozwa na Ahmad Tibi, na United Arab List chenye Wabunge watatu kinachoongozwa na Masud Ghnaim vinapinga ujenzi wa Makazi la walowezi kwenye ardhi ya Palestina, pia vinataka kuundwa kwa taifa la Palestina ambalo mji wake mkuu utakuwa Jerusalem Mashariki. Pia msimamo wa chama cha Wayahudi cha Meretz chenye wabunge watano kinachoongozwa na Zehava Gal-On hautofautoani sana na Msimamo wa vyama vinavyounda United Arab List.

Kutokana na tofauti hizo za kimitazamo baina ya vyama vya siasa vyenye nguvu kuhusu namna ya kutanzua mgogoro wa Palestina na suala la Makazi ya walowezi wa kiyahudi, uhakika wa Walowezi hao kuendelea kuikalia ardhi ya Palestina ni mdogo kwani Wakati wowote wanaweza kuondolewa kutegemea na sera za chama kilichopo Madarakani na makubaliano yatakayofikiwa baina ya Wapalestina na Waisrael.

NINI SULUHISHO LA KUDUMU LA HUU MGOGORO.
Kutokana na sababu za kihistoria, jamii zote mbili za Wayahudi (Waisrael) na Waarabu (Wapalestina) zina haki ya kuishi katika eneo hilo na kumiliki ardhi. Kila upande unapaswa kutambua na kuheshimu haki za upande mwingine. Mgogoro huu unaweza kutatuliwa kwa njia mbili tu ambazoni ni ama kuwa na Taifa moja lenye watu wa jamii mbili zenye kuishi pamoja (One state solution) au kuwa na mataifa mawili ya jamii mbili zinazopakana (Two state Solution) kama ilivyoamuliwa mwaka 1948 na Umoja wa Mataifa.

Wazo la kuwa na Taifa moja (One state solution):
Halikubaliki miongoni mwa Wapalestina ambao wana hofu kuwa hatua hiyo itawafanya wapoteze utambulisho wao na kufanywa watu wa daraja la pili nchini Israel. Kwa upande wa Israel wazo hili linakubalika zaidi na wanasiasa wa mrengo wa kulia nchini Israel ambao wanataka kuiona Israel ikiwa ni taifa moja. Wasichokitaka wanasiasa hao wa mrengo wa kulia ni haki ya Wakimbizi wa Kipalestina zaidi ya 7000,000 walioko nje ya Israel kuruhusiwa kurejea nchini humo.Hofu yao ni kwamba Waarabu watakuwa wengi (Majority) kuliko Wayahudi hivyo kupoteza hadhi ya Israel kuwa taifa Kiyahudi ( Jewish state )

Wazo la Kuwa na Mataifa Mawili (Two state solution)
Linakubalika kwa Wananchi na Wanasiasa wengi wa pande zote mbili. Kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa mpango huu ni hatma ya mji wa Jerusalem na Makazi (Settlements) ya Walowezi wa kiyahudi yaliyojengwa katika ardhi ambayo Palestina wanatarajia ndio iwe nchi yao. Ikiwa Palestina wataendelea na dai lao ya kutaka Jerusalem Mashariki kuwa mji mkuu, Israel inaweza kumaliza mgogoro kwa kuamua kuitwaa Jerusalem, kuondoa Makazi ya walowezi, kujenga mpaka wa ukuta utakaotenganisha Israel na eneo la Palestina la ukingo wa magharibi na kisha kuondoa wanajeshi wake kutoka ukingo wa Magharibi bila kushauriana na upande wowote (Unilateral Withdrawal). Kwa hatua hii Palestina itakuwa imepoteza dai lake la mji wa Jerusalem huku ikirejesha maeneo mengine yote yaliyokuwa yanakaliwa.

SULUHISHO LINALOKUBALIKA KIMATAIFA
• Ni Israel kukaa meza moja na nchi za Palestina na Jordan ili kujadili na kufikia makubaliano juu ya hatma ya Wayahudi kufanya Ibada na kuzuru maeneo matakatifu yaliyopo Jerusalem Mashariki.

• Kuondoa Makazi (Settlements) yote ya walowezi wa kiyahudi kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi.

• Kujiondoa kijeshi katika ardhi yote ya Palestina kwa kurudisha majeshi yake hadi kwenye mpaka wa Mwaka 1967 kabla ya vita ya siku sita. (1948 Armistice border)

• Kuondoa mzingiro uliowekwa dhidi ya Wapalestina huko Ukanda wa Gaza.

Kwa kufanya hivyo Palestina itakuwa huru. Mgogoro wa haki ya Wakimbizi wa Kipalestina kurudi nchini mwao utakuwa umemalizika na nchi hizo mbili zitaweza kuishi pamoja ambapo Jerusalem Magharibi itakuwa mji mkuu wa Israel na Jerusalem Mashariki itabaki kuwa mji mkuu wa Palestina.
 
HIVI NDIVYO MTAKI MSALITI ALIVYOUDONDOSHA UTAWALA WA CHIFU MKWAWA.

Jina lake ni Mtwa Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga, mtoto wa Chifu Munyigumba. Ukitaka kumzungumzia wala usizunguke sana, sema tu Chifu Mkwawa inatosha.

Kwa nini aliitwa Mkwawa? Hilo linatokana na jina lake “Mkwavinyika” ambalo lilifupishwa na kutamkwa “Mkwava” lakini baadaye watu wakaona ni rahisi zaidi kuita “Mkwawa” kisha ikazoeleka hivyo. Jina mashuhuri kabisa “Chifu Mkwawa.”

Alikuwa na mbinu nyingi za kupigana na kujilinda. Alitengeneza mfumo mzuri wa usalama na alijua jinsi ya kuwakabili Wazungu waliofanya majaribio kadhaa ya kumvamia wakiwa na bunduki pamoja na mizinga. Wajerumani mpaka leo hawawezi kumsahau Mkwawa.

Alikuwa chifu wa himaya ya Wahehe ambayo ndiyo Iringa ya leo na alisambaza mtandao wake wa kichifu kuanzia Kusini mpaka eneo la kati ya Tanzania ya leo, alisalitiwa na mtu aliyemwamini sana, aliyeitwa Mtaki Mwanyenza.

Mtaki hakuwa Mhehe, asili yake ni Mnyamwezi wa Tabora. Alifika Kalenga, yalipokuwa makao makuu ya Serikali ya Chifu Mkwawa, alipowapeleka Waarabu, aliotoka nao Tabora. Waarabu hao walikuwa wanatafuta watumwa,

Mtaki alikuwa mtu mjanja, aliyekuwa na uwezo kujua lugha tofauti na alikuwa anafahamu sifa za himaya ya Chifu Mkwawa, kwamba ina watu wenye nguvu waliowatandika Wajerumani kisawasawa.

Waarabu kwa kuongozwa na Mtaki, walifika mpaka Kalenga, wakakutana na Mkwawa. Katika mazungumzo yao, Mkwawa aliwaambia hawezi kuuza watu. Alisema watu wa himaya yake wote walikuwa sawa, hivyo hakukuwa na mwenye upungufu wa kutosha kuuzwa kama mtumwa.

Baada ya biashara hiyo ya watumwa kutofanyika, walifanya biashara tofauti. Mkwawa aliwauzia Waarabu pembe za ndovu na ngozi za wanyama mbalimbali wa porini kama simba, chui, nyati na kadhalika.

Biashara hiyo ilipofanyika, jambo lingine lilifuata. Mkwawa alipenda ustaarabu wa Waarabu, uvaaji wao hasa ufungaji wa kilemba. Ni hapo Chifu Mkwawa alisilimu kisha akaanza kuvaa kilemba na mavazi mengine aliyoiga kwa Waarabu.

Mkwawa hakuwa mbinafsi, aliwapenda sana watu wake. Zile pembe za ndovu na ngozi za wanyama ambazo aliwauzia Waarabu, walibadilishana na nguo ambazo ziligawanywa kwa watu wa himaya ya Mkwawa. Kihistoria watu wa himaya ya Mkwawa ni miongoni mwa jamii za kwanza Afrika Mashariki kuvaa nguo.

Mtaki alipofanikiwa kuwaunganisha Mkwawa na Waarabu, aliona kuna fursa katika kuwa karibu na Mkwawa. Alianza kwa kumshauri Mkwawa jenge boma la makazi ya chifu ambalo linakuwa limezungushiwa uzio mkubwa wa ukuta. Kabla ya hapo, makazi ya Chifu Mkwawa yalikuwa hayajazungushiwa.

Katika kumjengea hoja, Mtaki alimweleza namna ambavyo maboma mbalimbali ambayo yalikuwa makazi ya watawala wengine yalivyokuwa. Mkwawa alivutiwa na ushauri huo, akakubali kujenga.

Ushauri mwingine kutoka kwa Mtaki kwenda kwa Mkwawa ulikuwa ni kumuoa mtoto wa Mtemi Isike wa Tabora, aliyeitwa Ilagila binti Isike. Mkwawa alipomuoa Ilagila, alimuona Mtaki ni mtu mzuri kwake, akampenda na kumwamini.

Chifu Mkwawa aliamua kumtawaza Mtaki kuwa ni Mhehe na kwa vile Wahehe walikuwa na koo zao, Mkwawa alimtangaza Mtaki kuwa Mhehe wa koo ya Mwanyenza. Ndipo hapo alianza kuitwa Mtaki Myanyenza.

Utaratibu wa vyeo katika utawala wa Mkwawa, alikuwepo chifu mkuu ambaye ndiye Mkwawa, vilevile walikuwepo machifu wasaidizi ambao walifahamika kwa jina la Wanzagila.

Hao Wanzagila walikuwa viongozi wa kanda katika utawala wa Mkwawa. Kulikuwa na kanda nne na kila kanda ilikuwa na Mnzagila (chifu msaidizi). Wanzagila walikuwa wakiripoti kwa Mkwawa. Utaratibu huo ulimfanya Mkwawa atawale kwa urahisi zaidi.

Mkwawa alipomshiba Mtaki, aliamua kumteua naye kuwa Mnzagila lakini hakumpa eneo la kutawala, bali alimfanya kuwa Mnzagila maalum. Jukumu alilompangia lilikuwa usimamizi wa ujenzi wa boma la makazi ya Chifu Mkwawa ambalo liliitwa Lipuli. Ujenzi ulifanyika na kukamilika. Chifu Mkwawa alianza kuishi ndani ya Lipuli.

MKWAWA NA WAJERUMANI

Kabla ya Mtaki na Waarabu kwenda kwa Mkwawa, tayari Wajerumani walikuwa wameshakiona cha mtema kuni kutoka kwa Mkwawa. Hata kipindi Mtaki alipopokelewa na Mkwawa na kuaminiwa, Wajerumani walikuwa wametulia wakitamani ipatikane namna yoyote kuusambaratisha utawala wa Mkwawa.

Historia ipo hivi; mwaka 1885 baada ya kukamilika kwa Mkutano wa Berlin, uliohusu wakuu wa nchi za Ulaya kukutana na kujadiliana jinsi ya kugawana kanda za utawala barani Afrika, Ujerumani ilianza kujitandaza Tanzania Bara (Tanganyika).

Mkutano wa Berlin, ulifanyika kuanzia mwaka 1884 mpaka 1885, Berlin, Ujerumani. Kumalizika kwa mkutano huo, kulisababisha sasa Wazungu kuvamia Afrika. Wajerumani walipowasili Tanzania walianza kueneza ukoloni na kuzifanya tawala mbalimbali za jadi zilizokuwepo zisalimu amri.

Kati ya mwaka 1888 na 1889, Wajerumani walipata wakati mgumu katika Vita ya Abushiri ambayo ilihusu eneo la Pwani ya Tanzania Bara. Ni eneo ambalo pamoja na uwepo wa wenyeji, lilikuwa na Waarabu ambao walikuwa wamelowea. Wenyeji asilia walipambana hasa na Wajerumani.

Mwaka 1889 Wajerumani walifanikiwa kulidhibiti eneo la Pwani ya Tanzania Bara (Tanganyika), baada ya hapo wakaanza kumpigia mahesabu Mkwawa ambaye utawala wake ndiyo ulikuwa bado haujasalimu amri.

Wajerumani walianza maandalizi ya kumvamia Mkwawa. Mwaka 1891 walijipanga kutekeleza oparesheni ya kuubomoa utawala wa Mkwawa. Safari ya Wajerumani kutoka Dar es Salaam kwenda himaya ya Mkwawa, ilianza Julai 1891.

