Ichwampaka
Senior Member
- Nov 19, 2018
- 145
- 118
Waziri Mhe. Makamba ameongea akaeleweka vyema kabisa. Wakaja wabongo na ''a garbled story'' na kuzua mtafaruku mkubwa. Nilichokiona watu wengi uwezo wao wa kusikia na kuelewa ni mdogo sana; na kuna watu wengi wameenda shule ila uwezo wao wa kuchambua mambo ni mdogo sana. Makamba mbunge wa miaka mingi awe hajaona cranes za kunyanyua uzito wa tani 26?
Kwa nafasi yake, weledi na uzoefu wake kwanini usijione kuwa wewe ndio labda hujamuelewa Mhe. Makamba? Waziri mwenye staha kama yake anapotoa taarifa ya jambo nyeti kama hilo lazima ajiandae vyema with all the material facts on the ground.
Ukweli ni kuwa kreni la kunyanyua hilo geti la maji pindi bwawa likijaa ni sehemu ya ujenzi wa hilo bwawa. Kreni hizo zitajengwa hapo kwa kudumu (permanently). Alichokisema Mhe.
Makamba kuwa nchini hazipo, ni kuwa ''duka'' linalouza hizo kreni MPYA (zenye uzito wa tani 26 ) hapa nchini halipo lazima ziagizwe nje. Wangekuwa wanafunga za mitumba ingekuwa haina shida labda zingeweza kutafutwa na kupatikana hapa nchini ili turudi tena kwa Dowans na Richmond kuhusu mitumba.
Watu wamerusha mapicha ya movable cranes kama hawana akili nzuri.