Story za mkeo/mpenz wa ndoa

Story za mkeo/mpenz wa ndoa

story zangu za kawaida sana wala sidhani kama zinaboa, lakini pia nisiusemee moyo wa mtu may be zinamboa shida ni kwamba mdomo anao why haniambii? hajawahi sema na bikiona sisikilizwi au nakatishwa njiani nanyamaza baada ya muda utasikia mbona huongei, umeamua kuninunia sasa sielewi sijui ndo hii sitaki nataka au madeko tuu looh kama hapendeki...?

Ujue kuna watu wengine visirani pia.

Akikigeuza kisirani chake kako, chochote utakachofanya hapendi, anataka ufanye chengine.

Again muhimu kujuana mwanzo.
 
hapa mtoa mada umeonyesha jinsi ambavyo wanawake wako selfish..kwanini wewe uongee kila wakati? kwanini usikilizwe wewe tu kila wakati..mbona hutaki na yeye aongee mbona hutaki na yeye akupe story za kwake why should men always listen to women and not the other way around..sometimes sisi wanaume tunapenda ule ukimya kutafakari mambo mengi kichwani so kila mahali mkiwa mnaongea ni rahisi kupotezea...kwanza bora hata wa kwako anaongeza sauti ya redio..wengine wanaweza kua wanakuitikia we ukajua wanakusikiliza lakini mawazo yao yako mbali

Ukisoma kwa nia ya kuelewa utaona huyu mke anamuongelesha mume kwa nia ya kuwa na mazungumzo ya pande mbili kati yao, lakini mume ndo haongei.

Sijui hili umelikosa vipi wakati ndo msingi wa thread nzima.
 
sakapal, On Point, yaani on point kabisa.

Kuna watu kuongea utadhani analipia, achia mbali humlazimishi akusimulie yake hata kusikiliza yako tu taabu.

Mie nilishafanya maamuzi magumu, Ninaongea kila ninachojosikia, achambue yanayomhusu.
Ila tatizo langu huwa nataka nikiongea mtu anitazame usoni "eye contact'

Kama kuna tv iko on redio kuna wakati nazima ili tuongee.
Can you imagine ukaongelee wapi?? Au uanze kwenda nyumba ya tatu kupiga story wakati kwako kuna watu?? lol

heheeee mechekajeee lol yaani kweli sometimes yabidi kuwa kichwa ngumu manake..
 
oh my God,pole Sakapal,labda nami pia namkera mke wangu kwa tabia kama hiyo,labda hajaniambia tu,ngoja nirudi nikajichunguze kama nami namboa kama wewe unavyoborewa na mmeo nijirekebishe!asante kwa mada yako

thats good congrats Mc Tilly Chizenga enjoy ur conversation with ur wife
 
Cha mhimu dada yangu jaribu kuona ni aina gani ya story anazopenda. Vilevile as a learned lady you should know WHEN to talk to your husband and HOW to talk to him. You know him better than any one on this forum. All the best in search for harmony and peace and lovely family. Be blessed

Thanx but hadi nakuja kwenu nshacheza ngoma zote za kimanyema hadi kimakua but mdundo ni uleule inachosha na inaudhii, mi nilikuwa muongeaji frm day one coz alinikuta naongea na watu ndo hapo na alipenda sauti tuu...
sasa nashangaa au sauti yangu imebadilika na kuwa besi lol
 
Ukisoma kwa nia ya kuelewa utaona huyu mke anamuongelesha mume kwa nia ya kuwa na mazungumzo ya pande mbili kati yao, lakini mume ndo haongei.

Sijui hili umelikosa vipi wakati ndo msingi wa thread nzima.

jamani sio kila wakati muda wa maongezi...mjue wanaume wana mengi kichwani muwapage mda wa kufikiria kidogo...story njia nzima? ndo mana couples zingine kila mtu anakua na gari lake angalau mkirudi nyumbani mnakua mmemissiana...
 
Afu kuongea ni kipaji mjue.

Kuna wengine wanaongea huku kipaji hawana ni sababu ya stress.

SIsi home wote tuna maneno kama chereani na tunajua tuliporithi kwa baba yetu...mama ni mkimya mpaka ana bore.

Kuna dada yangu yeye ndio alikuwa King wa story ndani. Yani huyo mnaweza kuangalia movie wote afu yeye akaanza kuisimulia...na bado hutataka amalize...hata akirudia same story kesho bado hutachoka kumsikiliza.