Kikosi cha Ujerumani kiliongozwa na Mkuu wa Majeshi wa Ujerumani-Tanganyika, Emil von Zelewski, kilikuwa na askari takriban 500, Wajerumani wakiwa zaidi ya 40, huku Waafrika waliotekwa na kupewa mafunzo ya kijeshi na kufanywa askari wa vikosi vya Ujerumani wakiwa zaidi ya 460.

Mkwawa alikuwa na mfumo wa siri wa usalama. Kila kijiji kilikuwa na ofisa usalama ambao waliitwa Watandisi. Wajerumani wapoanza kuingia himaya ya Mkwawa. Mtandisi wa kijiji cha kwanza alikimbia mpaka kijiji cha pili na kumjulisha mtandisi wa eneo hilo kuhusu kuingia kwa Wazungu ambao waliwaita Walangala.

Hivyo, mtandisi wa kijiji cha pili alimfikishia wa kijiji cha tatu, hivyohivyo mpaka mtandisi wa mwisho alipomfikia Mkwawa ambaye alikwenda kwenye ngome yake ya kijeshi,Kalenga, akawaandaa wapiganaji wake.

Watandisi walikuwa watu wenye mbio na walijua njia za mkato, kwa hiyo walifikisha taarifa mapema na jeshi la Mkwawa lilijiandaa kabla ya Wajerumani hawajakaribia makao makuu.

Ni kwamba Wajerumani walimdharau Mkwawa, kwa hiyo hawakujua kama anaweza kuwa na mfumo mkali wa usalama. Walimuona ni kiongozi dhaifu ambaye wapiganaji wake walitumia mikuki na pinde wakati wao walikuwa na bunduki pamoja na mizinga.

Wajerumani walipokuwa njiani walishambulia na kuua watu waliokosa hatia. Walikutana pia na mabalozi watatu wa Mkwawa ambao walitumwa na Chifu Mkwawa ili wazungumze kupata suluhu lakini Zelewski aliagiza wauawe bila kuzungumza nao chochote.

Eneo la pori la Lugalo ndipo Mkwawa na askari wake zaidi ya 300 walijificha kimya. Wajerumani walipovuka Mto Ruaha, walianza kufuatiliwa na walipoingia Lugalo, walijikuta wanavamiwa na kushambuliwa.

Kwa vile walikuwa hawajaandaa bunduki zao, walijikuta wanapigwa kila upande japokuwa walijitahidi kujibu mashambulizi. Wajerumani 40 waliuawa akiwemo bosi wao Zelewski. Baada ya kuwa wamewazidi nguvu, Mkwawa aliagiza Waafrika waliokuwepo kwenye msafara huo wa Ujerumani wasiuawe.

Sababu ni kuwa waliteka bunduki nyingi pamoja na mizinga ambayo wao hawakuwa na utaalamu wa kuitumia. Alitaka Waafrika wabaki hai ili watumike kuwafundisha askari wa jeshi lake jinsi ya kutumia silaha hizo za moto.

Siku ambayo Wajerumani walikomeshwa na Mkwawa Lugalo ni Agosti 17, 1891. Na kwa kumbukumbu hiyo, ikawa sababu ya Kambi ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam, kupewa jina hilo.

Baada ya kuwa na silaha hizo, Mkwawa alianza kuweka utaratibu wa kwenda kushambulia ngome nyingine ambazo zilikuwa zimeshatekwa na Wajerumani ili kujilinda zaidi, hakutaka wawe karibu. Mashambulizi hayo yalizidi kuwatia hasira Wajerumani.

MKWAWA ALIVYOSALITIWA

Baada ya kukamilisha ujenzi wa Lipuli, Mkwawa alimwagiza Mtaki kwenda Dar es Salaam ili akutane na Wajerumani, waeleze mahitaji yao ni nini maana walikuwa wakipigana bila kujua Wajerumani walichohitaji.

Alimteua Mtaki kwa sababu alimuona mjanja-mjanja na kwa vile aliweza kuzungumza na Waarabu, kwa hiyo ilikuwa rahisi kwake kuelewana na Wajerumani. Safari ya Mtaki kwenda Dar es Salaam ikaanza. Huo ulikuwa mwaka 1898.

Mtaki alipofika Dar es Salaam alikutana na Waarabu ambao walimuunganisha na Wajerumani. Mtaki alipojitambulisha kuwa anatoka kwa Mkwawa kwanza hakuminika, aliulizwa maswali mengi na baada ya kuthibitisha walimrubuni.

Wajerumani walimweleza Mtaki kuwa wao wasingeweza kufanya mazungumzo yoyote na Mkwawa kwa sababu aliliaibisha taifa lao hasa kwa akitendo cha kumuua Zelewski. Wajerumani walimshawishi Mtaki akubali kuwapa siri za namna ya kumpindua Mkwawa na baada ya hapo, yeye angefanywa Chifu wa Wahehe.

Ahadi hiyo ya kufanywa Chifu wa Wahehe ilimsisimua Mtaki. Akamwaga siri zote za namna ya kumvamia Mkwawa bila kushtukiwa. Hakuishia hapo, Mtaki aliwaongoza Wajerumani kupitia njia isiyo na ulinzi ya Ifakara, Mgololo, Mufindi mpaka makao makuu ya utawala wa Mkwawa.

Njiani Wanzagila walipomuona Mtaki yupo na Wajerumani wala hawakushtuka, walijua ndiyo alikuwa anawapeleka kwa Mkwawa kwa ajili ya mazungumzo, hawakujua kuwa tayari Mtaki alikuwa ameshauza utawala wao.

Bila kutarajia, Mkwawa alishtuka Kalenga inalipuliwa na mizinga ya Wajerumani. Himaya ya Mkwawa ilidhibitiwa kila upande. Mkwawa baada ya kuona hana namna yoyote na kwa vile alikataa aibu ya kukamatwa na kuteswa na Wajerumani, aliamua kujipiga risasi iliyofumua kichwa. Hiyo ilikuwa Julai 19, 1898.

Ni Mtaki ndiye aliyemtambua Mkwawa na kuwathibitishia Wajerumani kuwa ndiye mwenyewe. Wajerumani walimkata kichwa na fuvu lake kwenda kuliweka kwenye makumbusho ya Ubersee, Bremen, Ujerumani, kabla ya Julai 9, 1954, kurejesha fuvu hilo la Mkwawa na kuhifadhiwa kwenye Jumba la Makumbusho la Mkwawa, Kalenga, Iringa.

Baada ya Mkwawa kuuawa, Wajerumani hawakutimiza ahadi ya kumpa Mtaki uchifu wa himaya yote ya Wahehe. Waliamini kuwa kama aliweza kumsaliti Mkwawa, basi angeweza kuwasiliti Wajerumani wakati mwingine kama angeshawishiwa.

Himaya ya Wahehe ikagawanywa mara nne, ili wawe viongozi wenye himaya ndogondogo na kufanya kazi kwa muongozo wa Wajerumani. Uhehe Kati, kiongozi wake alikuwa Lusinde Mwang’ingo, Kaskazini-Magharibi, alipewa Msengidunda Mwamgongolwa, Kaskazini-Mashariki, Msatima Mwakindole na
 
*KUTANA NA KESI ILIYOLITIKISA TAIFA, KESI YA DORIS LIUNDI, YENYE HUKUMU YA KIFO KWA KUNYONGWA.*

Majira ya asubuhi mnamo Februari 21, 1978. Ni baada ya kuambiwa mumewe wakati anaenda kazini kwamba akirudi asimkute hapo nyumbani, na kama akimkuta, atamtoa hapo nyumbani kwake uchi. Alikuwa na watoto wao wanne hapo nyumbani. Baada ya mumewe kuondoka, na yeye aliondoka na gari kuelekea mjini ambapo alinunua chupa kadhaa za sumu ya kuulia wadudu.

Alipofika nyumbani kwake, aliwaita watoto wake wote wanne chumbani kwake na kujifungia nao ndani, kisha akawaambia "tunaondoka" watoto wale walimuuliza, "tunakwenda wapi?" yeye akawajibu, "tunasafiri, lakini huko tunakokwenda hatupajui." Aliwabusu watoto wale na wao wakambusu mama yao na kisha wakapeana mikono kama ishara ya kutakiana safari njema. Baada ya tukio hilo, aliwapa kila mmoja kikombe chenye mchanganyiko wa ile sumu na Orange Squash na yeye akachukua mchanganyiko huo uliokuwa kwenye kikombe na kunywa. Baada ya kunywa mchanganyiko huo wote walianza kutapika, kutokana na kutapika huko, aliamua kunywa Iodine. Pia alikunywa vipande vya chupa zilizosagwa na kujifungia katika chumba kingine.

Mfanya kazi wake wa hapo nyumbani aitwae Ramadhan na mtu mwingne aliyetajwa kwa jina la Bibie waliwasikia watoto wakilia huko chumbani. Baadae kidogo alifungua mlango na kumwambia Bibie amuoshe mmoja wa watoto wale ambaye alikuwa ni mdogo kwa wenzie kwani alikuwa anatapika na kuharisha kisha akarudi ndani na kujifungia katika chumba hicho peke yake.

Aliombwa na Ramadhan pamoja na Bibie watumie simu ya pale nyumbani kumjulisha mumewe juu ya tatizo lile lakini alikataa.

Wale watoto wengine watatu nao walianza kutapika na kuharisha na hali zao zilibadilika na kuwa mbaya. Ramadhan aliwajulisha majirani na walipofika, yeye alikwenda hadi chumba cha pili alipokuwa amejifungia na kumuuliza kama ni kitu gani kimewatokea wale watoto. Alimwambia, "Ramadhan, naomba uniache nife na watoto wangu, kwa sababu baba Taji (yaani Mumewe) hanipendi."

Wote walikimbizwa hospitalini na watoto watatu waliripotiwa kufariki lakini yeye na mwanaye mkubwa madaktari walifanikiwa kuyanusuru maisha yao.

Taarifa ya kitabibu ilithibitisha kwamba wale watoto watatu walifariki kutokana na kunywa sumu, ambayo walinywesha na mama yao.

Kesi hii ni ya mwaka 1979 ya Agnes Doris Liundi, alishitakiwa na Jamhuri kwa kosa la kuwauwa watoto wake watatu kwa kuwanywesha sumu hapo mnamo tarehe 21 Februari 1978 nyumbani kwake. Kosa hilo la Kuua kwa kukusudia (Murder) limeainishwa kwenye kanuni ya adhabu (Penal Code) kifungu cha 196.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyosomwa pale mahakamani wakati wa kusikilizwa kwa kesi hii ilielezwa kwamba, Agnes Doris Liundi aliolewa na George Liundi mnamo Februari 1967.

Baada ya miaka miwili ya maisha yao ya ndoa iliyokuwa na furaha na amani, ghafla kukazuka kutoelewana na ugomvi usiyoisha kati ya wanandoa hao. Sababu iliyoelezwa kusababisha kutokuelewana huko ni hofu aliyokuwa nayo mume kuwa huenda mkewe siyo muaminifu kwake.

Kutokana na ugomvi huo, mtuhumiwa alifukuzwa hapo nyumbani kwao na mumewe.

Kama wiki moja hivi kabla ya kutekeleza mauaaji hayo, Mtuhumiwa na mumewe walihudhuria sherehe fulani. Wakiwa hapo kwenye hiyo sherehe ndipo mumewe alipomuona mwanaume mmoja ambaye alimtuhumu kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe na ndipo ule uhasama wao ukaibuka upya na kukazuka ugomvi mkubwa kati yao, yaani mtuhumiwa na mumewe, na ndio ukapelekea mtuhumiwa kutekeleza mauaji hayo siku ya tarehe 21, Februari 1978.

Ilielezwa pale mahakamni kwamba, kabla ya kutekeleza mauaji hayo, mtuhumiwa aliandika barua nne na zote zilikuwa na tarehe hiyo ya 21 Februari 1978, na barua hizo ziligunduliwa na Polisi na zilifikishwa pale mahakamani kama kidhibiti. Barua tatu zilikuwa zimendikwa kichwa cha habari kisemacho, "kwa yeyote anayehusika," na moja ilikuwa inamuhusu mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la mama Gaudensia ambaye ni rafiki wa mtuhumiwa.

Barua moja kati ya zile tatu zilizoandikwa kichwa cha habari kisemacho "Kwa yeyote anayehusika" ilisomwa pale mahakamani kama ifuatavyo:

c/o Box 9050
DAR ES SALAAM

21/2/1978

KWA YEYOTE ANAYEHUSIKA

Uamuzi niliouchukuwa ni wa mwisho. George mume wangu naomba asisumbuliwe au kuteswa au kulazimishwa kwa namna yoyote kwa sababu nilikuwa nampenda.

