smarte_r
JF-Expert Member
- Nov 8, 2013
- 4,564
- 12,014
Vipo vitu ambavyo hufundishwi popote. inatakiwa utumie akili yako ya kawaida kujiongeza ili uweze ku-survive
Leo nawaletea codes za kitaa ambazo kama ukizifata zitakusaidia uishi vizuri na watu wa mtaani kwako katika mji wowote hapa tanzania.
1. Jizoeshe kusalimiana na watu wa mtaani kwako
kwa sisi watanzania salamu ni ishara ya amani na njia ya awali ya kutengeneza mahusiano mema na watu. usiwe bahili wa kutoa au kupokea salamu. salimiana na watu wa rika zote wa mtaani kwako. kinyume na hapo, utasemwa vibaya kwamba unajisikia au unaringa. unless you don't care what your neighbors say about you.
2. Shiriki baadhi ya shughuli za kijamii kama misiba au harusi zinazohusu watu wa mtaani kwako
usijifanye kila siku upo busy na kazi, watu wa mtaani kwako wanakuona tu kwa mbali unakatiza na gari lako huku umefunga vioo ukila upepo wa AC.
Siku mojamoja huzunika pamoja na watu wa mtaani kwako kwenye matukio ya huzuni. Pia furahi nao pamoja kwenye matukio ya furaha pale inapobidi.
Watanzania huwa wananongwa sana wanapobaini fulani huwa hashiriki kwenye misiba inayotokea mtaani kwake. Shirikiana nao bila kujali ni kiasi gani umewazidi kimaisha, exposure au elimu.
3. Jizoeshe kununua bidhaa za vyakula kama mchele, unga wa kula au sukari kwenye kiduka cha mangi hapohapo kitaani kwako
Wapo wale wenzangu na mimi ambao mahitaji yao ya kila siku huyanunua kwenye ma-supermarket, which is good. Ila sio mbaya siku moja ukanunua kilo 10 au 20 za mchele kwenye kiduka cha mangi wa hapohapo kitaani kwako.
Hii itakujengea uhusiano mzuri kati ya wewe na yeye. Siku ukiishiwa stock ya chakula na huna fedha ya kutosha ya kwenda kununua vyakula Mlimani City, mangi atakuokoa. atakupa kilo 20 za mchele ule wewe na familia yako kwa ahadi ya kumlipa mwisho wa mwezi.
4. Jiepushe kuwa na madeni ya muda mrefu na mtu/watu wa mtaani kwako, yalipe kwa wakati
Madeni sio kitu kizuri, huwa yanatukosesha furaha na kutuongezea stress.
Bora udaiwe na mtu anayeishi mbali na wewe kuliko udaiwe na jirani yako. mtu huyu atakukosesha confidence kwasababu kimazingira hazipiti siku kadhaa bila ya nyinyi wawili kukukutana, anajua ratiba za mishemishe zako. Utaishiwa maneno ya kumdanganya(watu wenye madeni ni mabingwa wa uongo). Mlipe kwa wakati ili mmalizane kabla hajaanza kukutangaza vibaya kwa majirani.
5. Kwa wanaume, usitongoze mdada wa mtaani kwako ambaye muda mwingi anashinda katika njia ambayo unalazimika kuipita mara kwa mara:
hapa kuna faida na hasara, faida ni pale atakapo kukubalia na hatimaye umle "tunda". Hasara ni pale atakapokukatalia, hapa ndio kwenye tatizo. utaanza kumchukia(hiyo ipo naturally kwa sisi wanaume).
Ile njia ambayo kila mara unalazimika kuipata na ndio ambayo yeye anashinda mda mwingi, utaiona chungu. itakubidi uanze kupita njia nyingine ili umkwepe.
The rule of thumb is kama wewe unaishi mtaa A basi tongoza mdada anayeishi mtaa Z. huyu wa mtaa Z hata akikupa cha mbavu hutokuwa na cha kupoteza, afterall hamuonani mara kwa mara.
6. Chagua vijana watukukutu wawili au watatu wa mtaani kwako wafanye washikaji zako au machawa, ila nenda nao kwa tahadhari
Hii ina faida na itakuja kukulipa siku moja. inawezekana sifa za hawa vijana sio nzuri hapo mtaani kutokana na record yao ya matukio.
Jishushe na wafanye washikaji zako. hawa ndio watakuwa ma-informer wako wa kitaa. watakupa code zote za nani ni mwizi, nani ni mkabaji, nani anauza ngada mtaani kwako na kadhalika.
Watayapatia ulinzi makazi yako, watawaambia wahuni wenzao pale kwa braza smarter msiende kuharibu. ni mchizi wetu.
Ikitokea umeibiwa kitu, watakutajia aliyeiba. Wao ndio watapambana kuhakikisha hicho kilichoibiwa kinarudi. vijana hawa watakusaidia kukupa njia ya wapi uanzie kumsaka mwizi wako.
Code hii nimejifunza kwa mtoto wa tajiri fulani mkubwa sana hapa Tanzania(jina kapuni). mtoto huyu wa tajiri ni down-to-earth and very humble. wahuni wote wakubwa wa jiji la dar ni washkaji zake. wamemsaidia vitu vingi.
7. Kwa wanaoishi nyumba za kupanga au apartment, usijiingize katika mahusiano ya kimapenzi na mke/mume wa mpangaji mwenzio
Hapo kitaani kwako si kuna videmu/vikaka kibao? Hivi kweli umevikosa mpaka ulazimike kuingia ktk mapenzi na mke/mume wa mpangaji mwinzio? Acha mara moja kwasababu unacheza na moto. ipo siku utarushiwa shuka jeupe(kwa sauti ya mzee mpili wa wa ikwiriri) mwisho uanze kufikiria kuhama mtaa au kitongoji.
Ongezea codes nyingine za kitaa ambazo sijazizungumzia. Karibuni.