Afu alikuwa akitaka kuanzisha story anaanza kucheka wee mpaka machozi yanamtoka...hapo sie wengine tunakaa mkao wa kula, tunajua kuna bonge la story linakuja.

Unaweza kwenda nae mahali mkakutana na kituko...mkifika home anaanza kukisimulia kwa waliobaki...yani unashangaa anavyopangilia maneno mpaka na wewe uliyekuwa naye mkojo unakubana kwa kucheka.

Kuongea kipaji na ukiwa nacho huwezi kuwabore wanaokusikiliza.
 
jamani sio kila wakati muda wa maongezi...mjue wanaume wana mengi kichwani muwapage mda wa kufikiria kidogo...story njia nzima? ndo mana couples zingine kila mtu anakua na gari lake angalau mkirudi nyumbani mnakua mmemissiana...

Sawa,

Lakini kama mtu huko katika mood ya maongezi si unasema?

Halafu huyu mke anakwambia akinyamaza baba anamkoromea kwa nini kawa kimya.

Damned if she does, damned if she doesn't. Hilo unalionaje sasa?
 
:biggrin1: ndio maana wanaitwa WANAUME
 
Morning every one!! I salute you all, SALUTE!!!

Ni hivi , leo nina swali kwa wanaume hasa waliooa au walio kwenye mahusiano na mwanamke kwa muda mrefu, tafadhali naomba mueleze ukweli ili kunisaida mimi na hata wadada wengine wenye shida kama hii.

Niko na mahabat wangu, tunatabia ya kuondoka wote home kwenda kazini na kurudi pamoja kwa kutumia kabajaji ketu si unajua bongo usafiriwa shida? Na hii imekuwa ikitupa nafasi ya kuongea mambo mengi njiani na tukifika home ni kuangalia watoto kuoga na kulala. Sasa shida iko hivi, mimi napenda sana kuongea na hili analijua utakuta ile nimeingia tu kwenye gari naanza story sometimes za kuchekesha, sometimes za ofisini yaliyojiri ofisini kwetu siku nzima, leo nani kafanyaje, nani kaambiwa nn na bosi, mkutano leo ulikuwaje, na sometime hata siri za ofisi au mikakati ya ofisi yetu namtaarifu nikijua ni maongezi tu looh. Sijui anakuwa anachoka kusikiliza au hapendi tena sauti yangu yaani utakuta unaongea in btw hata hujamaliza anaongeza sauti ya redio like ninyamaze. Unakaa kimya baada ya muda unaanzisha story ingine heee! unashangaa anakuuliza kitu kingine tofauti labda nilikuwa nasimulia kuhusu habari ya watoto utasikia tuu wale mafundi walimaliza jana uliwalipa hela yao yote looh! nachokaje?
Baada ya kuona shida inazidi na sipati nafasi nzuri ya kusikilizwa nikaona bora nikae kimya na tuwe wote mabubu njia nzima toka mjini hadi home yaani napata shida.
SWALI;- Hivi kwa nini wanaume hampendi kusikiliza masimulizi ya wake zenu? hii hata kijana mmoja hapa ofisini nilishamsikia akiongea kwamba kunarafiki yake ameoa mwaka jana ila ukifika muda wa kwenda kwake hatamani coz anawaza jinsi ya kusikiliza story za mke wake za siku nzima na mkewe huyo anataka mumewe amsikilize hadi amalize. To me huyu kijana anaboreka na hizi story na amechoka kuzisikiliza, sasa kwa nini nyie wanaume msiwaambie wazi wake zenu kwamba usipige story zako za kutwa nzima? au mwambie kwa upole tu pls nimechoka leo naomba tuongee asubuhi au hata ukamwambia nasikia kichwa kinauma reserve the rest for tomorrow huyu mwanamke atakuwa in good place ya kukuelewa that u need a space ila isiwe kila siku. A u hata ukamsikiliza tu then akimaliza yule mwanamke anafurah basi na wewe unaendelea na mambo yako. Naomba niwaibie siri nyie wanaume...,
Sikilizeni wake zenu, hii ni kitu ndogo na ya kijinga but ni kubwa na ya muhimu sana hasa kwa wanawake yaani kama mm hapa naugulia coz sisikilizwi story zangu naishia kujikuta naongea mwenyewe na mbaya zaidi kunawakati anakwambia njoo tuongelee kitandani wakati wa kulala akishapata tunda lake ukirudi kuoga unamkuta anakoroma sometimes unamkuta macho but unaanza story ukijastuka mwenzio alishalala saa nyingi, inaudhi kweli muwe mnatuambia kwamba usiongee baby ninausingizi sana.
Mie napenda sana kuimba hata sometimes unaskia kero kumuimbia coz ukiimba anaona kama unampigia kelele yaani wanaume naomba mnisaidie shida ni nini?
Hampendi story? je ni story za kipuuzi? mbona hamsemi? maudhiiiiiiiiii??

