SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Nakumbuka kulikuwa na utaratibu barabarani kwenye mabasi makubwa ya masafa marefu yanayotoka mkoa mmoja hadi mwingine, askari wanaingia kukagua mabasi na moja ya mambo waliyokuwa wanaangalia ni kama basi limezidisha idadi ya abiria.
Kutokana na hulka ya Watanzania tulivyo, tulikuwa tunakaushia pale mabasi yalipokuwa yanazidisha watu wawili watatu, ambao wengi walikuwa wanakaa kwenye vigoda au hata chini katikati ya siti. Sasa hivi hili tatizo tulipofikia na tunapoelekea ni kubaya sana.
Juzijuzi nimepanda basi kulikuwa na abiria zaidi ya 10 waliokuwa wamesimama safari nzima. Kwa kuwa ni kama tumehalalisha hili suala, tunapoelekea unaweza kukata tiketi kwa bei halali ukiingia kwenye basi hauna uhakika wa siti kama ilivyo kwenye daladala na litaonekana kama jambo la kawaida na tutakuwa tumeshachelewa kulitatua.
Muundo na matarajio ya huduma katika usafiri wa mabasi makubwa ya masafa marefu hauna tofauti kubwa na usafiri wa ndege. Suala la "comfort" kwa abiria limezingatiwa sana. Inapofika hatua unasafiri umbali mrefu ila unajihisi kama uko ndani ya daladala ya Gongolamboto, hili ni tatizo kubwa.
Niliwahi kusema itafika kipindi hata kwenye safari za ndani za ndege, idadi ya abiria wanaopanda itaanza kuongezeka kuzidi inayotakiwa na huko pia abiria watakuwa wanasimama. Kipindi ndege inaruka au kutua, abiria mlio na siti zenu mtaambiwa msogee mshee siti na wenzenu na jinsi Watanzania tulivyo wakarimu tutafanya hivyo. Kama mtu anaweza kusimama masaa 4 katika basi atashindwa kusimama lisaa katika ndege?