Mohamed, makala yako haijanitaabisha lakini nakiri imenifedhehesha.
1. Ansbert Ngurumo amezungumzia pande mbili, ya serikali akisema hakufanikiwa mawasiliano, kama lipo la kuulizwa kuhusu ziara, Serikali Ijibu. Pili, akaeleza mazungumzo na ' Mwanadiplomasia' wa Vatican, hakusema ni kweli au si kweli bali kunukuu. Sina sababu za kumtetea maoni yawe yake na yaheshimiwe kama yako.
Sidhani maoni yenu wawili yanawakilisha taasisi yoyote.
2. Umezungumzia DP kwa kutumia neno '' Waarabu' . Ni kweli ni Waarabu na sidhani kama hilo ni tusi.
Mbona Wazungu wanaitwa hivyo? Kuna ubaya gani kuwaita DP Waarabu kama tunavyoita wale Wazungu waliowekeza bandari ya Zbar!
3. Matatizo ya mikataba ya DP hayakuanzia Tanzania. Kuna nchi nyingi wanayo. '' Reactions' za Watanzania ni kutokana na mafunzo ya DP kwingine. Mkataba uliangaliwa kifungu kimoja hadi kingine na kubaini mapungufu yaliyohitaji ufafanuzi. Kwa mfano, nani anasaini upande wa pili. Ni muda gani wa mkataba, kwanini uhusu maeneo nje ya Bandari ya Dar es Salaam. Kwanini uifunge mikono serikali wakati kunapotokea fursa n.k.
Maoni ya wapinga mkataba yabiwe kwa hoja. Maoni iwe ya kuzua au ya kweli, ukweli ni hoja inajibiwa kwa hoja. Nimefuatilia majibu ya baadhi ya hoja kutoka makundi ya jamii nikasikitika .
Utetezi wa Rais ni Mwislam, wala si kujibu vifungu unatia simanzi. Nilidhani
Mohamed Said utakuwa tofauti , sijaiona.
Mohamed, waeleze wanaopinga mkataba, uzuri upo wapi! Upotofu wa vifungu wanavyonukuu upo wapi.
Ni wapi kumefanyiwa hila n.k. Ukijibu hayo kwa kutumia hoja za Wanaopinga kwa kifungu na mantiki utasaidia kuonyesha chuki inayojengwa dhidi ya '' Waarabu'' na DP. Bila hivyo, utakuwa unajenga chuki
Kwa bahati nzuri sana Mohamed Said umefanya kazi Bandari katika nafasi kubwa. Unaelewa abcd zake.
Tueleze kwa kina na vifungu, uzuri wa Mkataba ili tuoene chuki za Wanaopinga mkataba dhidi ya DP
Ukitueleza kwa mtindo rahisi kama uliopo katika bandiko lako, huitendei haki jamii yako na Taifa
4. Umeunganisha Chadema na Wakatoliki kwa ushirika wa hujuma. Sijui kama unajua ACT Wazalendo, CUF ya Lipumba walipinga Mkataba. Ulichokifanya ni 'selective amnesia' ( hukumbuki baadhi ya mambo kwa kuchagua).
Lakini pia Mohamed una ji-contradict. Leo unasema Waislam walikataa wakiunga mkono DP ukiwanasibisha na CCM. Ni hawa CCM iliyokuwa TANU unaowatuhumu kila siku kwa madhila dhidi ya Waislam.
Ni hawa CCM na Serikali yao wasiojibu hoja mlizopeleka 'Bungeni'. Ni hawa waliolea 'mfumo kristo' kwa miaka dahar kwa mujibu wa
Mohamed Said . Leo hao wamegeuka wema kwa Waislam!!! Leo Chadema ndio imebeba madhila na yote unayolalamikia! Lini Chadema iliwahi kuongoza nchi kwa sekunde 1.
Kumbuka kwamba Chadema ni Wapinzani , wana mitazamo yao, kuchomeka udini ni kiwango cha chini sana.
Kuna hoja zinaweza kujadiliwa, hili si mojawapo. Wenye Weledi bila kujali itikadi zao wanaiangalia nchi kwanza!
Katika karne hii bado tunatazamana kwa taswira za Wazzungu na Waarabu!
5. Ziara ya Pope Tanzania ilifanyika wakati wa A.H, Mwinyi. Kwanini hili lionekane ni jambo geni.
Huko ulikohamia kwa Mtikila mimi siendi kwasababu hoja ni bandiko lako na hilo ndilo tujadili.
Kwa mtazamo huu, nimeshauri uondoe bandiko lako si kwasababu linakera , la hasha! ni jepesi sana kwa mtu mwenye kalamu kubwa kama yako. Ninahofu sana asijetokea mpuuzi akashawishika kukuomba hiyo kalamu !
JokaKuu Pascal Mayalla Mag3