Ever remaining,
Sakapal

ha ha haaaa... yaan uko kama mke wangu...lakini mimi huwa namsikiliza...kiukweli sio kwamba hapendi kukusikiliza lakini inategemeana na kazi anayofanya mumeo coz kama ni kazi inayomtaka aconcetrate then by the time akirud home anakuwa amechoka sana...hakika anakupenda tatizo ni hilo tu uchovu. Hata mie kama kuna siku nimechoka sana namuambia plz naomba tulale...!!!
pole sana Sakapal, bt trust me anakupenda wala hajakuchoka tatizo ni stress tu za mjini.
 
na nyie wanawake wengi mmezidi kulalamika mara ohh hatusikizwi mara wanaume this wanaume that...dont u knw maisha ya ndoa ni zaidi ya kusikiza stori zenu andf mostly kwetu wanaume huwa tunaziona "hazina tija na majiungu yasojenga"..am givin you a lil home work mukaifanye kwa nyakati zenu tofauti kila mmoja na mumewe na mutuletee mrejesho.
1- siku 1 jioni mnatoka kazini mcheck mmeo kama anaonyesha dalili za uchovu then mwambie hny lets stop by a nearby joint tukapige mdogomdogo plus story coz kuna deal la kuingiza kiasi flani cha pesa nadhani ushauri wako unahitajika sana, na mkifika agizeni kinywaji then mama anza kumpa hiloo deal la pesa na liwe kama la kifisadi hivi uone jinsi usikivu wa mzee utavyokuwa juu na cooperation ya kutosha to every detail of the deal.
2- another day mnatoka kazini fanya kama hapo juu(1) ila muambie tunaenda kuongelea jinsi shosti yako anavyozinguana na mmewe kiasi wanataka kupeana talaka, au kujadili jinsi mnavyoandaa sendoff ya rafiki yako mpo naye ofcn na wewe ni katibu wa kikao cha kina mama uone na upime usikivu wa mzee.

katika vikao vyote pima yafuatayo
1- attentiveness to your presentation of matters
2- contributions zake kwenye mada nzima
3- idadi yaq bia/soda atazokunywa katika kila kikao
4- muda mutakao tumia kukaa pamoja kujadiliana kwa kila kikao
5- idadi ya simu atazopiga katika kila kikao
6- conclussion yake kwa kila kikao na je kikao kipi kita-amsha au kuendeleza maongezi nyumbani hata usiku wa manane.

majibu utayopata ndio yatakupa picha sahihi ya aina ya story wanaume wanazopenda kusikia toka kwa wapenzi/wake zao.

irizi wari irizi..we r from jupiter you are from marzz.

ndo nimeipata leo hii that ur from jupiter and we r from mars, basi kuelewana kwetu ni kuvumiliana tuu na si ubabe wa unachotaka wewe au ninachotaka mimi tuu, kumbuka kwanza si wanawake wote wanapenda kukaa bar hasa walioolewa coz akiwaza akirudi home anamajukumu kibao, kufua nguo za ndani, usafi wa chumba chake, kumuandalia mume msosi, kupata report frm sanyato ya siku nzima ya home na ya watoto walishindaje, kukagua homework za watoto, kuandaa nguo za kesho job, kuahkiki sanyato halali bila jiko kuwa safi na nguo za watoto kaandaa na viatu, vitafunio vya asubuhi kesho yake vipo, kupata dosi ya mume home ni tabu tupu hata siku moja mwanamke hatamwambia hubby wake twende bar kwanza mume atashtuka umeanza lini hii tabia na ugomvi utaanzia hapo na kitakugeukia balaa.
Na wanaume ukiwapa deal za hela hawapendi sana coz atahisi utakuwa umezipata kwa mwanaume mwingine ambaye labda atakuwa ameshakumega so hizi nazipeleka kwa kaka yangu au mdogo wangu wa kiume na nikitaka hubby aijue namwambia huyu kaka yangu ndo ailengeshe kwa hubby. Tatizo wanaume hawatabiriki waweza fanya jambo kwa wema likaishia kukutoa jasho na ukajuta hata idea ilipoanza kukujia kichwani kwa nn hukuipuuzia.
Siwezi mpeleka mume wangu bar kumsimulia mambo ya kichenparty au send off ila huwa namwambia michango niliyonayo kwa mwezi huu ili nikimuomba hela ajue kuwa ya kwangu imetumbukia bahari ya masherehe na hii sio kila mwezi aah ahh.
Sometimes we need social life na wewe mwanaume kama unashindwa tafuta madel ya hela kwa wanaume wenzio ungoje mkeo akuletee kwanza utakuwa uko kimaslahi zaidi kuliko mapenz, pili mkeo akiwa hivi jua kuwa analiwa Tg..
wala research yako siendi ifanya hata kwa dawa, akili za kuambiwa changanya na zako lol
thanx for ushauri anyaways
 