Nimewachukuwa wanangu kwa sababu sitaki wateseke kama nilivyoteseka katika upweke wa kutisha. George mume wangu, hukujua ni kiasi gani nilikupenda nilipokuwa hai. Lakini sasa unaelewa.

KWA AFISA WA POLISI

Tafadhali msimchukulie mume wangu hatua yoyote kwa sababu hana hatia.

Kwa mujibu wa maelezo yake aliyoandikisha Polisi hapo mnamo 3 April 3, 1978, ikiwa ni miezi miwili baada ya tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa alieleza historia ya maisha yake tangu utotoni. Alieleza jinsi alivyoishi maisha ya tabu na mashaka baada ya mama yake kufariki ambapo alililelewa kwa mateso na upweke na mama yake wa kambo.

Mtuhumiwa alielezea maisha yao ya ndoa na mumewe yalivyokuwa na furaha na amani kwa kipindi cha miaka miwili tangu waoane, na jinsi maisha yalivyobadilika na ndoa yake kukumbwa na misukosuko isiyoisha.

Alisema kwamba, matatizo yalianza baada ya yeye kudai kwamba aliwahi kubakwa na kaka wa mmoja wa marafiki zake, na kutokana na kitendo hicho alimuambukiza mumewe maradhi ya zinaa. Hakuthubutu kumweleza mumewe kuhusu tukio hilo la kubakwa kwa muda mrefu alitunza siri hiyo, lakini baadae aliaamua kumweleza mumewe, jambo ambalo lilimletea matatizo makubwa katika ndoa yake mpaka kupelekea tukio hilo la tarehe 21 Februari 1978.

Wakati mumewe anaondoa hapo nyumbani siku hiyo ya tarehe 21 Februari 1978, mtuhumiwa alichanganyikiwa na alianza kukumbuka maisha yake ya utotoni jinsi yalivyokuwa ya mateso na kujikuta akiwa hana pa kwenda. Alimuona mumewe kama mama yake, baba yake, kaka yake na dada yake na maisha yake yote alikuwa akimtegemea mume wake huyo.

Aliamua kwenda kununua sumu na kurudi nayo nyumbani, alijaribu kulala lakini hakupata lepe la usingizi na hakupata suluhu, nini cha kufanya kuhusiana na jambo hilo, na ndipo alipoamua kunywa hiyo sumu.

Kwa maelezo yake mwenyewe alisema:

"Nilikuwa na hasira na wasiwasi kuhusiana na matatizo kati yangu na mume wangu. Nilijiuliza, ina maana matatizo haya yamefikia hatua ya kutisha kiasi cha mume wangu kufikia hatua ya kunifukuza. Nilijiwa na wazo kwamba, acha nijimalize (Kujiuwa) mwenyewe niwaache wanangu wakiwa hai. Lakini baadae nilianza kukumbuka maisha yangu ya utotoni jinsi yalivyokuwa ya mateso na upweke, na nilijiuliza kwamba huenda na wanangu nao wataishi maisha kama yangu kwa kuishi na mama wa kambo. Kwa kuwa mume wangu aliniambia nitakapoondoka nihakikishe siwaachi wanangu nyuma, niliamua kuwachukuwa na kuingia nao chumbani na kufunga mlango. kisha nikawaambia "tunaondoka" wakaniuliza, "tunakwenda wapi?" nikawajibu, "tunasafiri, lakini huko tunakokwenda hatupajui." Kisha nikawabusu na wao wakanibusu, wakapeana mikono kama ishara ya kutakiana safari njema. niliwapa kila mmoja kikombe chenye mchanganyiko wa ile sumu na Orange Squash na mimi nikachukua mchanganyiko huo uliokuwa kwenye glasi na kunywa. Baada ya kunywa mchanganyiko huo wote tulianza kutapika, kutokana na kutapika huko, aliamua kunywa Iodine. Pia nilikunywa vipande vya chupa zilizosagwa na kujifungia katika chumba kingine. Kutoka muda huo, nilipoteza fahamu na sikuweza kutambua kilichotokea baada ya hapo"

Wakati alipokamatwa mtuhumiwa alikuwa chini ya uangalizi wa daktari aliyejulikana kwa jina la Dk. Haule, huyu ni mtaalamu wa magonjwa ya akili aliyekuwa akifanya kazi katika Hospitali ya Muhimbili.

Aliwasilisha ripoti yake pale mahakamani na pia alitoa ushahidi wake pale mahakamani. Kwa kifupi katika maoni yake Dk. Haule alisema kwamba, wakati akitekeleza tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya, alikuwa anajua kwamba anawauwa watoto wake kwa kuwalisha sumu, lakini hakujua kwamba kufanya kitendo hicho ni kosa.

Kwa mujibu wa vifungu vya 12 na 13 vya sheria ya kanuni ya adhabu ambavyo vinahusika na swala hili la uwendawazimu vinaeleza kama ifuatavyo:

Kifungu cha 12. Sheria inamchukulia mtu yeyote kuwa ni mwenye akili timamu kwa wakati wowote mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo.

Kifungu cha 13. Mtu yeyote hawezi kuchukuliwa kuwa ametenda kosa kama kutenda kwake au kutokutenda kwake na katika muda wa kutenda au kutokutenda alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa na akili na hivyo kumfanya kutokutambua alichokuwa anakifanya.

Dk. Haule katika ushahidi wake kwenye ripoti yake aliainisha vidokezo vifuatavyo,

Kwa mara ya kwanza alipomuona mtuhumiwa muda mfupi baada ya tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa hakuwa katika hali ya kawaida na hakuonekana kujali. "nilikuwa kama vile naongea na mti." Alisema Dk. Haule. Kwa maoni yake Dk. Haule alisema, inawezekana kwamba mtuhumiwa alikuwa katika hali ya isiyo ya kawaida kwa majuma mawili au zaidi kabla ya tukio hilo, na kwamba, mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya wakati alipokuwa akiwanywesha sumu wanae, lakini hakujua kwamba kitendo hicho ni kosa.

Alielezea juu ya kipindi kigumu cha maisha ya ndoa ya mtuhumiwa alichopitia, jinsi maisha yake ya ndoa yalivyokumbwa na misukosuko ya kutoelewana na mumewe. Nafasi aliyokuwa nayo, maisha aliyopitia utotoni na jinsi alivyokuwa akimtegemea na kumtii mumewe. Dk. Haule, alikuwa na maoni kwamba, kitendo cha mtuhumiwa kuamua kujiuwa na kuwaua wanae, aliamini kwamba, alikuwa amemriwa na mumewe afanye hivyo. Alisema kwamba, alisoma barua zilizokuwa zimeandikwa na mtuhumiwa kabla ya kutekeleza mauaji hayo lakini barua hizo hazikuweza kubadili maoni yake juu ya jambo hilo.

Wakati fulani Dk Haule alidai kwamba mtuhumiwa hakuwa na tatizo la kurukwa na akili lakini baadae alisema kwamba mtuhumiwa alikuwa na tatizo hilo.

Kwaq mamneno yake mwenyewe Dk. Haule alisema. "Alikuwa amerukwa na akili, na aliona kitendo alichokifanya kilikuwa kinakubalika."

Dk. Haule alisema kwamba, mwaka mmoja baada ya tukio hilo hali ya mtuhumiwa iliimarika, kiasi cha kujua kwamba, kitendo alichokifanya kilikuwa ni kosa, lakini bado alikuwa kwenye matibabu.

Katika kesi hii mwanasheria aliyekuwa akimtetea mtuhumiwa alikuwa ameegemea kwenye utetezi wa uwendawazimu.

Akitoa utetezi wake wakili Jadeda alisema kwamba, wakati mtuhumiwa akitekeleza mauaji hayo, hakuwa akijua kwamba kitendo anachokifanya ni kosa. Wakili huyo alirejea maoni ya Dk. Haule.

Wakili huyo alisema kwamba, mtu yeyote aliyerukwa na akili anaweza kupanga hatua kwa hatua kutekeleza mauaji kama aliavyofanya mtuhumiwa na asijue kama kitendo alichokifanya ni kosa.
Wakili Jadeda alikuwa akipinga maoni ya upande wa mashitaka kwamba, mtuhumiwa alikuwa kijua kitendo anachokifanya ni kosa.

Akisoma hukumu Mheshimiwa Jaji Makame alikubaliana na swala la mtuhumiwa kuwa na dhamira ovu (Malice aforethought), hasa kwa kuangalia vitendo vya mtuhumiwa tangu maandalizi, dhamira na akiwa na utambuzi kwamba, akiwanywesha wanae sumu itawasababishia kifo, na hiyo inadhihirisha kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya, na si lazima ajue kwamba kufanya hivyo ni kosa.

Hata hivyo Mheshimiwa Jaji Makame alikuwa ameshawishika kuamini hivyo kutokana na barua nne alizoziandika mtuhumiwa kabla ya kutekeleza mauaji hayo, ambazo aliziandika sambamba na tendo alilofanya tarehe 21 Februari 1978. Barua hizo kwa uwazi zilionyesha kabisa kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua anachokifanya ni kosa.

Kwa maneno yake Mwenyewe Mheshimiwa Jaji Makame alisema, "Katika barua ambayo ilisomwa hapa mahakamani wakati wa shauri hili, mtuhumiwa alisema wazi kwamba mumewe asije akaadhibiwa au kuteswa kwa kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa. Pia kulikuwa na ombi la mtuhumiwa kwa Polisi kwamba, wasije wakamchukulia hatua mumewe kwa sababu hana hatia."

Muheshimiwa Jaji Makame aliendelea kusema kwamba, wazo la kutokuwa na hatia na kutompa mumewe adhabu katika barua alizoandika mtuhumiwa, linadhihirisha wazi kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua kwamba kitendo anachokifanya ni kosa na alitaka kuweka wazi kuwa mumewe hahusiki kwa namna yoyote na kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa. Alijua kama mumewe akihusishwa na kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa, ataadhibiwa kwa kosa hilo.

Mheshimiwa Jaji Makame aliendelea kusema,

"Ni kweli Dk. Haule alisema kwamba, ukiachana na barua hizo alizoziandika mtuhumiwa, lakini yeye alikuwa na maoni kwamba, mtuhumiwa hakuwa anajua anachokifanya kuwa ni kosa. Alisema, barua zilimuonesha kwamba, mtuhumiwa alikuwa akimtegemea mumewe kwa kiasi kikubwa na hasa katika mahusiano yao. Kama tunamuelewa Dk. Hauli vizuri, alikuwa huenda anamaanisha kwamba, hizo barua zilikuwa na uhusiano na imani aliyokuwa nayo mtuhumiwa kwamba, alikuwa ameshurutishwa kujiuwa na kuwauwa watoto wake na mumewe. Kwa bahati mbaya barua haijaeleza kuwa mtuhumiwa alikuwa na imani ile. Ilikuwa ni ahuweni aliyoiweka Dk Hauli. Japokuwa barua ilieleza kuwa mtuhumiwa alikuwa anamtegemea sana mumewe, lakini bado zilikuwa zinathibitisha kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua kitendo anachokifanya ni kosa.
Pia nashindwa kuunganisha maelezo ya barua hizo na maoni ya kurukwa na akili yaliyotolewa na Dk. Haule, aliposema kwamba, mtuhumiwa aliamini kuwa ameamriwa na mumewe ajiuwe na kuwauwa watoto wake."

Mheshimiwa Jaji aliendelea kusema,

"Kwangu mimi, namuona Dr. Hauli kama mtaalamu mwenye uzoefu na ujuzi mkubwa wa magonjwa ya akili, pamoja na mambo mengine, pia ni mwanachama Royal College of Psychiatrists na anayo Diploma ya Psychiatric Medicine aliyoipata nchini Uingereza. Naheshimu sana maoni yake kulingana na utaalamu wake na ninashindwa kupinga ushahidi wake. Pia ninakubaliana na ukweli kwamba hata kama mtuhumiwa ataonyesha kurukwa lakini hiyo itakubalika iwapo kutakuwa na kipimo chenye uwelekeo (Balance of Probability).

Mtuhumiwa lazima aoneshe ushahidi wote; kwamba kutokuwa na akili timamu ni zaidi ya kuwa timamu. Ingawa inawezekana ikawa chini ya tunachodhamiria. Katika kuliweka sawa hili mamlaka ya kuthibitisha inafananishwa na kesi ya Nyinge Siwato Vs Jamhuri 1959 East Africa 974 ikifuatiwa mara nyingi sana ikihusishwa na MbekuleV-R. 1971, East Africa 479. Jaji Enzi zake alielezea katika kesi ya Siwato "Mahakama haifungwi kukubaliana na ushahidi wa hospitalini (Medical Testimony) kama/endapo kuna sababu madhubuti ya kutofanya hivyo. mwisho wa siku ni kazi ya mahakama kutafuta ushahidi na viambatanisho katika kufanya hivyo, ni wajibu wangu kuangalia na kulipima na ushahidi uliotolewa kabla na ikiwemo utaalam wa Daktari."

