Story za mkeo/mpenz wa ndoa


Ujue kuna watu wengine visirani pia.

Akikigeuza kisirani chake kako, chochote utakachofanya hapendi, anataka ufanye chengine.

Again muhimu kujuana mwanzo.
 

Ukisoma kwa nia ya kuelewa utaona huyu mke anamuongelesha mume kwa nia ya kuwa na mazungumzo ya pande mbili kati yao, lakini mume ndo haongei.

Sijui hili umelikosa vipi wakati ndo msingi wa thread nzima.
 

heheeee mechekajeee lol yaani kweli sometimes yabidi kuwa kichwa ngumu manake..
 
oh my God,pole Sakapal,labda nami pia namkera mke wangu kwa tabia kama hiyo,labda hajaniambia tu,ngoja nirudi nikajichunguze kama nami namboa kama wewe unavyoborewa na mmeo nijirekebishe!asante kwa mada yako

thats good congrats Mc Tilly Chizenga enjoy ur conversation with ur wife
 

Thanx but hadi nakuja kwenu nshacheza ngoma zote za kimanyema hadi kimakua but mdundo ni uleule inachosha na inaudhii, mi nilikuwa muongeaji frm day one coz alinikuta naongea na watu ndo hapo na alipenda sauti tuu...
sasa nashangaa au sauti yangu imebadilika na kuwa besi lol
 
Ukisoma kwa nia ya kuelewa utaona huyu mke anamuongelesha mume kwa nia ya kuwa na mazungumzo ya pande mbili kati yao, lakini mume ndo haongei.

Sijui hili umelikosa vipi wakati ndo msingi wa thread nzima.

jamani sio kila wakati muda wa maongezi...mjue wanaume wana mengi kichwani muwapage mda wa kufikiria kidogo...story njia nzima? ndo mana couples zingine kila mtu anakua na gari lake angalau mkirudi nyumbani mnakua mmemissiana...
 
Afu kuongea ni kipaji mjue.

Kuna wengine wanaongea huku kipaji hawana ni sababu ya stress.

SIsi home wote tuna maneno kama chereani na tunajua tuliporithi kwa baba yetu...mama ni mkimya mpaka ana bore.

Kuna dada yangu yeye ndio alikuwa King wa story ndani. Yani huyo mnaweza kuangalia movie wote afu yeye akaanza kuisimulia...na bado hutataka amalize...hata akirudia same story kesho bado hutachoka kumsikiliza.

Afu alikuwa akitaka kuanzisha story anaanza kucheka wee mpaka machozi yanamtoka...hapo sie wengine tunakaa mkao wa kula, tunajua kuna bonge la story linakuja.

Unaweza kwenda nae mahali mkakutana na kituko...mkifika home anaanza kukisimulia kwa waliobaki...yani unashangaa anavyopangilia maneno mpaka na wewe uliyekuwa naye mkojo unakubana kwa kucheka.

Kuongea kipaji na ukiwa nacho huwezi kuwabore wanaokusikiliza.
 
jamani sio kila wakati muda wa maongezi...mjue wanaume wana mengi kichwani muwapage mda wa kufikiria kidogo...story njia nzima? ndo mana couples zingine kila mtu anakua na gari lake angalau mkirudi nyumbani mnakua mmemissiana...

Sawa,

Lakini kama mtu huko katika mood ya maongezi si unasema?

Halafu huyu mke anakwambia akinyamaza baba anamkoromea kwa nini kawa kimya.

Damned if she does, damned if she doesn't. Hilo unalionaje sasa?
 
Sawa,

Lakini kama mtu huko katika mood ya maongezi si unasema?

Halafu huyu mke anakwambia akinyamaza baba anamkoromea kwa nini kawa kimya.

Damned if she does, damned if she doesn't. Hilo unalionaje sasa?

:biggrin1: ndio maana wanaitwa WANAUME
 

ha ha haaaa... yaan uko kama mke wangu...lakini mimi huwa namsikiliza...kiukweli sio kwamba hapendi kukusikiliza lakini inategemeana na kazi anayofanya mumeo coz kama ni kazi inayomtaka aconcetrate then by the time akirud home anakuwa amechoka sana...hakika anakupenda tatizo ni hilo tu uchovu. Hata mie kama kuna siku nimechoka sana namuambia plz naomba tulale...!!!
pole sana Sakapal, bt trust me anakupenda wala hajakuchoka tatizo ni stress tu za mjini.
 