Na mjaribu saa ingine kuja na story za kuongeza kipato ili familia imee sio mastori ya harusin na maofisini mwenu tu kila siku bana yaaani uje na say mpango wa biashara na jinsi ya operationalization mimi ntakusikiliza kila siku hata wa manane ila ya Mke; Honey nikwambie kitu..........
Mume; Enheee........
Mke; Jana ofisini ile kikao yooote mpaka jioni ile tukatoka secretary na bosi tumewaacha ofisin ana inasemekana wana uhusiano wa kimapenzi
Mume; Bad Habit.........
Mke; Inauma sanaaa

At Home......
Mke; Mume wangu
Mume; Naam......
Mke; Hivi unajua this weekend ndo ile send-off
Mume;Owk....ntakupeleka then ukiwa tayari ntakufuata mke wangu.....
Mke; Sasa utakuta kwenye send-off watu huwa wanajikandika mipoda kama wachawi yaani mi sipendagi...........
Mume; Ngrrrrrrrrrrrrrrr.........................ngrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr kalala zamaaaaani as mistory yako inaboa saaaaanaaaaaaa na ni non-constructive

Tafakari................chukua hatua
ha ha ha........................ kama hansadi vile..umenukuu kila kitu
 
Afu kuongea ni kipaji mjue..Kuna wengine wanaongea huku kipaji hawana ni sababu ya stress.

nyumba kubwa well said..
Kweli bwana kuna watu kuongea wamejaaliwa yaani wanajua namna ya kupangilia maneno mpaka basi..
Ninaye shemeji yangu kwa kweli ukifika kwake unabaki kucheka tu..she is truly a charming lady..
Bahati mbaya mume wake hapendi vile anavoongea..so, unakuta akianza stori zake broo anaanza kumtuma ili mradi amkate flow ya maongezi..Kingine nilichogundua kupitia huu uzi..wanaume wengi hawapendi kustorishwa na wake zao..
Na wanapenda ile ya one way traffic conversation..yaan mke awage wa kuulizwa na kuitikia tu..lol!!
 
Last edited by a moderator:
Mwanamme anayejua maongezi anamjibu vizuri mkewe na kuyaongoza hayo maongezi kuelekea kule anakofikiri kunafaa zaidi.

Sasa wewe unaona mkeo anaendekeza gossip, badala ya kuonyesha hufagilii na kuongea habari hizo hizo kwa kina zaidi, unamuacha mamaa anakuwa kama anafanya jitihada za kuwa social wakati wewe ume mute.

Unakosa mvuto.

Unaweza kupinduliwa kwa kitu kidogo tu, katokea kijana mtanashati hana lolote zaidi ya maongezi mazuri, anakufanya mbaya.

Halafu utalalamika wanawake wa siku hizi wasaliti.

Kumbe usaliti umeanza mwenyewe kwa emotional neglect iliyo borderline torture.

Mara nyingine mtu anaweza kuanza kuongelea weather sio kwa maana ya kwamba anataka kuongelea weather, anataka ku crack the ice tu kwa nyepesi nyepesi, sasa kama mwanamme kichwa you take that and run, you build up the convo.

Sasa wewe mtu kaanza na weather tu unasema huyu naye kashaanza story zake za ajabu ajabu.

Utaonyesha humpendi, anakuboa. Mtu kama unampenda kweli hata akikoroma utaona kama muziki.