Mheshimiwa Jaji Makame akihitimisha hukumu hiyo alisema:

"Inawezekana hasa kwamba sheria yetu katika swala la kurukwa na akili imepitwa na wakati na ni ya zamani sana, Dk. Haule katika ushahidi alieleza kuwa katika utaalamu wa sasa, utofauti kati ya kurukwa na akili na kutojitambua katika utenedaji vinapingana. Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa hekima linaweza kulifanyia marekebisho hili sambamba na sheria ndogo ndogo na kulileta katika utandawazi wa kitabibu. Mipaka ya kimahakama, ikiwemo ya Afrika Mashariki wamefanya hivyo."

Mtuhumiwa katika kesi hii alihukumiwa kunyongwa.

Mama Taji alikuja kupewa msamaha na Raisi Nyerere miaka 7 baadae.

Amefariki tarehe 7 January mwaka huu.
 
MJUE RAIS MWENYE KICHAA

(Rais Mwendawazimu)

Serikali ya Ufilipino imeteketeza jumla ya magari 29 ya kifahari (19 mji wa Manila, 7 mji wa Davao na matatu mji wa Ci-ebu) yenye thamani ya dola milioni 2.9 (sawa na shilingi bilioni 6 za kitanzania) baada ya kubainika kuwa yameingizwa nchini humo kinyemela bila kulipiwa kodi. Spika wa zamani wa bunge la nchi hiyo (wao wanaita Rais wa bunge) Bw.Aquilino Pimentel amekosoa uamuzi huo na kusema serikali ingeyauza magari hayo au kuyataifisha badala ya kuyateketeza.

Lakini Rais wa nchi hiyo Rodrigo Duterte amemuonya Spika huyo na kudai kuwa atamteketeza kama magari hayo ikiwa ataendelea kutetea "wahujumu uchumi" walioingiza magari hayo nchini humo na kukwepa kodi.!
Aliwahi kusema kuwa yeye ni Adolf Hitler wa Ufilipino na aliwahi kumuua MTU kipindi cha ujana wake kwa kumpiga risasi kisa alimwangalia sana usoni.

Rais huyu huwaua wahalifu kikatili kabisa kwa kuwatupa chini kutoka kwenye ndege inayoenda kasi, anashtumiwa kwa kufanya mauaji ya ajabu sana ktk kipindi chake chote ikiwa ni pamoja na kuamrisha watu wapigwe risasi hadharani na wengine wabebwe kwenye ndege kisha watupwe chini ili wakome kabisa kufanya vitendo vya kiharifu hasa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya!

Aliwahi kuwakabidhi police wamchunguze mwanae kama kweli alikuwa akijihusisha na biasahara ya mihadarati na ikibainika kuwa ni kweli hakuna cha mahakamani bali ni kupigwa risasi hadharani tu.

Aliwahi kupiga kelele ndani ya ndege wakiwa angani kutokea Malaysia akidai kwamba ameongea na Mungu na amejulishwa kuwa Mungu angeweza kuitamiza chini ndege yao kama Rais huyo angeendelea kutoa maneno yake yenye utata na alikiri kutoropoka tena!!.

Baada ya wiki moja alianza kujijamba kuwa hufrahia sana kuua watu!!!.

Huyo ndiyo rais mtata zaidi Duniani.

Rodrigo Duterte.
 
*KUTANA NA KESI ILIYOLITIKISA TAIFA, KESI YA DORIS LIUNDI, YENYE HUKUMU YA KIFO KWA KUNYONGWA.*

Majira ya asubuhi mnamo Februari 21, 1978. Ni baada ya kuambiwa mumewe wakati anaenda kazini kwamba akirudi asimkute hapo nyumbani, na kama akimkuta, atamtoa hapo nyumbani kwake uchi. Alikuwa na watoto wao wanne hapo nyumbani. Baada ya mumewe kuondoka, na yeye aliondoka na gari kuelekea mjini ambapo alinunua chupa kadhaa za sumu ya kuulia wadudu.

Alipofika nyumbani kwake, aliwaita watoto wake wote wanne chumbani kwake na kujifungia nao ndani, kisha akawaambia "tunaondoka" watoto wale walimuuliza, "tunakwenda wapi?" yeye akawajibu, "tunasafiri, lakini huko tunakokwenda hatupajui." Aliwabusu watoto wale na wao wakambusu mama yao na kisha wakapeana mikono kama ishara ya kutakiana safari njema. Baada ya tukio hilo, aliwapa kila mmoja kikombe chenye mchanganyiko wa ile sumu na Orange Squash na yeye akachukua mchanganyiko huo uliokuwa kwenye kikombe na kunywa. Baada ya kunywa mchanganyiko huo wote walianza kutapika, kutokana na kutapika huko, aliamua kunywa Iodine. Pia alikunywa vipande vya chupa zilizosagwa na kujifungia katika chumba kingine.

Mfanya kazi wake wa hapo nyumbani aitwae Ramadhan na mtu mwingne aliyetajwa kwa jina la Bibie waliwasikia watoto wakilia huko chumbani. Baadae kidogo alifungua mlango na kumwambia Bibie amuoshe mmoja wa watoto wale ambaye alikuwa ni mdogo kwa wenzie kwani alikuwa anatapika na kuharisha kisha akarudi ndani na kujifungia katika chumba hicho peke yake.

Aliombwa na Ramadhan pamoja na Bibie watumie simu ya pale nyumbani kumjulisha mumewe juu ya tatizo lile lakini alikataa.

Wale watoto wengine watatu nao walianza kutapika na kuharisha na hali zao zilibadilika na kuwa mbaya. Ramadhan aliwajulisha majirani na walipofika, yeye alikwenda hadi chumba cha pili alipokuwa amejifungia na kumuuliza kama ni kitu gani kimewatokea wale watoto. Alimwambia, "Ramadhan, naomba uniache nife na watoto wangu, kwa sababu baba Taji (yaani Mumewe) hanipendi."

Wote walikimbizwa hospitalini na watoto watatu waliripotiwa kufariki lakini yeye na mwanaye mkubwa madaktari walifanikiwa kuyanusuru maisha yao.

Taarifa ya kitabibu ilithibitisha kwamba wale watoto watatu walifariki kutokana na kunywa sumu, ambayo walinywesha na mama yao.

Kesi hii ni ya mwaka 1979 ya Agnes Doris Liundi, alishitakiwa na Jamhuri kwa kosa la kuwauwa watoto wake watatu kwa kuwanywesha sumu hapo mnamo tarehe 21 Februari 1978 nyumbani kwake. Kosa hilo la Kuua kwa kukusudia (Murder) limeainishwa kwenye kanuni ya adhabu (Penal Code) kifungu cha 196.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyosomwa pale mahakamani wakati wa kusikilizwa kwa kesi hii ilielezwa kwamba, Agnes Doris Liundi aliolewa na George Liundi mnamo Februari 1967.

Baada ya miaka miwili ya maisha yao ya ndoa iliyokuwa na furaha na amani, ghafla kukazuka kutoelewana na ugomvi usiyoisha kati ya wanandoa hao. Sababu iliyoelezwa kusababisha kutokuelewana huko ni hofu aliyokuwa nayo mume kuwa huenda mkewe siyo muaminifu kwake.

Kutokana na ugomvi huo, mtuhumiwa alifukuzwa hapo nyumbani kwao na mumewe.

Kama wiki moja hivi kabla ya kutekeleza mauaaji hayo, Mtuhumiwa na mumewe walihudhuria sherehe fulani. Wakiwa hapo kwenye hiyo sherehe ndipo mumewe alipomuona mwanaume mmoja ambaye alimtuhumu kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe na ndipo ule uhasama wao ukaibuka upya na kukazuka ugomvi mkubwa kati yao, yaani mtuhumiwa na mumewe, na ndio ukapelekea mtuhumiwa kutekeleza mauaji hayo siku ya tarehe 21, Februari 1978.

Ilielezwa pale mahakamni kwamba, kabla ya kutekeleza mauaji hayo, mtuhumiwa aliandika barua nne na zote zilikuwa na tarehe hiyo ya 21 Februari 1978, na barua hizo ziligunduliwa na Polisi na zilifikishwa pale mahakamani kama kidhibiti. Barua tatu zilikuwa zimendikwa kichwa cha habari kisemacho, "kwa yeyote anayehusika," na moja ilikuwa inamuhusu mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la mama Gaudensia ambaye ni rafiki wa mtuhumiwa.

Barua moja kati ya zile tatu zilizoandikwa kichwa cha habari kisemacho "Kwa yeyote anayehusika" ilisomwa pale mahakamani kama ifuatavyo:

c/o Box 9050
DAR ES SALAAM

21/2/1978

KWA YEYOTE ANAYEHUSIKA

Uamuzi niliouchukuwa ni wa mwisho. George mume wangu naomba asisumbuliwe au kuteswa au kulazimishwa kwa namna yoyote kwa sababu nilikuwa nampenda.

Nimewachukuwa wanangu kwa sababu sitaki wateseke kama nilivyoteseka katika upweke wa kutisha. George mume wangu, hukujua ni kiasi gani nilikupenda nilipokuwa hai. Lakini sasa unaelewa.

KWA AFISA WA POLISI

Tafadhali msimchukulie mume wangu hatua yoyote kwa sababu hana hatia.

Kwa mujibu wa maelezo yake aliyoandikisha Polisi hapo mnamo 3 April 3, 1978, ikiwa ni miezi miwili baada ya tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa alieleza historia ya maisha yake tangu utotoni. Alieleza jinsi alivyoishi maisha ya tabu na mashaka baada ya mama yake kufariki ambapo alililelewa kwa mateso na upweke na mama yake wa kambo.

Mtuhumiwa alielezea maisha yao ya ndoa na mumewe yalivyokuwa na furaha na amani kwa kipindi cha miaka miwili tangu waoane, na jinsi maisha yalivyobadilika na ndoa yake kukumbwa na misukosuko isiyoisha.

Alisema kwamba, matatizo yalianza baada ya yeye kudai kwamba aliwahi kubakwa na kaka wa mmoja wa marafiki zake, na kutokana na kitendo hicho alimuambukiza mumewe maradhi ya zinaa. Hakuthubutu kumweleza mumewe kuhusu tukio hilo la kubakwa kwa muda mrefu alitunza siri hiyo, lakini baadae aliaamua kumweleza mumewe, jambo ambalo lilimletea matatizo makubwa katika ndoa yake mpaka kupelekea tukio hilo la tarehe 21 Februari 1978.

Wakati mumewe anaondoa hapo nyumbani siku hiyo ya tarehe 21 Februari 1978, mtuhumiwa alichanganyikiwa na alianza kukumbuka maisha yake ya utotoni jinsi yalivyokuwa ya mateso na kujikuta akiwa hana pa kwenda. Alimuona mumewe kama mama yake, baba yake, kaka yake na dada yake na maisha yake yote alikuwa akimtegemea mume wake huyo.

Aliamua kwenda kununua sumu na kurudi nayo nyumbani, alijaribu kulala lakini hakupata lepe la usingizi na hakupata suluhu, nini cha kufanya kuhusiana na jambo hilo, na ndipo alipoamua kunywa hiyo sumu.

Kwa maelezo yake mwenyewe alisema:

"Nilikuwa na hasira na wasiwasi kuhusiana na matatizo kati yangu na mume wangu. Nilijiuliza, ina maana matatizo haya yamefikia hatua ya kutisha kiasi cha mume wangu kufikia hatua ya kunifukuza. Nilijiwa na wazo kwamba, acha nijimalize (Kujiuwa) mwenyewe niwaache wanangu wakiwa hai. Lakini baadae nilianza kukumbuka maisha yangu ya utotoni jinsi yalivyokuwa ya mateso na upweke, na nilijiuliza kwamba huenda na wanangu nao wataishi maisha kama yangu kwa kuishi na mama wa kambo. Kwa kuwa mume wangu aliniambia nitakapoondoka nihakikishe siwaachi wanangu nyuma, niliamua kuwachukuwa na kuingia nao chumbani na kufunga mlango. kisha nikawaambia "tunaondoka" wakaniuliza, "tunakwenda wapi?" nikawajibu, "tunasafiri, lakini huko tunakokwenda hatupajui." Kisha nikawabusu na wao wakanibusu, wakapeana mikono kama ishara ya kutakiana safari njema. niliwapa kila mmoja kikombe chenye mchanganyiko wa ile sumu na Orange Squash na mimi nikachukua mchanganyiko huo uliokuwa kwenye glasi na kunywa. Baada ya kunywa mchanganyiko huo wote tulianza kutapika, kutokana na kutapika huko, aliamua kunywa Iodine. Pia nilikunywa vipande vya chupa zilizosagwa na kujifungia katika chumba kingine. Kutoka muda huo, nilipoteza fahamu na sikuweza kutambua kilichotokea baada ya hapo"

Wakati alipokamatwa mtuhumiwa alikuwa chini ya uangalizi wa daktari aliyejulikana kwa jina la Dk. Haule, huyu ni mtaalamu wa magonjwa ya akili aliyekuwa akifanya kazi katika Hospitali ya Muhimbili.

