Suala la GSM kudhamini baadhi ya timu za Ligi Kuu liangaliwe upya, linajenga mazingira hasi na kupunguza ushindani katika ligi

Suala la GSM kudhamini baadhi ya timu za Ligi Kuu liangaliwe upya, linajenga mazingira hasi na kupunguza ushindani katika ligi

Gsm ni shareholder wa team gani?
Simba ndio ilikua timu ya kwanza kutoka hadharani na kupinga wakati GSM alipotaka kudhamini timu zote zinazoshiriki NBC premier league.

Wakati wakati uo Azam anadhamini Ligi nzima na wanapokea mgao wa Azam Kila mwezi.
Timu zinahitaji udhamini ili zipunguze makali ya gharama za kuziendesha.

Baadhi ya vilabu viliona Simba ni wapuuzi, zikajiongeza na kuitumia fursa ya udhamini wa GSM.

Kama Simba ilikamiwa na ivyo vilabu vyenye udhamini wa GSM kwanini na wao Simba wasiwakazie Yanga ambao Wana dhaminiwa na GSM?
 
Jana nimeona kwenye kombe la xecafa singida Black stars wamevaa jezi zenye nembo ya GSM, huyo GSM ndio mdhamini wa Yangq, lakini timu kama Coastal Union, Namungo zina udhamini kama huo.

Kwa mazingira ya kibongo hili jambo lina ukakasi sana.

Kwa nchi zilizoendelea ambazo zinajali professionalism hili suala halina shida kabisa.

Lakini hapa kwetu hao wanaodhaminiwa wana mikakati mingi dhidi ya timu hasimu na Yanga hasa Simba.

Msimu ulioisha timu zilizovaa jezi za GSm ziliikazia sana Simba, mfano Namungo na Singida na hata Coastal kama sio bao la Onana dakika za mwisho ingekula kwetu.

Hatujui hizi timu kwenye udhamini wao zimewekeana terms gani pindi zikicheza na Simba.

Simba imesajili vizuri sana msimu huu lkn ninahofia tunaweza kuvurugana kutokana na mipango na mikakati michafu iliyopo kwenye udhamini.

Kama Mp dewji akiingia naye kudhamini baadhi ya timu itakuwaje.

TFF waliangalie hili jambo ama uongozi wa Simba uliangalie hili jambo vinginevyo hawa nzi wa kijani watachukua ubingwa tena kwa hila.

Ligi ya bongo inachezwa sana nje kuliko ndani, usipokuwa makini nje umeliwa.
Ficha ujinga wako. Babra hakushinda kuizuia GSM kudhamini ligi nzima, alishinda Simba isiweke nembo za gsm kwenye matambala yake. Kwa kuwa gsm alitaka timu zote zimtangaze simba ikagoma, hivyo deal likafa maana haitakuwa ligi tena.



Sasa pata shule hapa

Tuhuma zilizopo, kwamba hakuna fair competition katika ligi ya Tanzania sababu GSM anafadhili (sponsors) clubs nyingi tanzania hazina mashiko, ni kowango cha juu cha ujinga. Zinatajwa:-

1. Yanga
2. Coastal
3. Singida
4. Pamba
5. Namungo.
6.


Haya tunaijibu kwa kuiangalia Umbro ndani ya EPL ligi kubwa duniani.

Umbro sponsored Teams in EPL

1. West Ham United.
2. Ipswich Town FC.
3. Brentford FC.
4. Hearts FC.
5. AFC Bournemouth.
6. Huddersfield Town.
7. Luton Town.

Kwa majibu haya, tuendelee na mjadala au tuufunge?

Simba wekezeni kwa kusajili wachezaji wazuri. Hoja mnazoleta ni utoto mtupu na ishara ya kushindwa mashindano. Mlizoea kuzifunga timu ambazo hazina hata nauli, wamepata wafadhili, wanasafiri, wanalala hotel, wanakula, wanakunywa, wanalipa mishahara, halafu nyie mnatamani wapokonywe ufadhili huo warudi nyuma?


Kama mnadhani ni rahisi, mwambieni Mo aaxhe kutoa mikopo umiza afadhili timu zote
zilizobaki halafu mje tushindane
 
Back
Top Bottom