Na akileta story nyepesi nyepesi unazipeleka kunako, si kumchunia.

Mmmh!i mkuu ikitokea hivyo (kwa red) ujue wazi tu kwamba you were wrong in your selection
 
Usichulie wanaume wa MMU kama sample...unajua kwa nini?...mimi nadhani wengi wao ni waongeaji ndio maana wakawa members wa MMU in the first place.

Ni kawaida ya wanaume waongeaji kutokupenda wanawake waongeaji....kwa kuwa wanataka audience, sasa mkiongea wote nani amsikilize nani?

Mimi mwenyewe maishani mwangu sijawahi ku date mwanaume mwenye maneno ka chiriku. Maana najua tutakuwa tunapiga kelele si kuongea...na wala nisingeweza kudumu na mtu anaye ni shut nikiongea.

Na nikikutana na mtu awe ke au me anayeongea sana mi huwa nakaa kimyaaa. Kuna dada nimemjua kama mwaka hivi ni muongeaji....basi nikiwa nae mi natingisha kichwa tu maana simuwezi. Huyo dada ni mwanasiasa... na anajisifugi 'unajua sisi wanasiasa tunaongea sana'...mi nasema 'nawajua sana' aliwahi mpaka kugombea ubunge akakosa. Ila mume wake nimeshakutana nae ni mkimyaaa otherwise sijuhi kama angeweza kuishi na vuvuzela maana most ya mazungumzo yake ni nonsense.

nyumba kubwa well said..
Kweli bwana kuna watu kuongea wamejaaliwa yaani wanajua namna ya kupangilia maneno mpaka basi..
Ninaye shemeji yangu kwa kweli ukifika kwake unabaki kucheka tu..she is truly a charming lady..
Bahati mbaya mume wake hapendi vile anavoongea..so, unakuta akianza stori zake broo anaanza kumtuma ili mradi amkate flow ya maongezi..Kingine nilichogundua kupitia huu uzi..wanaume wengi hawapendi kustorishwa na wake zao..
Na wanapenda ile ya one way traffic conversation..yaan mke awage wa kuulizwa na kuitikia tu..
lol!!
 
Hapo ndo mnaambiwa msifakamie, mmeona kijungu kumbe kina dhahma si kijungujiko.

Inabidi kujua haya mambo kabla hujakuwa na mtu.

Pia, mwanamme wa kweli haogopi challenge ya kumuelekeza mwanamke wake.

Na kujidanganya kwamba mtaongea 'story za msingi' muda woye haiyumkiniki.

Anaweza kuleta story ya gossip kama baba kichwa unaipindua gossip ileile inatoa funzo lenye nugget of wisdom kwake, anaweza kutoa story iliyojaa dharau na kijicho baba akaona nafasi ya kueleza umuhimu wa kuheshimu watu na kuondoa husda, anaweza kumcheka kilema akafunzwa kwa methali 'hujafa hujaumbika'.

Sasa ushaona mke wako ana mapungufu, unataka nani ayarekebishe?

Na kumnyamazisha hakutamuelimisha, mwanamme hafukii tatizo kwa muda, analitatua.

Kumnyamazisha kunatengeneza time bomb litakalolipuka siku moja.

BIG UP SANA Kiranga :yo:
 
...Ni kawaida ya wanaume waongeaji kutokupenda wanawake waongeaji....kwa kuwa wanataka audience, sasa mkiongea wote nani amsikilize nani?..Mimi mwenyewe maishani mwangu sijawahi ku date mwanaume mwenye maneno ka chiriku. Maana najua tutakuwa tunapiga kelele si kuongea...na wala nisingeweza kudumu na mtu anaye ni shut nikiongea.

Nadhani umefanya research yako wrongly..
Itakuwa kitu cha ajabu sana kama unadate mtu ambaye hamna 'compatibility'..
Miongoni mwa vitu vinavyowafanya watu wawe pamoja ni hili la kustorishana..
Sikatai inawezekana kuna 'extreme cases' ambapo me au ke ni mwongeaji kuliko mwenziwe kiasi cha kupigiwa mfano..
But my brain tells me kwamba pale ambapo kuna mwanamke muongeaji kuna mwanaume muongeaji pia..
Sema kwa muktadha wa mleta mada inaonekana 'wameanza kuchokana'..yaan mume hana furaha tena na stori za mkewe
 
leo ukiingia tu kwenye bajaji weka headphones masikioni then weka sauti kubwa imba na kufuatia wimbo unaousikiliza ,then mlie chabo anajisikiaje then unipe majibu yangu

heheeee weweeeee hunitakii mema sifanyi hivo hata siku moja lol!! ya nini kunaswa kibao hali bajaji yenyewe haina tinted lol
au tatavizia kona kali apige spidi kubwaa na mie sina hili wala lile aniangushe ili kuniudhii tu aaah nakula kobisi tu hadi aanzishe yeye story lol
 
Morning every one!! I salute you all, SALUTE!!!