Aliwasilisha ripoti yake pale mahakamani na pia alitoa ushahidi wake pale mahakamani. Kwa kifupi katika maoni yake Dk. Haule alisema kwamba, wakati akitekeleza tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya, alikuwa anajua kwamba anawauwa watoto wake kwa kuwalisha sumu, lakini hakujua kwamba kufanya kitendo hicho ni kosa.

Kwa mujibu wa vifungu vya 12 na 13 vya sheria ya kanuni ya adhabu ambavyo vinahusika na swala hili la uwendawazimu vinaeleza kama ifuatavyo:

Kifungu cha 12. Sheria inamchukulia mtu yeyote kuwa ni mwenye akili timamu kwa wakati wowote mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo.

Kifungu cha 13. Mtu yeyote hawezi kuchukuliwa kuwa ametenda kosa kama kutenda kwake au kutokutenda kwake na katika muda wa kutenda au kutokutenda alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa na akili na hivyo kumfanya kutokutambua alichokuwa anakifanya.

Dk. Haule katika ushahidi wake kwenye ripoti yake aliainisha vidokezo vifuatavyo,

Kwa mara ya kwanza alipomuona mtuhumiwa muda mfupi baada ya tukio hilo la mauaji, mtuhumiwa hakuwa katika hali ya kawaida na hakuonekana kujali. "nilikuwa kama vile naongea na mti." Alisema Dk. Haule. Kwa maoni yake Dk. Haule alisema, inawezekana kwamba mtuhumiwa alikuwa katika hali ya isiyo ya kawaida kwa majuma mawili au zaidi kabla ya tukio hilo, na kwamba, mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya wakati alipokuwa akiwanywesha sumu wanae, lakini hakujua kwamba kitendo hicho ni kosa.

Alielezea juu ya kipindi kigumu cha maisha ya ndoa ya mtuhumiwa alichopitia, jinsi maisha yake ya ndoa yalivyokumbwa na misukosuko ya kutoelewana na mumewe. Nafasi aliyokuwa nayo, maisha aliyopitia utotoni na jinsi alivyokuwa akimtegemea na kumtii mumewe. Dk. Haule, alikuwa na maoni kwamba, kitendo cha mtuhumiwa kuamua kujiuwa na kuwaua wanae, aliamini kwamba, alikuwa amemriwa na mumewe afanye hivyo. Alisema kwamba, alisoma barua zilizokuwa zimeandikwa na mtuhumiwa kabla ya kutekeleza mauaji hayo lakini barua hizo hazikuweza kubadili maoni yake juu ya jambo hilo.

Wakati fulani Dk Haule alidai kwamba mtuhumiwa hakuwa na tatizo la kurukwa na akili lakini baadae alisema kwamba mtuhumiwa alikuwa na tatizo hilo.

Kwaq mamneno yake mwenyewe Dk. Haule alisema. "Alikuwa amerukwa na akili, na aliona kitendo alichokifanya kilikuwa kinakubalika."

Dk. Haule alisema kwamba, mwaka mmoja baada ya tukio hilo hali ya mtuhumiwa iliimarika, kiasi cha kujua kwamba, kitendo alichokifanya kilikuwa ni kosa, lakini bado alikuwa kwenye matibabu.

Katika kesi hii mwanasheria aliyekuwa akimtetea mtuhumiwa alikuwa ameegemea kwenye utetezi wa uwendawazimu.

Akitoa utetezi wake wakili Jadeda alisema kwamba, wakati mtuhumiwa akitekeleza mauaji hayo, hakuwa akijua kwamba kitendo anachokifanya ni kosa. Wakili huyo alirejea maoni ya Dk. Haule.

Wakili huyo alisema kwamba, mtu yeyote aliyerukwa na akili anaweza kupanga hatua kwa hatua kutekeleza mauaji kama aliavyofanya mtuhumiwa na asijue kama kitendo alichokifanya ni kosa.
Wakili Jadeda alikuwa akipinga maoni ya upande wa mashitaka kwamba, mtuhumiwa alikuwa kijua kitendo anachokifanya ni kosa.

Akisoma hukumu Mheshimiwa Jaji Makame alikubaliana na swala la mtuhumiwa kuwa na dhamira ovu (Malice aforethought), hasa kwa kuangalia vitendo vya mtuhumiwa tangu maandalizi, dhamira na akiwa na utambuzi kwamba, akiwanywesha wanae sumu itawasababishia kifo, na hiyo inadhihirisha kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua ni nini anachokifanya, na si lazima ajue kwamba kufanya hivyo ni kosa.

Hata hivyo Mheshimiwa Jaji Makame alikuwa ameshawishika kuamini hivyo kutokana na barua nne alizoziandika mtuhumiwa kabla ya kutekeleza mauaji hayo, ambazo aliziandika sambamba na tendo alilofanya tarehe 21 Februari 1978. Barua hizo kwa uwazi zilionyesha kabisa kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua anachokifanya ni kosa.

Kwa maneno yake Mwenyewe Mheshimiwa Jaji Makame alisema, "Katika barua ambayo ilisomwa hapa mahakamani wakati wa shauri hili, mtuhumiwa alisema wazi kwamba mumewe asije akaadhibiwa au kuteswa kwa kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa. Pia kulikuwa na ombi la mtuhumiwa kwa Polisi kwamba, wasije wakamchukulia hatua mumewe kwa sababu hana hatia."

Muheshimiwa Jaji Makame aliendelea kusema kwamba, wazo la kutokuwa na hatia na kutompa mumewe adhabu katika barua alizoandika mtuhumiwa, linadhihirisha wazi kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua kwamba kitendo anachokifanya ni kosa na alitaka kuweka wazi kuwa mumewe hahusiki kwa namna yoyote na kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa. Alijua kama mumewe akihusishwa na kitendo alichokifanya yeye mtuhumiwa, ataadhibiwa kwa kosa hilo.

Mheshimiwa Jaji Makame aliendelea kusema,

"Ni kweli Dk. Haule alisema kwamba, ukiachana na barua hizo alizoziandika mtuhumiwa, lakini yeye alikuwa na maoni kwamba, mtuhumiwa hakuwa anajua anachokifanya kuwa ni kosa. Alisema, barua zilimuonesha kwamba, mtuhumiwa alikuwa akimtegemea mumewe kwa kiasi kikubwa na hasa katika mahusiano yao. Kama tunamuelewa Dk. Hauli vizuri, alikuwa huenda anamaanisha kwamba, hizo barua zilikuwa na uhusiano na imani aliyokuwa nayo mtuhumiwa kwamba, alikuwa ameshurutishwa kujiuwa na kuwauwa watoto wake na mumewe. Kwa bahati mbaya barua haijaeleza kuwa mtuhumiwa alikuwa na imani ile. Ilikuwa ni ahuweni aliyoiweka Dk Hauli. Japokuwa barua ilieleza kuwa mtuhumiwa alikuwa anamtegemea sana mumewe, lakini bado zilikuwa zinathibitisha kwamba mtuhumiwa alikuwa anajua kitendo anachokifanya ni kosa.
Pia nashindwa kuunganisha maelezo ya barua hizo na maoni ya kurukwa na akili yaliyotolewa na Dk. Haule, aliposema kwamba, mtuhumiwa aliamini kuwa ameamriwa na mumewe ajiuwe na kuwauwa watoto wake."

Mheshimiwa Jaji aliendelea kusema,

"Kwangu mimi, namuona Dr. Hauli kama mtaalamu mwenye uzoefu na ujuzi mkubwa wa magonjwa ya akili, pamoja na mambo mengine, pia ni mwanachama Royal College of Psychiatrists na anayo Diploma ya Psychiatric Medicine aliyoipata nchini Uingereza. Naheshimu sana maoni yake kulingana na utaalamu wake na ninashindwa kupinga ushahidi wake. Pia ninakubaliana na ukweli kwamba hata kama mtuhumiwa ataonyesha kurukwa lakini hiyo itakubalika iwapo kutakuwa na kipimo chenye uwelekeo (Balance of Probability).

Mtuhumiwa lazima aoneshe ushahidi wote; kwamba kutokuwa na akili timamu ni zaidi ya kuwa timamu. Ingawa inawezekana ikawa chini ya tunachodhamiria. Katika kuliweka sawa hili mamlaka ya kuthibitisha inafananishwa na kesi ya Nyinge Siwato Vs Jamhuri 1959 East Africa 974 ikifuatiwa mara nyingi sana ikihusishwa na MbekuleV-R. 1971, East Africa 479. Jaji Enzi zake alielezea katika kesi ya Siwato "Mahakama haifungwi kukubaliana na ushahidi wa hospitalini (Medical Testimony) kama/endapo kuna sababu madhubuti ya kutofanya hivyo. mwisho wa siku ni kazi ya mahakama kutafuta ushahidi na viambatanisho katika kufanya hivyo, ni wajibu wangu kuangalia na kulipima na ushahidi uliotolewa kabla na ikiwemo utaalam wa Daktari."

Mheshimiwa Jaji Makame akihitimisha hukumu hiyo alisema:

"Inawezekana hasa kwamba sheria yetu katika swala la kurukwa na akili imepitwa na wakati na ni ya zamani sana, Dk. Haule katika ushahidi alieleza kuwa katika utaalamu wa sasa, utofauti kati ya kurukwa na akili na kutojitambua katika utenedaji vinapingana. Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa hekima linaweza kulifanyia marekebisho hili sambamba na sheria ndogo ndogo na kulileta katika utandawazi wa kitabibu. Mipaka ya kimahakama, ikiwemo ya Afrika Mashariki wamefanya hivyo."

Mtuhumiwa katika kesi hii alihukumiwa kunyongwa.

Mama Taji alikuja kupewa msamaha na Raisi Nyerere miaka 7 baadae.

Amefariki tarehe 7 January mwaka huu.
Mkuu hii simulizi kama inafanana na simulizi ya Taji Liundi
 
HII NDIYO LIBYA ALIYOIJENGA MUAMMAR GADDAFI.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo Gaddafi aliyasimamia na kuyatekeleza katika utawala wake wa miaka 42 kwa Libya.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na tovuti za mawasiliano za Libya na Zimbabwe zimeeleza kuwa nchini Libya hakuna mwananchi aliyewahi kulipa bili ya umeme, umeme ulikuwa bure kwa raia wake wote.

Hakukuwa na riba katika mikopo, benki zote Libya zilikuwa chini ya Serikali, mikopo ilitolewa kwa wananchi bila riba ya kiasi chochote .

Taarifa hizo zikafafanua kuwa makazi ni haki ya msingi nchini Libya, Gaddafi aliwahi kusisitiza kwamba wazazi wake hawawezi kupata makazi hadi kila raia apate makazi. Baba wa Gaddafi alifariki dunia wakati yeye, mama yake wakiwa wanaishi katika hema.

Wanandoa wote wapya nchini humo walipata Dola 50,000 kwa Serikali kwa ajili ya kununua makazi yao kuwasaidia kuanzisha familia mpya.Elimu na huduma za kiafya vilitolewa bure. Wakati Gaddafi nachukua nchi asilimia ya waliokuwa na elimu ilikuwa 25, kwa sasa inafikia 83.

Kwa waliotaka kuwa wakulima, walipewa ardhi bure, nyumba katika shamba lao, vifaa, mbegu na mifugo kwa ajili ya kuanzisha miradi.Iwapo kuna waliokuwa hawawezi kupata huduma za elimu na afya wanazostahili, Serikali iliwalipia kwa ajili ya kuzipata nje ya nchi, hizi hazikuwa bure, walitakiwa kuchangia, walipata Dola2,300 kwa mwezi kwa ajili ya makazi na usafiri.

Kwa waliokuwa wakitaka kununua magari, Serikali ililipia kwa asilimia 50 ya bei. Bei ya petroli ilikuwa karibu na bure, lita ililipiwa kwa Dola 0.4.

