Suala la Covid19, nimegundua Wachina, Wazungu wana roho mbaya

Chanjo ya ebora uligundua wewe? je huko kwa wachina na wazungu kuna ebora?
 
HIV na Corona yote ni magonjwa ya kutengeneza maabara.

Inasikitisha namna binadamu alivyo muovu.
 
Covidol
Panadol
Sheladol
.......iol
Loh.....
Kwa hizi ulizoweka hapa sahau ndg,second wave hakuna hata inayofua dafu hapo.

Heri ungeniambia niende Tanzania oxygen limited niwape oda ya mtungi Wa oxygen nikae nao home.
 
Wewe ndo ulikuwa unalalamika kuwa shemeji yako hakuachii pesa ya matumizi. Unataka amwachie dada yako na wewe pia. Kawaoa nyote? Mwanaume huwezi dai utendewe mambo ya kipumbavu. Wewe unasumbuliwa na malaria unataka mzungu akutengenezee Chanjo. We una akili? Kwa nini sasa asikuoe na wewe? Unaumwa Corona unasema chanjo yake huiamini. Wakati huo dawa zilizojaa Hosp yako ni kutoka kwake. Panadol,Asprin,Alu n.k

Unataka akutengenezee dawa ya HIV wakati unaesumbuliwa ni wewe. ARV unatumia za kwake na condoms pia . Wewe unachoweza ni majungu na uvivu tu. Na kulia lia unalilia kufanyiwa mambo na mzungu. Huo upumbavu achaneni nao. Mjitegemee kiukweli. Siyo kuchagua sehemu ambazo mnaona mtapiga deal ndo mnadai mnashtukia Wazungu.
 
Kila siku ndio tunasemaga hicho hicho humu, ila kuna misukule ya wazungu huwa inakuja kukinga kifua..
 
Kwa nini unataka watu wengine wakutengenezee chanjo wewe?
 
Mliosoma syllabus za zamani za ujamaa chuki itakuuweni.
Ndui,ebola,zika, malaria nk mbona wamepambana nazo Hadi kuzizibiti na Hali wao sio waathirika.
Ubaguzi na chuki dhidi ya wazungu utakuuweni.
Syllabus ya biology form one wanasema kirusi hafi.
Usipanic bro. Naona unagombana na keyboard Kisa Mzungu utadhani uko kwenye payroll yake.

Usilete mambo ya panado kwenye mjadala wa chanjo ya kirusi. Sitaki asaidie ila najadili consistency ya mahusiano yake na matatizo ya Jamii ya mwanadamu. Kuna kipindi AIDS ilikuwa kama hii Pandemic. Huko Bukoba hadi Nyumba zinafungwa lakni hakukuwa na hamasa yoyote. Ila uzoefu umeonyesha Mzungu anahangaika na mambo yake kuliko ya wengine kama ulivyokuwa brainwashed kwa hizo panadol sijui ARV.

Kwa maana nyingine kwa roho hii ameonyesha yeye hicho unachodhani ni msaada kwa wafrika ni chambo tu na hana nia kihivyo ya kusaidia mwafrika
 
Kwa nini unataka watu wengine wakutengenezee chanjo wewe?
Sitaki watu wengine wanitengenezee chanjo.
Nataka uelewe ukiona Mzungu anapambana mwafrika apate nafuu flani usikurupuke, ujue tu anataka kuonekana mwema lakini hana huo wema kama anavyosifia na kuabudiwa kwa ARV,Panadol sijui Ndui.

Anajua kunafaida anapata na ingekuwa utu basi angepambana kwa level hizo hizo za pandemic ya corona.

Hiki ndicho nimejifunza. Sisi tumejisaidia Mkuu na tunapambana kwa njia zetu. Asilazimishe basi option zake ndio ziwe SI Unit ya utatuzi. Hata sisi tukikubakiana kujifukiza au Miti Shamba atuache, maana hata yeye chanzo zake wanabishana hakuna ambayo ni universal isiyokosoleka.
 
Anapambana kwakua anajua asipopambana kukutibu wewe utamuambukiza wakati anakuhitaji uendelee kumlindia rasilimali wakati akija kuzivuna azikute salama.
 
Sasa Kuna mtu aliyewazuia na nyinyi kutafuta hizo chanjo za hayo magonjwa yanayowasumbua? Au ndiyo ndugu llawama

Usome kwa utulivu.
Hapa anataka uelewe sio kila juhudi ya Mzungu na presha ya kutaka kumsaidia mwafrika huwa ni njema.anaweza kukusaidia 1% akakuaminisha ni 100% alafu yeye anajua 99% kabaki nayo ili akutumie baadae kwa Faida yake.

Hata hizo chanjo hujiulizi kwa nini hata Kabla corona haijafika afrika Bill gate na mkewe anatabiri vifo hadi watu washindwe kuzikana afrika ili kutafuta uhalali wa kuleta chanjo yake huku. Sasa uhalaka huo na utabiri uliofeli ulisukumwa kwa sema au kuwafanya waafrika specimen za kutestia chanjo
 
Of course kuna geopolitics na soft power politics.

Lakini pia, Waafrika wengi ni watu wa kulalamika tu.

Wakipewa chanjo, watalalamika wamepewa chanjo na mabeberu, mabeberu wanataka kuwaua wachukue mali za Afrika.

Wasipopewa chanjo, watalalamika mabeberu wana chanjo, lakini hawawapi Waafrika.

Ili mradi watu walalamike tu, kwa lolote lile litakalofanyika, au litakalokosa kufanyika.
 
Asante sana, umenena vyema.
 
Sasa mkuu unataka akuangaikie wewe kama nani yake!!!, wamefanya sehemu yao ingawa wakati mwingine pia wana maslahi yao. Wewe mwenye tatizo umefanya nini kulitatua? Mangapi wametusaidia na kama kutumaliza tungeishaisha. Leo Stone kwa maslahi anayojua yeye anasema chanjo haiaminiki na wakati imethibitishwa na shirika la afya duniani na imeonyesha ufanisi wa juu huko ilikotumika. Ni nani anayepambana na HIV/AIDS, TB, Malaria, Ukoma na magonjwa lukuki tuliyonayo na ambayo mengine huko kwao imebaki historia tu.
 
Hapa tunapiga stori au una ushahidi au umefanya kautafiti kidogo utuwekee hicho ulichogundua. Kuanza mjadala kwa kutumia tu hisia zako bila takwimu kwa haya msuala ya kisayansi si sahihi sana.
 
Ndo unapoonesha upumbavu. Yaani pandemic iwe Bukoba halafu ahangaike mzungu kukusaidia. We una akili? Wewe n mkeo au mumeo au na familia yako mnaumwa kaswende halafu jirani ambaye haumwi unamlaumu kwa nini hakutengenezei dawa. Wewe una akili?

Covid ni ugonjwa ambao upo Duniani.na dunia inachangamana so watu wanahangaika na Ugonjwa wa Dunia kuliko ambao upo kwako peke yako. We we unaweza laumu kuwa Jirani yako hampatii chakula mumeo hivyo mumeo anakosa nguvu za kiume. So unataka jirani ambaye yeye ana mke wake na watoto amsaidie mumeo au aisaidie familia yako. Huo ni upumbavu.
😁😁😁😁😁😁
 
Mbona wewe ndo una roho mbaya mkuu.yani tatizo la kwao mimi ndo nikupambanie wakati wote tupo sawa?
Ndo nyie mkifulia mna raumu ndugu kwa upumbavu wenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…