Suala la Academic International School kudai ada ya muhula wakati huu halikubaliki, Serikali tunaomba muingilie kati

Ni kweli ila kwa wafanyakazi wao nao wapunguziwe mishahara? Nadhani wazazi walipe full ada tu.
 
Sidhani kama ni sahihi kulipa ada kipindi hiki ambacho wanafunzi hawasomi,shule itafute namna ya kujiendesha,unalipaje ada wakati huna uhakika watoto wanarudi lini shuleni
itafute namna?namna ipi,hembu weka hiyo namna hapa
 
Sidhani kama ni sahihi kulipa ada kipindi hiki ambacho wanafunzi hawasomi,shule itafute namna ya kujiendesha,unalipaje ada wakati huna uhakika watoto wanarudi lini shuleni
Hii si sahihi, ni wazi kuwa ipo siku shule zitafunguliwa tu. Wazazi walipe ada ili mambo mengine kwa watumishi wa hizo shule yaendelee. Uongozi wa shule utafidia tu!!
 
Mtoto ulimpeleka mwenyewe wala hukushauriana na serikali, sasa hivi unataka serikali iingilie kwenye maamuzi ulofanya mwenyewe!!!
Shule zina utaratibu wa kujiendesha, kama mna malalamiko kama wazazi basi shaurianeni na bodi ya shule muone cha kufanya.
 
itafute namna?namna ipi,hembu weka hiyo namna hapa
Hio ni kazi ya shule kuumiza kichwa,labda kwa ushauri ;kama wana mikopo waombe benki zisitishe makato kwa muda,watumie akiba ya shule kujiendesha,kama ni kodi waiombe serikali isitishe kwa muda,kama shule ina miradi mbadala ndio muda wa kuitumia nk nk
 
Kinachotakiwa kwa Sasa ni kulipia ada kidogo ambazo zitasaidia kuendesha shule na sio kulipa full. Logic ni simple kipindi hiki wanafunzi hawafundishwi kwa hiyo walipe kidogo kwa ajili ya assignment wanazotuma online. Tuchukulie mfano huu ugonjwa ukaenda kwa miaka miwili je tutaendelea kulipa ada?

Na je ukiisha kesho na shule zikarudi na kuna wanafunzi mfano form six walishamaliza ada je watalipa tena?

Kikubwa hapa Wizara husika itoe mwongozo ambao utafuatwa na shule zote.

Halafu wana JF mna balaa. Humu humu ndio wote tunamiliki vogue, tunaishi USA, tunamijengo Masaki nk. Leo kaja mtu anasomesha mtoto international mnamshauri ampeleke shule ya kata. Mmeshasahau majivuno yenu yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usilipe,simple as tht
Kwani atafukuzwa?.!
 

Hiyo shule ina walimu je unataka hao walimu walipwe na nini?

Kama huwezi kulipa peleka mtoto shule za kata.
 
Kwa nini ya vyumbani unayaleta sebuleni?
 
Hii si sahihi, ni wazi kuwa ipo siku shule zitafunguliwa tu. Wazazi walipe ada ili mambo mengine kwa watumishi wa hizo shule yaendelee. Uongozi wa shule utafidia tu!!
Serikali imefunga shule kwa muda usiojulikana,sasa utaendelea kulipa ada mpaka chanjo ipatikane?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…