Libya haidaiwi nje, pia ina akiba inayofikia Dola150 bilioni nje ambayo kwa sasa imezuiliwa.Kwa waliomaliza vyuo, Serikali iliwapatia posho sawa na mshahara wa maofisa hadi watakapopata ajira yenye uhakika. Sehemu ya mauzo ya mafuta ya Libya iliwekwa moja kwa moja kwenye akaunti ya raia wake.

Kila mwanamke aliyejifungua alipata posho ya Dola5000, mikate 40 iliuzwa kwa dola0.15, asilimia 25 wa Walibya, wana shahada ya chuo kikuu.Kama hiyo haitoshi taarifa hizo zimeeleza kuwa alisimamia mradi mkubwa kabisa wa umwagiliaji, uliopewa jina la Great Man-made River, kuhakikisha maji yanakuwepo kwenye maeneo yote ya nchi yenye jangwa.

Wakati wa vikwazo kwa Serikali yake miaka ya 1980, Libya ilikuwa miongoni mwa nchi tajiri kabisa kwa msingi wa pato la ndani, ikwa na kiwango cha juu cha maisha kuliko Japan. Ilikuwa ni nchi tajiri kuliko zote kabla ya vuguvugu la mapinduzi.

Wastani wa kiwango cha maisha kwa pato la kichwa ni Dola11,314 . Gaddafi amewahi kutumia fedha nyingi kwa ajili ya safari zake na miradi yake, lakini amefanya mabo makubwa ambayo hakuna dikteta aliyewahi kuyafanya kwa watu wake. Alirejesha pato kwa watu wake, aliwajali.
Mkuu sasa hivi maisha yao yakoje?
 
HIVI NDIVYO FIDEL CASTRO ALIVYOPONYOKA KATIKA MAJARIBIO HAYA YOTE YA KUULIWA.

Baada ya fidel kutwaa madaraka kwa kumpindua Batista ndani ya siku 100 za mwanzo alifanya mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na kutwaa baadhi ya mashamba ya miwa, kusogeza huduma za jamii karibu, kupiga marufuku ubaguzi wa rangi nk..

Nchi ya Cuba ilikuwa na idadi kikubwa ya watu ambao hawajasoma zaidi ya asilimia 60 ya watu wale walikuwa hawajui kusoma na kuandika, chini ya Castro akaanzisha utaratibu wa wale wachache wanaojua kusoma na kuandika wawafundishe wale wasiojua, wakasambaa kote nchini chini ya msemo maarufu wa 'kama hujui jifunze ujue na kama unajua fundisha'.

Kupitia mpango huo watu wengi wa Cuba wengi walijua kusoma na kuandika na elimu ilitolewa bure.

Pia nchi hiyo wakati wa Fidel anaingia madarakani ilkuwa na jumla ya madaktari 6000 tu na wengi walikuwa hapoHavana, kule vijijini huduma zilikuwa hakuna na watoto wengi walikufa kwa kukosa huduma. Castro akawaambia madaktari wale waliorundikana mjini wasambae mpaka vijijini wakatoe huduma. Wengi waligoma na kukimbia nchi, ndio chanzo cha wengi kwenda miami na pia watu wengi waliokuwa na uchumi mzuri ambao mali zao zilitaifishwa walimchukia Fidel na kuikimbia nchi, ndio hao walokuwa wakishangilia juzi.

Ili kuleta huduma za afya karibu Fidel alianzisha vyuo vitatu maalum kwa ajili ya kupambana na uhaba wa madaktari na alifanikiwa sana, vifo hasa vya watoto vilipungua sana kuliko baadhi ya miji huko USA wakati huo.

Maadui wa Castro waliongezeka toka nje na ndani ya nchi, CIA walitumia mbinu chafu za kumuondoa Fidel duniani na mipango mingi iliwahusisha wacuba wengi waliokimbia nchi hasa waliokuwa wakiishi Miami.

Sasa Fidel alipambana na mbinu hizo kwanza kitengo cha ujasusi kilikuwa chini yake, kiliitwa DGI(Director General of Intelligence) na kitengo hiki kilikuwa kama mali binafsi ya Fidel, wengi wa waliofundishwa walikuwa nI vijana wadogo hasa walioungana nae huko kwenye milima ya Ciera Maestra wakati wakipambana na Batista na vijana hawa walikusanywa na mama mmoja aliyekuwa karibu sana na Fidel, aliitwa Celia Sanches, huyu alikufa kwa Saratani mwaka 1980.

Vijana hawa asilimia 95 walifanya kazi ya kijasusi bure bila malipo na wakati mwingine walichukuliwa vijana wadogo sana na kupelekwa ""shambani""ambako walipewa elimu ya ujasusi wa hali ya juu sana, na pia walikuwa wazalendo sana kwa nchi yao na watiifu kwa Fidel.

Hakuna CIA officer aliyeingia Cuba bila kufahamika, mipango ya mauaji iliyopangwa na Fidel iligundulika haraka kwani Fidel alifanikiwa kupenyeza vijana wengi kwenda USA hasa Miami na Florida na huko waliishi wakifuatilia kila Wamarekani wanachokipanga juu ya Fidel na wengi wa vijana hawa bila CIA kufahamu kwamba ni majasusi waliwatrain tena ili kufanikisha mipango yao ya kumuua Fidel Castro, vijana hawa walibaki watiifu kwa Fidel na hivyo mipango yote waliyopanga ilimfikia el comandante Fidel Castro bila wasiwasi.

Baada ya John F. Kennedy kuwa Rais wa Marekani alimkabidhi ndugu yake aliyeitwa Robert Kennedy jukumu la kumuua Fidel Castro kwa kupitia Counter Intelligence na Double Agent.

Vijana wa Fidel waligundua njama hizo na zikafika mezani kwa el comandante Fidel Aljandro Castro luz.

Akihojiwa na mwandishi wa Reuters, Fidel alitahadharisha Marekani kwa kusema jaribio lolote la kumuua kiongozi wa Cuba litakuwa na madhara kwa Marekani na wasitishe mipango yao, Wamarekani walisikia lakini walikaidi na Robert Kennendy akaendelea na mipango ya kumuua Castro.

November 22 Lee Oswald alimpiga risasi Rais wa Marekani John F. Kennedy na baada ya saa moja ikatangazwa raisi ameuawa, inaaminika Castro alifahamu mipango hiyo japo alikanusha sana.

Baada Kennedy kuingia madarakani CIA walimwambia ni lazima Fidel aondolewe madarakani hii ni baada ya Fidel kutaifisha mali nyingi zilizokuwa zikimiliwa na Wamarekani na pia alianza kuagiza bidhaa toka Soviet.

Baada ya pressure kubwa toka kwa CIA, Rais kenedy akaidhinisha kuondolewa madarakani kwa Fidel Castro na katika mpango huo Kennedy alisema hataki ijulikane kuwa Marekani ndio imehusika na mpango huo kwa hiyo akawataka CIA wahakikishe wanakamilisha mpango huo bila kuacha alama ya mhusika mkuu.

CIA wakaanza mpango huo kwa kuwahusisha wacuba waliokimbia nchi hasa wale waliokuwa Miami, jumla yao ilikuwa 1400 na kikosi cha watu hao kikapewa jina la kikosi 2506, wakapelekwa eneo maalumu na kuanza kupewa mafunzo ya kwenda kumwondoa madarakani El commandante Fidel Castro.

Mazoezi ya anga, majini na ardhini yalifanyika katika kundi hilo la wakimbizi waliokuwa wakipewa mafunzo walikuwepo maagent wa Fidel waliokuwa wakipenyeza taarifa zao havana.

Mazoezi yalipokamilika zilipangwa hatua tatu za mashambulizi ambazo Rais Kennedy alizipitisha, njia ya kwanza ilikuwa ni kutumia ndege za kivita kuzipiga air base zote za Jeshi la Anga la Fidel, walitaka kushambulia na kuzimaliza ndege zote.

Njia ya pili ilikuwa ni kwenda kumalizia mabaki yoyote ya ndege ambayo haikulipuka kwenye mpango wa kwanza na njia ya tatu ilikuwa ni kuingia kwa hao wakimbizi wa Cuba waliopewa mafunzo kwenda kushambulia na kumwondoa Fidel madarakani.

Njia ya kwanza ikaanza kutumika, marubani wavamizi walipewa ndege, ndege zile za kivita zilibadilishwa rangi na kufanana sana na zile za Jeshi la Cuba na pia zilipakwa matope ili zikiwa angani zionekane ni chakavu, jamaa wakaenda wakashambulia kambi ya anga ya Fidel na waliangamiza asilimia 80 ya ndege za Castro, Jeshi la Anga la Castro lilibakiwa na ndege sita tu na marubani saba, ilikuwa big loss kwa comrade.

Baada ya njia ya kwanza kuleta matokea chanya kwa Wamarekani, huko New York kiongozi wa Cuba Umoja wa Mataifa akaitisha kikao, akaituhumu Marekani, Marekan ikakataa katakata kuhusika, wakadai ndege zilizoshambulia ni za Wacuba wenyewe walioasi Jeshi.

Balozi wa Cuba akasema ndege za Jeshi la Cuba sio zilizoshambulia, ndege zilizoshambulia zina mngurumo tofauti na ndege za Cuba, ndege zilizoshbulia ni za Marekani ila mmezibadilisha rangi zifanane na za Cuba ila mmeshindwa kubadili muungurumo.

Hapo rais Kennedy akaingiwa na ubaridi na akasitisha njia ya pili iliyokuwa imepangwa, Maafisa wa CIA walichukia sana kuona rais amekataa njia ya pili kutumika.

CIA wakaenda njia ya tatu ya kuwa deploy wale 1400 ili wavamie Cuba, kule Cuba Fidel mwenyewe aliingia front na kusema hii ni kazi ya Marekani na Cuba will respond in kind.

Baada ya kauli hiyo Fidel alizihamisha zile ndege sita zilizosalia na pia akaandaa mpango mkakati wa kujibu.

Wale wavamizi 1400 wa mara ya kwanza ilikuwa imepangwa waingie Cuba kupitia Trinidad lakini baada ya Kennedy kuigomea njia ya pili, Maafisa wa CIA nao wakabadili njia ya kuingia Cuba kwa hawa wavamizi, wakaelekezwa waingie cuba kupitia hapo the bay of pigs. Mahali hapo Fidel alipafahamu sana sana, lakini katika kujiandaa na adui mwonekano wa pwani ile ilibadilishwa kwa kiasi kikubwa, kiasi kwamba maadui walipokuwa wakija walishindwa kuona vizuri hasa ni wapi Majeshi ya Cuba yamejificha.

Meli zikiwa zimewabeba wavamizi zikafika Pwani ila Jeshi la Cuba likawa na taarifa. El Commandante Fidel akiwa mstari wa mbele kuendesha mapambano, wale wavamizi walishambuliwa sana na meli moja iliyobeba vifaa maalumu ilizamishwa na nyingine iliyowabeba hao wavamizi.

Walipigwa sana, zile ndege sita zilizosalia zikawa zinazunguka anga ya Cuba hasa hapo bay of pigs, wengi wa wavamizi waliuawa na wengine kuchukuliwa mateka. Taarifa zikafika Marekani juu ya hasara kubwa na kushindwa kwa zoezi hilo.

Rais Kennedy akatoa ndege sita za kijeshi kwenda kusaidia, hazikufua dafu kwani ndege nne zilidunguliwa na Jeshi la Cuba, ilikuwa loss kubwa kwa Marekani.

Mpango wa kumtoa madarakan Fidel ukafeli vibaya sana, hivyo ndivyo ilivyokuwa juu ya bay of pigs.
 
HIVI NDIVYO MAJASUSI YA KIRUSI YALIVYOKUWA YAKIDUKUA MAZUNGUMZO YA UBALOZI WA MAREKANI KWA UFUNDI WA HALI YA JUU.


Mnamo mwaka 1946, kundi dogo la wanafunzi watoto wa shule wa nchini Urusi kutoka katika kikundi kidogo kilichojulikana kama "Vladimir Lenin All-Union Pioneer Organization (wapo kama vijana flani hivi wa skauti wa hapa Bongo) walimpatia zawadi ya nembo ya taifa la marekani (kama huku kwetu Tanzania ni ile nembo yetu ya bibi na bwana) ndugu Avarell Harriman, aliyepata kuwa balozi wa Marekani nchini Urusi (USSR)

Ile zawadi, kama ishara ya urafiki mwema wa urusi kwa marekani ambaye alikuwa ni mshirika wake mkuu katika vita ya pili ya dunia, ilikuja kuning'inizwa katika eneo maalum la makazi ya balozi huyo yaliyokuwapo katika jiji kuu la Moscow.

