Mwalimu wa chekechea kawatoa wanafunzi wake nje..
Mwalimu:Angalieni juu, mnaona nini?
Wanafunzi:Mawinguuu!!!
Mwalimu:Vizuri, kingine je?
Wanafunzi:Hamna kingineee!!
Mwalimu:Je, Mungu mnamuona??
Wanafunzi:Hatumuonii
Mwalimu:Sasa tutaaminije?, me ninawaambia hakunaga Mungu.
Dogo mmoja akadakia,,,"Mwalimu, samahani kidogo!".
Mwalimu: "Bila samahani"
Dogo akatoka mbele...Anaanza kuwauliza wenzake,,,
Dogo:Angalieni kichwani kwa mwalimu, mnaona nin?
Wanafunzi:Nyweleee!!
Dogo:Vizuri, kingine je?
Wanafunzi:Hamnaaa!!!
Dogo:Mnaona akili??
Wanafunzi:Hatuiooniii
Dogo:Sasa tutaaminije?, mimi nawaambiaga hana akili huyu mwalimu.
Ile chekechea mpaka sasa imefungwa.