Nyie Watanganyika mmeanza kuwehuka, huu muungano ulikuwa mzuri wakati Magu yupo kitini sasa Mungu kafanya yake mnaanza matusi .
Watanganyika ndio mliokuwa mnawaona wazanzibari wamechanganyikiwa wanapodai kutokukubali aina hii ya Muungano, hivi sasa nyinyi ndio mualalamikie wao kuwa wanawabagua.
Wazanzibari hawajapata kukubali kuungana na Tanganyika tangu hapo kabla. Kinachofanyika ni siasa za uchama na ufisadi wa kikundi cha wanasiasa mahasidi ndio wanaosababisha yote haya kutokea.
Kama mna hamu na kuuvunja muungano huu, wakataeni kwa makusudi na wala msisubiri kura, wakataeni kuwa hamtaki kufanyiwa maamuzi nao, kataeni siasa za kijinga zinazoanzisha chuki na kuwapata watu kama lukuvi na Gwajima, ambao wanahamasisha ubaguzi wa wazi zidi ya imani za watu. Wazanzibari hawakuanza wao, mamwehu wenzenu ndio walioanza haya na ndio maana wao wanalipiza. NYANI HAONI KUNDULE.
TANGANYIKA kwa jina la Jamhuri ya muungano wa TANZANIA kila siku inakataa kata kata kukubali baadhi ya mambo katika Mtangamano wa kikanda wa Afrika Mashariki. Mlikat\ kuhusu ardhi, mlikataa kuhusu viza ya pamoja ya utalii, mnakataa kuhusu Political federation pamoja na mambo kadhaa wa kadhaa ambayo nchi wanachama wengine kama Kenya na Uganda wanawaona ni kikwazo wa kufanikisha kupiga hatua nyengine mbele hadi nao wanaanza kuanzisha makubaliano baina yao ‘coalition of the willing (CoW)’ yaliyojumuisha Kenya, Rwanda na Uganda. Haya yote yametokea kwa sababu Tanganyika haikukubali na haitakubali kukubaliana na nchi wanachama wengine kuruhusu wasichokitaka kiwe cha wote. KWAHIYO ZANZIBAR KUKATAA MNACHOHITAJI SIO VIBAYA WALA SIO DHAMBI kama mnavyojitia hamanazo kuwasema vibaya na kuwapa majina mabaya na sifa zisizowahusu kwa kuwa hawataki kutangamana na watanganyika katika baadhi ya mambo. MUWE NA ADABU MAHASIDI WAKUBWA.
China juu ya kuwa na UTAWALA MMOJA na Hongkong, Makao pamoja na Taiwan lakini bado hawaachiwi wachina kutoka Bara kuingia tuu katika visiwa hivi watakavyo. Kuna utaratibu maalum wa kuingia kule visiwani kwa wachina kutoka bara. Watanganyika nyinyi mmeachiwa mnaingia mpaka kwa majahazi Mkokotoni kule, hamdaiwi hata passport na hii ni mara baada ya yule mkavirondo mwenzenu kuwapa nafasi hiyo.
Watanganyika mnazidi sifa na mnaona ni haki yenu kumiliki mkitakacho visiwani zanzibar kisa MUUNGANO. kwahilo msahau.
Askofu wenu atasema mpaka apapuke, na hata itokee serikali kuwapa hicho mtakacho wazanzibari wenyewe ndio wenye kuishi zanzibar hawatawaachia muvuruge muamala wao wa maisha kisa muungano na mtangamano wa kisiasa. Wazanzibari wananamna nyingi za kuwakataa na kukataa fitna zenu mnazozipanga na kuzitekeleza.
Hamshangai, mumeenza miaka mingi kutekeleza mipango na mikakati ya kuiritadisha zanzibar. Kaani kitaalam mujaribu kupitie na kutathmini mafanikio ya utekelezaji wa mikakati yenu. Linganisheni na rasilimali mnazozitumia, halafu jiulizeni je mmefanikiwa kwa kiasi gani.
Mnatumia nguvu nyingi na muda kudhoofisha watu ambao vuchwani mwao wanahangaika na kujitafutia rizki za halali wala hawana vita na nyinyi. Wazanzibari waliowengi wanaishi vyema bila ya kuwabagua watanganyika, iwe wakristu au waislamu. Ubaguzi unatokea na unaanza mara tuu baada ya nyinyi kuanza kuwatendea wasioyataka na kuyakubali, na jamii yoyote duniani ina mila na desturi zake. Ukiifanyia kinyume na matakwa yake itakubagua tuu kwasababu haikubali kufuata mnachowaingizia.
Mitaani wazanzibari wanaishi na wakristu vyema tuu, na hususan wakristu wetu waliozaliwa mkunazini, mbuzini, kwerekwe tunafahamiana lugha, tabia, utani na mengine mingi ila tunatofautiana imani. Tunaamiliana kwenye matendo kama biashara, Misibani, makazini na kwengineko. Nyinyi wakristu wakuletwa mje mjaze uwanja wa Aman kama juzi siku ya maazimisho na kuja kubadilisha mtazamo wa ukristu Zanzibar kwa wanaowapa misaada ya kiutu na kiimani kutoka makanisa ya ulaya, Amerika na Korea abadan hamtafahamu sura na mtazamo wa Wazanzibari dhidi ya ukristu katika iman zao. Mnachowafanyia ndio watakachokufanyieni.
HAMTAACHIWA MUVURUGE MTAKAVYO KWA SABABU ZA UTANZANIA NA MUUNGANO.
KILA JAMII INA TABIA, MILA NA DESTURI ZAKE, HATA IKIWA TUTAFANANA LUGHA NA IMANI, BADO TUTATOFAUTIANI MAADILI, MITAZAMO NA MENGINE MINGI.
NIMEELEZA FIKRA ZANGU BAADA YA KUSOMA FIKRA ZENU, NITAENDELEA KUSOMA FIKRA ZA WENGINE BILA YA CHUKI NA HASIRA. NILIPOTUMIA LUGHA ISIOPENDEZA MTANISAMEHE.
......... ILA HII NDIO DAWA YA NONGWA ZENU.