Nembo ile ya taifa la marekani iliendelea kuning'inia pale ukutani kwa kwenye makazi ya balozi kwa muda wa miaka saba (7), mpaka kwa bahati mbaya wataalam kutoka wizara ya mambo ya nje (bila shaka ni maofisa wa CIA) walipokuja kugundua kumbe ile zawadi ilikuwa ni zaidi ya urembo wa ukutani.

Mara paaaaaap, kumbe ilikuwa ni kifaa cha kunasia mazungumzo (bugging device)........!!!!!.


Warusi waliunda kifaa cha kusikilizia mazungumzo kwa siri sana (bug), ambacho makachero wa kupambana na wapelelezi wa nchi hasimu (counterintelligence unit) wa Marekani walikitunga jina na kukiita (The Thing).

Kifaa kile kilifichwa kwa usiri sana ndani ya nembo ya taifa la Marekani na kimekuwa kikisikiliza mazungumzo ya balozi Harriman pamoja na mabalozi wote waliomfuata kwa kipindi chote ambacho kifaa kile kilikuwa kinaning'inia mule ndani.

Balozi yule alikiri kwa kusema ya kuwa Ilidhihirisha siku ile kumbe USSR ilikuwa na wataalam wa kutisha sana wa masuala ya electronics.

Balozi alisema ya kuwa sasa ninaamini ya kwamba kwa ugunduzi huu utaalam mzima wa serikali kusikilizana siri umefikia viwango vya hali ya juu sana vya technology.

Wanadiplomasia pamoja na wamarekani wengine waliokuwa wakifanya kazi katika ubalozi wao pale USSR walikwisha amini zamani hata kabla ya kuwa kuta zote zilizopo jiji la Moscow "zina masikio"

Aliyewahi kuwa rais wa marekani kwa miaka ya zamani sana bwana James Buchanan aliwahi kisema ya kwamba mara zote wanadiplomasia wetu huzungukwa na mashushushu wenye taaluma zote kubwa na ndogo, na ni mara chache sana tunaweza kukodisha ama kuajiri mtumishi wa ndani ambaye sio informer wa polisi.

Mwanzoni mwa karne ya 20, ujasusi kwa njia za kibinadamu pamoja na usikilizaji wa mazungumzo ulijawa na technology mpya ya nyaja pamoja na vifaa vidogo vya kusikilizia na kurekodia mazungumzo.

Wageni wote waliokuwa wakiingia katika nyumba ya makazi ya balozi walikuwa wakipewa kadi punde tu wanapowasili wakitahadharishwa ya kuwa nyumba vyote pamoja na bustani ndani ya eneo lile vilikuwa vinapelelezwa kwa ukaribu sana na makachero wa KGB.


Hiki kifaa kiliundwa na bwana Termen, ambaye alipata kuishi nchini Marekani kwa kipindi kirefu kidogo kisha akaja kurudi Urusi kabla ya vita ya pili ya dunia.

Baada ya kuwasili Russia, bwana theremin alipelekwa moja kwa moja katika chuo cha siri chenye maabara kisha kupewa jukumu la kuunda na kuja na njia ya kitaalam ya namna na kusikilizia mazungumzo ya nyumbani kwa balozi wa Marekani nchini Russia.

Kifaa alichofanikiwa kuunda mtaalamu huyo kilikuwa na antenna pamoja na cylinder pamoja na waya mdogo sana uliotumika kama microphone. Majasusi wa KGB waliokuwa wanazurura maeneo ya mtaa huo ambapo kuna makazi ya balozi wa marekani, walikuwa na uwezo wa kuwasha hicho kifaa kwa remote maalum inayotumia mawimbi ya radio.

Sasa pale ambapo balozi ama mtu mwingine yeyote aliyepo chumbani akiongea, yale mawimbi ya sauti yalikuwa nayawaendea moja kwa moja vijana wa KGB na kuweza kusikiliza mazungumzo mazima.

Maajabu ya hicho kifaa ni katika udogo wake. Kilikuwa ni kidogo mno. Tena saaaanaa aiseee. Kilikuwa hakitumii chanzo chochote cha umeme wali betri, hakukuwa na nyaya ambazo zingeweza kugundulika wala betri za kubadilisha na kiliweza kifanya kazi pindi tu KGB wakikiwasha kwa remote inayotumia mawimbi ya redio. Laa sivyo kinazimika kiasi kwamba wakaguzi wa CIA wasingeweza kukigundua.

Wizara ya mambo ya nje ya marekani kupitia wataalam wake wa kufagia vifaa vya kunasia sauti (bug sweepers) walipatwa na mashaka kwamba KGB waliunda kifaa cha namna hii pale ambapo wataalam wa mawimbi ya radio kutoka jeshi la marekani pamoja na uingereza waliokuwa wanachungua mawasiliano ya USSR bila kutarajia wakajikuta wanakamata mawasiliano ya sauti ya wanadiplomasia wao kwa kutumia vifaa vyao wenyewe.

Matukio ya namna hiyo pamoja na kitendo cha marekani kuruhusu wafanyakazi wa urusi kufanyia marekebisho nyumba ya balozi wao kabla ya kuhamia mwaka 1952, ambapo ndio ili nafasi nzuri kwa KGB kupandikiza vifaa vya kusikilizia, ilipelekea CIA kutuma wataalam wake kupitia wizara ya mambo ya nje kwenda kufagia nyumba nzima (bug sweeping) bila mafanikio.

Walitoka kapa mpaka wakaanza kushuku labda KGB wamebadili mbinu zao za kupandiliza vifaa ama taaluma ya CIA ya kugundua vifaa hivyo ndio imepitwa na wakati.....!!!!!

Baada ya kuona hali si hali, wizara ikaamua kutuma tena wataalam wawili, Ford pamoja na Bezjian, mpaka Moscow kufanya zoezi upya tena kwa kina na umakini zaidi. Bezjian akahisi labda KGB waliondoa kifaa chao kabla zoezi jipya la ukaguzi halijaanza na kisha kupachika tena hali ilipokuwa shwari.

Ili kuwakamata vizuri KGB, akaamua kujifanya kama tu ni mgeni wa balozi Kennan. Vifaa vyake vya kazi vilikuwa vipo tayari na vimefichwa vizuri kabisa hata kabla hajafika na kisha kukaa pale kwa balozi kwa siku kadhaa huku akicheza karata na kuwaangalia kwa umakini wafanyakazi wa nyumba ya balozi wakati huo anatumia muda wa usiku kutafuta kifaa hicho cha kunasia sauti. Lakini safari hii wakachemka tena. Hola. Wakatoka patupu.

Sasa jioni moja wakati balozi yupo kwenye chumba chake hicho akiwa anasoma kwa sauti ya chini kidogo baadhi ya nyaraka zake za siri wakati wataalam wa CIA bwana Ford na Bezjian wakiwa wanazunguka nje ya nyumba wakiwa na vifaa vyao vya detection, ghafla Bezjian akafanikiwa kukamata sauti ya bwana Kennan kwenye receiver yake na kisha taratiiibu kabisa akaamua kuifuatilia ile signal mpaka chanzo chake inapotokea.

Bezjian akaenda katika chumba cha kusomea na kumwambia Kennan kwa ishara kwa aendelee kusoma kwa sauti zaidi kwa maana kuna signal ameikamata. Ile signal iliyokuwa na sauti ya Kennan ilionekana inatokea katika kuta nyuma ya ile "zawadi aliyopewa balozi.

Bezjian akaondoa ile zawadi kutoka ukutani kisha kwa kutumia nyundo akaanza kupasua ukuta ambapo ile zawadi ilikuwa imetundikwa. Wakati anabomoa ukuta signal ikapotea ghafla.

Bezjian ndipo machale yakamcheza kuwa kile kifaa cha sauti hakikuwa katika ukuta, bali kilikuwa ndani ya ile zawadi ya balozi na kisha kuamua kuvunja ile zawadi kwa kutumia nyundo ile ile.

Ndani ya dakika chache zoezi likakamilika na yule mtaalam wa CIA akakuta ndani ya ile zawadi kulikuwa na kifaa kidogo sana kinachoweza kulingana na penseli.

Kwa usiku wote ule, ofisa wa CIA bwana Bezjian akaamua kulala na kifaa kile chini ya mto wake ili kwamba KGB wasije kukiiba. Kesho yake kifaa kikapelekwa kwenda marekani chaaaaap ili kisomwe na kitengenezwa mbadala wake na idara za usalama za marekani jambo ambalo likawa kama vile ndio chanzo cha mashindano ya silaha baina ya USSR na USA katika kuunda vifaa vya kunasa mawasiliano vya hali ya juu zaidi ili kila mmoja amchunguze mwenzake zaidi.

Kwa miaka mingi sana hii zawadi ya mtego ilining'inizwa juu ya kuta za nyumba ya balozi wa marekani iliyokuwa busy sana na wageni wa aina tofauti tofauti mpaka wale wa levels za juu sana kama General wa jeshi Eisenhower, watumishi wa ikulu ya marekani pamoja na wabunge wengi sana, wakibadilishana taarifa mbali mbali kuhusiana na hali ya usalama na ustawi wa nchi yao.

Mmoja wa watumishi wa KGB ambaye alikuwa anasimamia kifaa kile akaja kukiri baadaye ya kuwa kile kifaa kiliwawezesha kupata taarifa muhimu zilizowezesha USSR kuweza kuwazidi kete wamarekani katika siasa za dunia wakati wa kipindi kigumu cha vita baridi.
 
*MJUE MWANAHARAKATI BIBI TITI MAANA HALISI YA MWANAMKE WA SHOKA.*



Sasa basi, katika sehemu hii ya simulizi za Bibi Titi, tutaangalia ni nini kilimsibu mpaka akakosana vibaya sana na wenziwe katika chama cha TANU na kupoteza ubunge na uwaziri, kufukuzwa kama mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU, na kupigwa marufuku kwa asasi ya Kiislamu ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) ambayo yeye alikuwa kiongozi wake mwandamizi hapa Tanzania.

Anasimulia Alhaji Abdallah Tambaza:

Nikiwa kijana mdogo sana jijini kwetu hapo siku hizo za kudai Uhuru, kwenye miaka ya mwisho ya 50s, nilikuwa nikimwona bibi yule pale ofisi za TANU Makao Makuu, akiwa na viongozi wenzake wakiwa wamesimama nje ya ‘kajumba kao kadogo ka TANU ka vyumba sita tu, kalikojengwa kwa miti na kukandikwa udongo’. Wakati ule nilikuwa mwanafunzi pale Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, mkabala na ofisi hiyo.

Lakini pia, nilikuwa nikimwona mitaani kwetu; mtaa wa Sikukuu na Udowe ambako alikuwa akija kumtembelea binti yake peke, Halima, aliyekuwa ameolewa hapo na kijana mcheza soka maarufu wakati huo Mzee Iddi Hamisi. Mzee Iddi, alikuwa mpachika mabao wa klabu ya Cosmopolitan ya Dar es Salaam, wakati ule klabu hiyo ilipokuwa inawika na kuwa na hadhi kama vile Simba au Yanga kwa sasa. Kwa kweli ilikuwa ndio klabu ya kwanza kupata tiketi ya kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya Afrika kwenye miaka ya 60s, lakini ikakwama kutokana na fedha.

Lakini sikumfaidi hasa bibi Titi mpaka pale nilipokuwa nikichukuliwa— mimi na ndugu zangu— tukiwa na babetu au mametu, kwenda kwenye mikutano ile ya uamsho na siasa, ambayo Titi alikuwa mzungumzaji mkubwa akianza; halafu Mheshimiwa (Nyerere) anamaliza.

Kwa zama zile, miongoni mwa Waafrika, mtu aliyepaswa au kustahili kuitwa mheshimiwa, alikuwa ni Nyerere peke yake. Neno hilo ‘mheshimiwa’ hakuitwa Gavana, DC wala PC. Ukisema mheshimiwa, hiyo peke yake ilitosha kuwa wewe ulikuwa unaamanisha kipenzi chao Nyerere kutoka Butiama, aliyewashangaza wengi kwa uwezo wake wa kujieleza na kujenga hoja, ambaye kwa wakati huo, pamoja na sauti yake nyororo na nyembamba, alikuwa akipata taabu sana kutamka neno Watanganyika, ila mpaka kwa kulivuta kidogo:

‘‘Wataaa-nganyika wenzangu, Uhuruu na Umoja; Uhuruu na Kazi; Uhuruu na Maendeleo,” hiyo ni moja ya kaulimbiu kuu za wakati huo.

