STRESS FREE: Vichekesho on fleak! Weka na cha kwako hapa tufurahi

STRESS FREE: Vichekesho on fleak! Weka na cha kwako hapa tufurahi

Angalia huyu bibi alivyomfanyia huyu jamaa

Bibi na Babu walisafiri wakielekea kwa mtoto wao ambae hawajamuona zamani.

Walipofika njiani wakawa wamechoka Sanaa. Wakaamua kutafuta hotel ili walale.

Wakakubaliana walale kwa masaa 4. Wakalala, Walipoamka, mfanyakazi wa Hotel akawatoza Tsh. 500,000/=

Wale wazee wakashangaa hata kama ni hotel ya kisasa lakini sio laki tano kwa masaa 4.

Babu akagoma kulipa akasema aitiwe meneja.

Meneja akaja kuwasikiliza

Babu: " Kwanini bili ni kubwa hata kama ni hotel ya kisasa?"

Manager;"kuna maswiming puli, ya kisasa "

Babu; "Lakini hatukuyatumia"

Manager; "Ah ah ah. Lakini mungeweza kama mngetaka"

Babu: "Hata hivo bado haithamini kuwa laki 5"

meneja: "Pia Kuna waimbaji kutoka sauzi, Uganda , Congo"

Babu: "Lakini sisi hatukuwasikiliza"

Meneja: "Ndiooo. Lakini mngeweza kama mngetaka"

Babu; aka give up na kumwambia mkewe andika cheki uwape,,

Bibi akaandika akampa meneja.

Meneja anaangalia anaona sh. 50,000

Akashangaa na kusema. "VP mbona hamsini'"

Bibi akajibu "450,000 ya kulala na mimi"

Meneja akajibu; "Lakini sijalala"

Bibi :"ungeweza kama ungetaka"[emoji38][emoji38]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Jana nilikula bakuli 4 za maharage.Demu wangu akanipigia kunialika chakula cha jioni home kwao.Nilipofika akanikumbatia kwa bashasha vile hakuamini kama ningeenda,akasema"bby nina suprise kwako,fumba macho"nikafumba.Akanifunga kitambaa usoni kisha akaniongoza hadi kwenye kiti changu mezani.Kabla hajanifungua kitambaa cm yake ikaita chumbani,akaomba aende kupokea ila akanisisitiza nisifungue kitambaa,akaenda..Yale maharage nilokula yakaanza kunikoroga tumbo,likajaa gesi.Nikajibinua kwa kushoto nikapunguza gesi kidogo.Harufu ilikuwa mbaya nikatoa leso mfukoni nikapungapunga hewa kupunguza harufu,masikio yakiwa makini kusikiliza maongezi ya cm chumbani.Nikajibinua upande wa pili nikaachia makombora km matatu ya kimyakimya.Harufu ilikuwa mbaya zaidi ya kabej na maharage yalochacha!nikachukua leso nikapukutapukuta hewa.Mara cm ikakata huko chumbani,akaja,akaniulza"bby hujatoa kitambaa kwel?"kwa uso usio na hatia nikamjibu"hapana bby",akanifungua.Ghafla wageni 12 akiwemo baba na mamaake wameketi huku wameziba pua!!
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
MAPENZI NI MATAMU ILA ACHA KIHEREHERE..

Ama hakika mapenzi ni matamu sana ukimpata akupendaye mkashibana. Kumjali mpenzi wako ni jambo la msingi sana lakini ni vizuri kuepuka kuwa na kiherehe sana. Jamaa mmoja alijikuta taabani mara baada ya kumkurupukia mpenzi wake.

Jamaa mmoja alikuwa na demu wake ambaye alikuwa anamjali sana kwa kila kitu. Yule demu alikuwa kila anachotaka jamaa anatoa. Kwa ufupi jmaa alikuwa anamjali sana demu wake.

Siku moja kama kawaida jamaa aliamka asubuhi na kuchukua simu yake kisha akampigia mpenzi wake wa moyo.

Jamaa: Mambo baby umeamkaje?
Demu: Siko poa sana…
Jamaa: Nini mbaya mpenzi?
Demu: Nina mimba halafu sikupanga iwe sasa!
Jamaa: Khaaa! Mbona tulikuwa tunatumia kinga umepataje?
Demu: Kani nani kasema ya kwako?

Hivi navyooongea jamaa kakimbizwa Muhimbili kazimia kwa mshtuko! Kweli mapenzi ni matamu! Ungekuwa wewe ungefanyaje aisee?[emoji23][emoji23][emoji23]
Apo lazima uzime tu
 
[emoji23] Faida 3 za uvutaji wa sigara[emoji818]

FAIDA KUU TATU ZA SIGARA
1. Mvuta sigara hazeeki
2. Mvuta sigara haumwi na mbwa
3. Mvuta sigara nyumbani kwake haingii mwizi

UFAFANUZI

1. Hazeeki kwa sababu hufa mapema kwa kifua kikuu

2. Haumwi na mbwa kwa vile kifua na mapafu yanapooza na hulazimika kutembea na bakora

3. Nyumbani kwake haingii mwizi kwa kuwa inafika wakati ambapo halali:
atakohoa usiku kucha hivyo mwizi anajua yupo macho
kumbe kikohozi tu![emoji28][emoji28]
 
[emoji239][emoji239]
 

Attachments

  • _20170415_141214.JPG
    _20170415_141214.JPG
    74.5 KB · Views: 176
[emoji23] Kilichotokea nikiiwa namsaidia mtoto home work[emoji818]

Kusaidia Mtoto wa Nursery Homework ni Ngumu. Unamuuliza "Nina Pipi Tano, nikiwagawia Watoto Watatu, kila mmoja Pipi Mojamoja nabakiwa na ngapi? Anakwambia, "toa Kwanza nizione.."[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji117][emoji16] Sifa 10 za mwanaume ambaye kila binti anayetaka aolewe angependa aolewe naye!![emoji23][emoji116][emoji818]

SIFA 10 ZA MWANAUME AMBAYE KILA BINTI ANAETAKA KUOLEWA ANGEPENDA AOLEWE NAE.

