Mbona kama unalialia na kuumia tu ndugu kwa maumivu! Ni wivu ndiyo umekuzidi, au!! Uwe unafurahia jirani yako akifanya kitu kizuri, ma ndipo na wewe utabarikiwa.
Binafsi kama shabiki wa Yanga nitafurahi sana kuona na sisi timu yetu ina uwanja wake binafsi kama ilivyo kwa vilabu vichanga nchini; mfano Azam, Mtibwa, Ihefu, Namungo, nk. Na wewe unatakiwa uombe yule mwekezaji wako mjanja mjanja, na yeye aje na mkakati wa kujenga uwanja wa timu.
Mambo ya kuendelea kutegemea viwanja vya serikali na vile vya ccm! Au kwenda kuhemea uwanja wa Azam Compex; ni upumbavu wa kiwango cha juu sana kwa timu zilizoanzishwa miaka zaidi ya 80 iliyopita.