Ni ukweli uliowazi kwamba watu kama akina Bibi Titi hawakuzuka tu na kuwa viongozi katika Chama cha TANU. Watu wa namna ile; wenye vipaji vya namna ile; majasiri namna ile huwa wametengenezwa. Hufundwa majumbani, hupikwa na wazazi wao wakaiva na kuwa tayari kupambana na lolote lijalo.

Titi mama yetu ni mmoja wao. Alizaliwa mwaka 1926 na mara alipofikia umri wa miaka 13 (kwa maana ya ‘kuvunja ungo’), tayari alipewa mume. Hiyo maana yake ni kwamba alikuwa tayari amefundwa na wazazi wake mapema kuja kuyakabili maisha na changamoto zake zijazo.

Titi, akiwa bado kwenye umri mdogo kabisa aliweza kuaminiwa kuongoza katika uimbaji kwenye shughuli za kimila na harusi kwa kutumia sauti yake nyororo, maneno yenye bashasha na vipaji vingi vingine ambavyo alivionyesha tokea mapema.

Shneidder Plantan, ndiye aliyemwingiza Titi na mumewe katika siasa, baada ya kuwa amependekezwa na wanawake wenziwe waliomjua uwezo wake kutoka katika vikundi mbalimbali vya harakati za kinamama na mambo kama hayo. Kadi ya mumewe ni namba 15 na ya kwake ilikuwa 16.

Mwaka 1957, pale kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, mbele ya mgeni kutoka chama cha Labour cha Uingereza, alipewa nafasi kuhutubia mkutano wa TANU wakati Nyerere akiwa Butiama mapumzikoni kwa mamake. Enzi zile kulikuwa na fikra potofu kwamba mwanamke ni mtu wa kukaa nyumbani tu na kulea watoto. Kwamba kazi kama zile za siasa hawaziwezi hata kidogo.

Kwa kujiamini na huku akiwaonyoshea kidole wanaume, aliwaambia wanawake wenzake:

“…Mnawaona hawa! Basi wafanye watakavyofanya hawa, pamoja na hao wengine wote wanaotisha duniani, wametoka katika matumbo ya wanawake na waliishi humo miezi tisa… kila mmoja wao kanyonya ziwa la mamake miaka miwili… sasa tujitokeze wasitushinde hawa!

“… wanawake amkeni, tokeni majumbani tuje tupambane pamoja na wanaume mpaka uhuru upatikane msiogope …msiogope… msiogope

“…kutawaliwa siyo kuzuri ndugu zangu, hili ni letu sote si la wanaume peke yao, njooni kina dada, njooni kina mama na vikongwe pia!” aliunguruma Titi huku kelele za nderemo, hoihoi na vigelegele vikihanikiza uwanjani pale.

Kwa mara ya kwanza nyimbo zile mashuhuri za kwenye harusi na sherehe nyingine alianza kuwaimbisha wanawake wenzake na kuwatia hamasa isiyo na kifani:

“Hongera mwanangu wee hongera, nami nihongere wee hongera! x 2

Mama usungu mama usungu! x 2 Oieh!

Oieh! Linauma mno wee oieh!

Linauma mno eh! Oieh linauma mno!’’

Kutoka hapo siku hiyo, Bibi Titi ikawa ndio habari ya mjini na sifa zake zikazagaa kila pembe ya ukanda huu wa Afrika Mashariki. Wanawake makundi kwa makundi wakawa wamejitokeza na kukikubali chama na harakati zake. Majumbani, kwenye misiba, harusini kote ikawa ndio mazungumzo … Titi…Titi…Titi!

Wapigania uhuru wa Kenya wa wakati huo, akiwamo Tom Mboya, Jaramogi Oginga Odinga (baba wa Odinga wa sasa), walipopata habari wakaleta maombi Titi aende kwao kuwasaidia kushawishi serikali ya Mngereza kumtoa kifungoni Mzee Jomo Kenyatta (babake Rais Kenyatta wa sasa), kwa kosa la uhaini wa kudai kujitawala.

Titi, alitia fora kwenye mikutano yake kule Mombasa, Kisumu, Machakos na Nairobi. Titi, alisimama majukwani kule Kenya akiwa amevalia ‘mini skirts’ zake maridadi kabisa , akilia kwa uchungu kumpigania Kenyatta awe huru na wanawake waje wajae kwenye harakati.

Haukupita muda mrefu, miaka kadhaa baadaye, Mzee Jomo Kenyatta aliachiwa huru kule Kenya na haraka haraka akaja Tanganyika na kuhutubia maelfu ya watu, akiwemo mwandishi huyu, pale kwenye viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.

Kenyatta akiwa amevalia suruali yake ya corduroy rangi ya udongo (maarufu khaki Kenya siku zile) na koti kubwa la kijivujivu, alipeperusha juu usinga wake mweusi na kutumia muda mwingi kumshukuru Bibi Titi kwa kazi aliyowafanyia Wakenya.

Kwenye mkutano ule, ndipo Nyerere alipotamka kwamba yuko tayari kuahirisha uhuru wa Tanganyika, ambao tayari ulikuwa umeshajulikana, ili tusubiri Kenya nao wapate wa kwao na hapo nchi hizi ziungane kuwa moja na Kenyatta awe ndio rais wake. Ni tamko zito sana hilo, ambalo bila shaka yeyote, lilitokana na kazi ya Mama Titi. Uhuru uchelewe na urais apewe mtu mwengine! Leo isingewezekana. Si unaona Zanzibar; Karume kataka mwenyewe Muungano haraka kwa kuogopa kupinduliwa, leo inaonekana kalazimishwa na Nyerere.

Baada ya Uhuru kupatikana, Titi alipata ubunge jimbo la Rufiji, na akachaguliwa kuwa Waziri Mdogo wa Wizara ya Utamaduni na Maendeleo. Alikuwa pia mweyekiti wa mwanzo wa UWT na kiongozi mwanadamizi wa East African Muslim Welfare Society (tawi la Tanganyika), pamoja na mjumbe wa Maulid Committee (kamati ndogo ya kuandaa Maulid kila mwaka). Mwenyekiti hapo akiwa waziri mwenzake Tewa Said Tewa (Mbunge wa Kisarawe) na Chifu bdallah Said Fundikira aliyepata kuwa Waziri wa Sheria akawa Katibu.

Timu hiyo, kwa kushirikiana na wajumbe wengine wa EAMWS hapa nchini walifanya mambo makubwa sana katika kuendeleza Uislamu na Waislamu; na kwa kiasi fulani walifanikiwa katika kutaka kupunguza pengo lililopo kielimu baina ya Waislamu na watu wa dini nyengine.

Kufumba na kufumbua, waliweza kupata kiwanja kikubwa pale Chang’ombe karibu na Uwanja wa Taifa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha kwanza Tanganyika, kabla hata kile cha Mlimani hakijaanza.

Pamoja na kumwalika Nyerere kuja kuweka jiwe la msingi, Nyerere na serikali anayoingoza, hakupendezwa na jambo lile. Mipango ikafanywa, si tu kuusimamisha mradi ule uliokuwa unafadhiliwa na Rais wa Misri wakati huo, Gamal Abdel Nasser, bali kuivunja kabisa taasisi ile ya EAMWS na kuwaundia Waislamu baraza jengine.

EAMWS, lilikuwa na nguvu kubwa sana kwa kila hali, maana ndani yake lilijumuisha madhehebi zote za dini ya Kiislamu wakiwamo Waismailia, Mabohora, Waithnasheri, Mashia, Ibadhi na Ahmadia. Patron wake alikuwa ni H.H. Aga Khan likiwa na madhumuni ya kusaidia na kuendeleza Uislamu.

Mwalimu na wenzake katika TANU, pamoja na kukataa ubaguzi kwa kukubali kuwapokea na kuwapigia kura Wahindi kwenye mpango wa ‘kura tatu’, kwenye hili la Uislamu— Wahindi wakaonekana Wahindi— hawakutakiwa wasaidie Waislamu wenzao na hapo ikavunjwa EAMWS kwa amri ya Serikali na likaundwa BAKWATA la Waafrika watupu (Sunni tu).

Titi alipoteza kiti chake cha ubunge Rufiji kwa mtu aliyekuwa si maarufu hata kidogo. Tewa naye alipoteza Kisarawe na alipelekwa kuwa Balozi wa Tanzania kule China. Alhaji Chifu Abdallah Said Fundikira, akapelekwa Nairobi, Kenya kuwa Mwenyekiti wa ‘marehemu’ Shirika la Ndege la Jumuiya Afrika Mashariki (EAAC)—liliuawa kikatili Juni 30,1977.

Ndani ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU, hayati Bibi Titi alipambana na kuwagaragaza wanasiasa wakongwe kwa hoja nzito pale mjadala wa kuivunja EAMWS ulipokuwa unajadiliwa na halmashauri hiyo.

Bibi Titi mwenyewe, miaka 30 baada ya kuangushwa kwake kisiasa, ameliambia gazeti la Rai kwamba kuanguka kwake kisiasa kulisababishwa na kule kumpinga Nyerere kwenye Halmashauri Kuu ya TANU, wakati Nyerere alipokuwa anatafuta kuungwa mkono na Waislamu ndani ya chama kwa kuivunja EAMWS.

Mnamo mwaka 1968, Bibi Titi alikamatwa pamoja na mwanasiasa mwengine aliyepata kuwa Waziri wa Kazi na kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi nchini Michael Kamaliza, kwamba walishirikiana na wanajeshi wengine wane wakitaka kumuua na kuipindua serikali ya Nyerere. Titi na wenzake walitiwa hatiani katika kesi iliyochukuwa siku 120 kusikilizwa; na hivyo kufungwa jela maisha.

Waswahili wana msemo usemao; tenda wema nenda zako. Habari za kukamatwa na kufungwa jela kwa Bibi Titi ziliwashitua na kuwasikitisha mno watu wa Kenya; na hasa wanawake ambao walikuwa wana deni kwake.

Mwanamama mmoja, mwanasiasa machachari nchini Kenya, alivuka mpaka na kumfuata Nyerere Butiama, alikokuwa amepumzika baada ya kuomba wakutane huko mbele ya mamake Mwalimu, Mama Mgaya.

Baada ya mapokezi na maamkizi, mama yule alimkabili Nyerere uso kwa uso na kumwambia kuwa alichofanya ni kukosa fadhila kwa Bibi Titi, ambaye amewafanyia makubwa watu wa Afrika Mashariki ujanani kwake.

‘’Utakuwa ni wizi wa fadhila na kukosa utu kama wewe Nyerere utaendelea kumfunga jela Bibi Titi kwa yote aliyokufanyia wewe, nchi yako na wapenda haki na usawa wote wa upande huu wa dunia

“Tafadhali sana nakuomba nimetumwa kwako nikiwakilisha watu wa Kenya na wanawake wa nchi hizi mbili umwachie huru Bibi Titi, kama yeye alivyopambana na Wazungu mpaka Kenyatta wa kwetu (Kenya) akatoka jela,’’ Alimaliza mama yule akarudi kwao Kenya.

Akiwa ofisini kwake Kenya tayari ameshasahau; siku moja akapata habari kwamba kuna mgeni kutoka Tanzania anataka kumwona. Akaagiza apitishwe. Alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje John Samuel Malecela akiwa na ujumbe kutoka kwa Mwalimu: “Nimetumwa nije nikupe habari njema kwamba Nyerere tayari ameshamwacha huru Bibi Titi,”alisema Waziri Malecela.

Mama alijibu, “Kamwambie Nyerere kwamba kwa niaba ya wanawake wa Kenya na watu wa Afrika Mashariki, ninasema ahsante sana, kwa uungwana wake,”alimaliza

Hivyo ndivyo alivyofungwa na kufunguliwa mama yetu aliyerejea tena kuishi maisha ya chini kabisa ya kawaida kule Temeke, Mtaa wa Ngarambe, maana nyumba zake mbili za kisasa pale Upanga alizokuwa akimiliki wakati wa enzi zake za uongozi zilitaifishwa na Azimio la Arusha. Aliwekwa chini ya ulinzi fulani hivi (semi house arrest), maana kutwa alikuwa akikaa nje barazani kwake akiiuza mafuta ya taa kwa kupimia watu rejareja na siku zikawa zinasogea mbele. Rais Mwinyi alipokuja madarakani alimrejeshea mama yule zile nyumba zake mbili pale Upanga, na habari zinasema akapewa na senti mbili tatu kujiendesha maisha yake yaliyobaki.

Tunamwomba Mola ailaze mahala pema peponi roho ya mama yetu huyu—Ameen! Ameen!.
 
Bibi Titi
IMG-20180708-WA0011.jpg
 
Back
Top Bottom