Suala la Academic International School kudai ada ya muhula wakati huu halikubaliki, Serikali tunaomba muingilie kati

Kuna wanaoponda sana mara ni upumbavu kupeleka mtoto shule za binafsi hili mara lile unaweza ukawa uwezo wako wa kifikiri na kupambanua mambo ndo umefikia ukomo hapo. Hebu tujiulize wenye kuwaza hivyo je shule binafsi zinachukua idadi ya wanafunzi kiasi gani kwa nchi nzima ndo tuone kama bado serikali inaweza kuwaaccomodate hao wanafunzi wote. Hivi tumeshajiuliza kwanini hata serikali inaweka mwongozo kwa kima cha chini kwa sekta binafsi?
Mzazi anapoamua na kumpeleka mtoto shule binafsi haimaanishi kuwa ana pesa za kumwaga wengi humu tunajfahamu matokeo ya shule nyingi hasa hizi za kata kwa mantiki kwamba mzazi ambaye ameona umuhimu wa kujinyima ampeleke mwanae shule za binafsi anakubaliana na sharti la kuumizwa na wenye hizi shule.
Kwa baadhi ya members wamemuwakia mtoa mada kama vile sijui kajimwambafai vile.
Humu ndani kuna zaidi ya threads mbili zinazungumzia baadhi ya watamzania kufurahia amguko au mtu mwimgine hasa mwenye mafanikio haijalishi ni makubwa kiasi gani ila mzazi katoa lalamiko just from no where unaanza kumwita mpumbavu. Unafaidika nini ikiwa wanao wanasoma shule za kata tulia tu hiko ni jambo la kawaida . Hakuna jamii isiyo na watu wa daraja la juu kati na chini. Kubaliane tu na hali yako haisaidii kumtolea mwenzio pofu mtu hata kumfahamu humfahamu. Nawaza nimewakwaza ila ndo hivyo. Social stratification haikosekani ktk jamii yoyote ulimwenguni ila haimaanishi uadui.
 
Mimi nadhani ingependeza jiwe angesema tufunge na tuombe ili watu wasiojulikana wajulikane ili tuwaulize ni nani alim shoot Kamanda Tundu lisu

Kwaio Haya maombi ya covid 19 hayana maana kwangu kama hatutaanza na maombi ya kuwasakama watu wasiojulikana.

Mmenipata hapo lumumba? Over.

son of almighty God.
 
Capitalist system, unanipa huduma nakulipa. Hunipi huduma nasitisha malipo. Ningekuwa mzazi nisingetoa mia, it's give n take.
 
Tena hapo vocha juu yako mzazi....na bado unawalipa !! Kuna wazazi wengine ni mama lishe wanapenda watoto wao wasome shule nzuri na wao hali ngumu sasa hivi. Kingine ni wazazi wote wana smartphone?
 
Hizo ni mbwembwe zako! Hiyo hela ungeweka bank ningezaa kbs. Mtoto akipata ugonjwa ghafla akishindwa kusoma kwa mwaka au miaka 2,utajilaumu na kujuta kimoyo moyo au kwenda kbs shule kulalanika.....punguza sifa za kwenye keyboard.
Mimi nimelipa ada ya miaka miwili mbele.

Wewe ya mwaka mmoja tu unalialia hapa wakati shule za Magufuli zipo
 
Hahahaa...ndo maana mmewaambia siye tunaosomesha katani tuache wivu jamani
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walipe tu hakuna namna kama bado mwafundisha sisi huku mpk shule zifunguliwe kwa kweli tukutane mwisho wa agizo full burdaan
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujatumia busara mkuu, kumbuka hiyo shule ni biashara ya mtu. Na biashara kipindi hiki zimepata pigo kubwa, na ukumbuke pia wanahitaji nao kulipa mishahara.

Kumbuka, IF YOU ASK THE PRICE, YOU CAN NOT AFFORD IT

Wewe hizo shule sio class yako
Tatizo sio class tatizo ni value for money, hali ngumu sio kwao tu ni kwetu sote kuna watu wamefunga biashara, watu wamepoteza ajira hiki ni kipindi cha kufunga mkanda kwelikweli hili janga bado tunalo vya kutosha tu ukiwachekea mabepari unakufa na njaa quarantine
 
Unataka serikali ifanyaje? Suspend mikataba? Sheria hazijaenda quarantine ndugu yangu, au mliambiwa incase shule zimefungwa kwa emergency hamtalipa ada?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naona ni haki yao kudai ada, maana hata ukipangishwa nyumba miezi sita alafu ukasafiri miezi minne ukiwa ndani ya mkataba huwezi kusema hulipi kisa hujakaa kwa kuwa ulikua upo safari
ASA si kwa sababu vyombo vyako viko ndani na umefunga chumba,we leo aje kondakta akwambie lipa nauli ili hali gari hujapanda utakubali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakukua na utaratibu kwenye corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vema kulipa kwa kadri ya mkataba kuwa utalipa kiasi hiki January, March, July na August 2020!
Je kama kwa bahata mbaya Mtoto amekufa je? Maana hakuna tofauti ya Mtoto aliyekufa na ambae hayupo shuleni kwa mda huo, wote hawafundishwi kwa na wote hawatumii maji na wote hawali chakula cha hapo,na wote hawachafui mazingira ya shule,so why should I pay for

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi kwelikwei
 
Kwani mzazi analipa ada kwa sababu gani? Basi kama ni hivyo ufanyike utaratibu shule zipewe reimbursement toka serikalini. Mzazi analipia huduma anayopata mwanaye na si kulipia mshahara wa mfanyakazi huku mtoto akiwa hapati huduma yoyote. Kumbuka wazazi nao wanahangaika kutafuta pesa na kujinyima ili watoto wapate huduma kusudiwa. Ni heri kama hizi zingekuwa shule za wazazi na sio biashara binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…