Ni hivi , leo nina swali kwa wanaume hasa waliooa au walio kwenye mahusiano na mwanamke kwa muda mrefu, tafadhali naomba mueleze ukweli ili kunisaida mimi na hata wadada wengine wenye shida kama hii.

Niko na mahabat wangu, tunatabia ya kuondoka wote home kwenda kazini na kurudi pamoja kwa kutumia kabajaji ketu si unajua bongo usafiriwa shida? Na hii imekuwa ikitupa nafasi ya kuongea mambo mengi njiani na tukifika home ni kuangalia watoto kuoga na kulala. Sasa shida iko hivi, mimi napenda sana kuongea na hili analijua utakuta ile nimeingia tu kwenye gari naanza story sometimes za kuchekesha, sometimes za ofisini yaliyojiri ofisini kwetu siku nzima, leo nani kafanyaje, nani kaambiwa nn na bosi, mkutano leo ulikuwaje, na sometime hata siri za ofisi au mikakati ya ofisi yetu namtaarifu nikijua ni maongezi tu looh. Sijui anakuwa anachoka kusikiliza au hapendi tena sauti yangu yaani utakuta unaongea in btw hata hujamaliza anaongeza sauti ya redio like ninyamaze. Unakaa kimya baada ya muda unaanzisha story ingine heee! unashangaa anakuuliza kitu kingine tofauti labda nilikuwa nasimulia kuhusu habari ya watoto utasikia tuu wale mafundi walimaliza jana uliwalipa hela yao yote looh! nachokaje?
Baada ya kuona shida inazidi na sipati nafasi nzuri ya kusikilizwa nikaona bora nikae kimya na tuwe wote mabubu njia nzima toka mjini hadi home yaani napata shida.
SWALI;- Hivi kwa nini wanaume hampendi kusikiliza masimulizi ya wake zenu? hii hata kijana mmoja hapa ofisini nilishamsikia akiongea kwamba kunarafiki yake ameoa mwaka jana ila ukifika muda wa kwenda kwake hatamani coz anawaza jinsi ya kusikiliza story za mke wake za siku nzima na mkewe huyo anataka mumewe amsikilize hadi amalize. To me huyu kijana anaboreka na hizi story na amechoka kuzisikiliza, sasa kwa nini nyie wanaume msiwaambie wazi wake zenu kwamba usipige story zako za kutwa nzima? au mwambie kwa upole tu pls nimechoka leo naomba tuongee asubuhi au hata ukamwambia nasikia kichwa kinauma reserve the rest for tomorrow huyu mwanamke atakuwa in good place ya kukuelewa that u need a space ila isiwe kila siku. A u hata ukamsikiliza tu then akimaliza yule mwanamke anafurah basi na wewe unaendelea na mambo yako. Naomba niwaibie siri nyie wanaume...,
Sikilizeni wake zenu, hii ni kitu ndogo na ya kijinga but ni kubwa na ya muhimu sana hasa kwa wanawake yaani kama mm hapa naugulia coz sisikilizwi story zangu naishia kujikuta naongea mwenyewe na mbaya zaidi kunawakati anakwambia njoo tuongelee kitandani wakati wa kulala akishapata tunda lake ukirudi kuoga unamkuta anakoroma sometimes unamkuta macho but unaanza story ukijastuka mwenzio alishalala saa nyingi, inaudhi kweli muwe mnatuambia kwamba usiongee baby ninausingizi sana.
Mie napenda sana kuimba hata sometimes unaskia kero kumuimbia coz ukiimba anaona kama unampigia kelele yaani wanaume naomba mnisaidie shida ni nini?
Hampendi story? je ni story za kipuuzi? mbona hamsemi? maudhiiiiiiiiii??

Ever remaining,
Sakapal
pole dada. ninachokiona hapa midundo yenu haiendani, kila mmoja wenu anadunda kivyake. pole sana!
 
Back
Top Bottom