'Street codes' za kukusaidia uishi vizuri na watu mtaani kwako katika mji wowote Tanzania

Umemaliza mkuu, pointi ya 6 imenisaidia sana kila sehemu napokwenda. Huyu atakuambia achana na yule ni mvuta bangi, mwizi nk, ila wewe mfanye rafiki
 
Kwa hiyo unapingana na mtoa mada??.
 
Karne hii kukaa kwenye vijiwe vya kahawa na draft??
 
8. Epuka nyendo zako zote kuwa wazi sana machoni kwa kila mtu. Miche miche zako nyingi zisiwe zinatabirika. Kwa mfano, unapenda nini zaidi, hupendi nini, unatoka saa ngapi, unarudi nyumbani saa ngapi, unafanya kazi gani, una biashara gani, una mipango gani ya kimaisha, una miliki nini nk.
 
imekaa vizuri sana hii. [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Hii imenishinda kabisa.

Najua kuna mambo nayakosa kwa kutokaa kijiweni lakini sijazowea,kwanza naweza kukaa wakapiga stori ambazo sina interest nazo.

Watakaa waanze kubishana mpira na makelele na hapo kuna wazee,na kubishana kwa makelele siweezi kabisa mwishowe nikitoka wakati wanabishana wataniona ninaringa hivyo nasubiri watulie kisha naondoka kistaili ya aina yake.

Hii imenifanya nisijue majina ya watu ambao nipo nao mtaani wengi tunajuana kwa sura ila majina siwajui,lakini ajabu wao wananijua.

Jambo moja muhimu mtoa mada kagusia ni kununua vitu vidogo vidogo hapo duka la mtaani,jambo muhimu saaaana hili.

Mimi kuna wazee hununua kwao vitu kama sukari,dawa ya mbu,unga,sabuni za unga n.k
Hii imenifanya wanione peace sana kinyume na ambavyo walinichukulia huko nyuma
 
Ahsante sana mkuu, naongezea hasa wale wanaume wanaopenda soka nenda uwanjani hapo ndo wahuni wapo wengi,
Shiriki nao kwenye michezo itakusaidia
 
kukaa kijiweni kupiga story na watu wa mtaani hili hata kwangu huwa linanishinda.

kwanza ratiba zangu haziruhusu, natoka asubuhi narudi jioni. nikirudi home jioni nakuwa nimechoka, huwa sipendi kutoka kwenda kuzurula. natulia zangu home ili nipate mda wa kutosha wa kuwa karibu na familia yangu.
 
Ahsante sana mkuu, naongezea hasa wale wanaume wanaopenda soka nenda uwanjani hapo ndo wahuni wapo wengi,
Shiriki nao kwenye michezo itakusaidia
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 

katika hili acha nikupongeze. mbinu hii inasaidia sana uweze ku-blend na jamii iliyokuzunguka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…