ndo nimeipata leo hii that ur from jupiter and we r from mars, basi kuelewana kwetu ni kuvumiliana tuu na si ubabe wa unachotaka wewe au ninachotaka mimi tuu, kumbuka kwanza si wanawake wote wanapenda kukaa bar hasa walioolewa coz akiwaza akirudi home anamajukumu kibao, kufua nguo za ndani, usafi wa chumba chake, kumuandalia mume msosi, kupata report frm sanyato ya siku nzima ya home na ya watoto walishindaje, kukagua homework za watoto, kuandaa nguo za kesho job, kuahkiki sanyato halali bila jiko kuwa safi na nguo za watoto kaandaa na viatu, vitafunio vya asubuhi kesho yake vipo, kupata dosi ya mume home ni tabu tupu hata siku moja mwanamke hatamwambia hubby wake twende bar kwanza mume atashtuka umeanza lini hii tabia na ugomvi utaanzia hapo na kitakugeukia balaa.
Na wanaume ukiwapa deal za hela hawapendi sana coz atahisi utakuwa umezipata kwa mwanaume mwingine ambaye labda atakuwa ameshakumega so hizi nazipeleka kwa kaka yangu au mdogo wangu wa kiume na nikitaka hubby aijue namwambia huyu kaka yangu ndo ailengeshe kwa hubby. Tatizo wanaume hawatabiriki waweza fanya jambo kwa wema likaishia kukutoa jasho na ukajuta hata idea ilipoanza kukujia kichwani kwa nn hukuipuuzia.
Siwezi mpeleka mume wangu bar kumsimulia mambo ya kichenparty au send off ila huwa namwambia michango niliyonayo kwa mwezi huu ili nikimuomba hela ajue kuwa ya kwangu imetumbukia bahari ya masherehe na hii sio kila mwezi aah ahh.
Sometimes we need social life na wewe mwanaume kama unashindwa tafuta madel ya hela kwa wanaume wenzio ungoje mkeo akuletee kwanza utakuwa uko kimaslahi zaidi kuliko mapenz, pili mkeo akiwa hivi jua kuwa analiwa Tg..
wala research yako siendi ifanya hata kwa dawa, akili za kuambiwa changanya na zako lol
thanx for ushauri anyaways
 
ha ha ha........................ kama hansadi vile..umenukuu kila kitu
 
Afu kuongea ni kipaji mjue..Kuna wengine wanaongea huku kipaji hawana ni sababu ya stress.

nyumba kubwa well said..
Kweli bwana kuna watu kuongea wamejaaliwa yaani wanajua namna ya kupangilia maneno mpaka basi..
Ninaye shemeji yangu kwa kweli ukifika kwake unabaki kucheka tu..she is truly a charming lady..
Bahati mbaya mume wake hapendi vile anavoongea..so, unakuta akianza stori zake broo anaanza kumtuma ili mradi amkate flow ya maongezi..Kingine nilichogundua kupitia huu uzi..wanaume wengi hawapendi kustorishwa na wake zao..
Na wanapenda ile ya one way traffic conversation..yaan mke awage wa kuulizwa na kuitikia tu..lol!!
 
Last edited by a moderator:

Mmmh!i mkuu ikitokea hivyo (kwa red) ujue wazi tu kwamba you were wrong in your selection
 
Usichulie wanaume wa MMU kama sample...unajua kwa nini?...mimi nadhani wengi wao ni waongeaji ndio maana wakawa members wa MMU in the first place.

Ni kawaida ya wanaume waongeaji kutokupenda wanawake waongeaji....kwa kuwa wanataka audience, sasa mkiongea wote nani amsikilize nani?

Mimi mwenyewe maishani mwangu sijawahi ku date mwanaume mwenye maneno ka chiriku. Maana najua tutakuwa tunapiga kelele si kuongea...na wala nisingeweza kudumu na mtu anaye ni shut nikiongea.

Na nikikutana na mtu awe ke au me anayeongea sana mi huwa nakaa kimyaaa. Kuna dada nimemjua kama mwaka hivi ni muongeaji....basi nikiwa nae mi natingisha kichwa tu maana simuwezi. Huyo dada ni mwanasiasa... na anajisifugi 'unajua sisi wanasiasa tunaongea sana'...mi nasema 'nawajua sana' aliwahi mpaka kugombea ubunge akakosa. Ila mume wake nimeshakutana nae ni mkimyaaa otherwise sijuhi kama angeweza kuishi na vuvuzela maana most ya mazungumzo yake ni nonsense.


 

BIG UP SANA Kiranga :yo:
 

Nadhani umefanya research yako wrongly..
Itakuwa kitu cha ajabu sana kama unadate mtu ambaye hamna 'compatibility'..
Miongoni mwa vitu vinavyowafanya watu wawe pamoja ni hili la kustorishana..
Sikatai inawezekana kuna 'extreme cases' ambapo me au ke ni mwongeaji kuliko mwenziwe kiasi cha kupigiwa mfano..
But my brain tells me kwamba pale ambapo kuna mwanamke muongeaji kuna mwanaume muongeaji pia..
Sema kwa muktadha wa mleta mada inaonekana 'wameanza kuchokana'..yaan mume hana furaha tena na stori za mkewe
 
leo ukiingia tu kwenye bajaji weka headphones masikioni then weka sauti kubwa imba na kufuatia wimbo unaousikiliza ,then mlie chabo anajisikiaje then unipe majibu yangu

heheeee weweeeee hunitakii mema sifanyi hivo hata siku moja lol!! ya nini kunaswa kibao hali bajaji yenyewe haina tinted lol
au tatavizia kona kali apige spidi kubwaa na mie sina hili wala lile aniangushe ili kuniudhii tu aaah nakula kobisi tu hadi aanzishe yeye story lol
 
pole dada. ninachokiona hapa midundo yenu haiendani, kila mmoja wenu anadunda kivyake. pole sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…