1. Awe na pesa nyingi

2.Siyo lazima awe mzuri wa sura

3. Ajenge ukweni

4.Awe mpole

5.Asimuonee wivu mke wake

6.Awe mwenye upendo wa dhati

7.Asishike simu ya mke wake.

8.Akimkuta na mwanaume apite tu, akitaka kujua ni nani asubiri nyumbani

9.Awe anamskiliza mke wake kwa kika kitu.

10.Asipende mwanamke mwingine zaid yake

UKIMPATA MWANAUME MWENYE SIFA HIZO KAPIME DNA LAZIMA ATAKUWA NI BABA AKO.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji117][emoji16] Sifa 10 za mwanaume ambaye kila binti anayetaka aolewe angependa aolewe naye!![emoji23][emoji116][emoji818]

SIFA 10 ZA MWANAUME AMBAYE KILA BINTI ANAETAKA KUOLEWA ANGEPENDA AOLEWE NAE.

1. Awe na pesa nyingi

2.Siyo lazima awe mzuri wa sura

3. Ajenge ukweni

4.Awe mpole

5.Asimuonee wivu mke wake

6.Awe mwenye upendo wa dhati

7.Asishike simu ya mke wake.

8.Akimkuta na mwanaume apite tu, akitaka kujua ni nani asubiri nyumbani

9.Awe anamskiliza mke wake kwa kika kitu.

10.Asipende mwanamke mwingine zaid yake

UKIMPATA MWANAUME MWENYE SIFA HIZO KAPIME DNA LAZIMA ATAKUWA NI BABA AKO.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Jamaa mmoja akiwa na mtutu wa kivita maarufu kama AK47 alivamia kanisa moja la kiroho na kukuta watu wanafanya ibada. Akiwa ameuelekeza mtutu wake juu jamaa alianza kupaza sauti huku akielekea madhabahuni.

“Nani ni mtoto wa mungu hapa?” Jamaa alihoji kwa ubabe. “Nauliza hivi, nani ni mtoto wa mungu hapa ili nimpeleke sasa hivi kwa baba yake mbinguni!”

Waumini wote walikaa kimya na jamaa akaongeza mkwara kwa kufyatua risasi tatu kwenye paa la kanisa. Waumini wote wakapaza sauti, “ni mchungaji. Kila siku huwa anasema yeye ni mtoto wa mungu.”

Kwa upole na unyenyekevu mwingi mchungaji akajibu, “mbona mnanisaliti wapendwa? Nyote nyie mnajua kwamba mimi ni mtoto wa Githinji. Sasa ninahusianaje na huyo mungu!”

Chezea safari ya mbinguni wewe!!!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
[emoji23] Baada ya kumkuta mwanamme mwingine chumbani kwake na mke wake cheki huyu anachokifanya[emoji818]

NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi,
DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu
NAKUA: Hakuna kitu kama hicho
DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguo….

NAKUA kaingia ndani kamkuta mkewe kalala kitandani kajifunika shuka gubigubi hadi kichwani. Kaenda kwenye kabati kufungua mlango , akamkuta rafiki yake wa miaka mingi yuko uchi ndani ya kabati
NAKUA: Aise unajua we fala sana, we rafiki yangu miaka yote hiyo halafu unamtisha mwanangu eti wewe jini, hebu toka huko nenda kwenu kacheze michezo hiyo na mwanao.[emoji23][emoji23][emoji38]
 
[emoji125]
 

Attachments

  • _20170417_121647.JPG
    _20170417_121647.JPG
    67.2 KB · Views: 185
[emoji23] Huyu mwanamke ni noma cheki alichomwambia mme wake baada ya kumnunulia nguo za ndani[emoji818]

Mume kaingia duka la nguo na kamnunulia mke wake chupi dazeni moja zote za rangi nyeusi, akaenda kumzawadia. Mpenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote ni nyeusi si akaropoka.
MY HONEY: Sasa umeninunulia chupi zote nyeusi, sasa watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili,

Jamaa alifura akawa kama mbogo na hapo ndipo zogo kuu lilipoanza

MUME:Watu gani hao watakaokuambia unachupi moja, inamaana unawaonyesha kitumbua changu? Leo utanambia'
Ungekuwa wewe ungefanya nini?

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23] Angalia huyu mke wa mtu anavyojichanganya hadi kwa mme wake[emoji818]

MUME: "Mke wangu nasikia John katembea na wake za watu wooote hapa mtaani kasoro mmoja tu!"

MKE: "Mmmh! basi huyo aliebaki atakuwa MAMA MBILINGE KISIKI, maana yule mama ndo ANAJIFANYAGA MGUMU sanaaa.!!"

Je, huyu mama angekuwa mkeo ungekuwa na swali lingine la kumuuliza?

[emoji23][emoji3]
 
wavuta bangi walikua hawana kiberiti kwa ajili ya kuwashia bangi,basi wakamtuma mwenzao mmoja akaombe nyumba za jirani,jamaa kazunguka hatimaye akarudi palepale na kuwauliza *oy jaman naazma kiberiti* jamaa wakamjibu,*hata sisi kuna mtu tumemtuma akaombe hapa hatuna* bangi sio kiko.
Hahaha[emoji23][emoji23]bangi hatari
 
Back
Top Bottom