Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,156
Leo tena jamii ya Watanzania wameshusha pumzi kwa mara nyingine baada ya kusikia Mashehe wa uamsho kuachiliwa huru.
Kuna maoni mengi sana kwa watu. Mengi ya maoni hayo pamoja na kupongeza kitendo hicho wameenda mbali kwamba serikali iwalipe fidia. Hili limekuwa kubwa zaidi.
Wanasiasa na wanaharakati walilipigia kelele kwa muda mrefu Sasa baada ya kuachiliwa wamelipokea tena kwa namna nyingine.
Sio mjuzi wa sheria lakini naamini serikali walikuwa na sababu za msingi kuwashikilia hawa Mashekhe.
Tunapoanza kupiga kelele kuwa wakadai fidia mahakamani nadhani tungewapa muda kwanza. Wale Mashekhe naamini sio watu wa kusemewa na kuelekezwa kila kitu.
Wanao uwezo wa kujisimamia na kuamua kwa busara zao baada ya kusikiliza nafsi zao juu ya tuhuma walizoshutumiwa nazo.
Kuondoa shitaka mahakamani baada ya muda mrefu hivyo Mimi na wewe tunaweza tusijue kwa undani sababu iliyoifanya serikali kufikia uamuzi huo.
Tusije mtaani na kuwatakatifuza wakaonekana kana kwamba walikuwa mahabusu kwa kosa la kusingiziwa au kuonewa
Miaka tisa ni mingi sana kumfanya mtu ajue alipokosea na kujutia makosa yake na akawa tayari kujirudi kabisa.
Moja ya Mashekhe walioachiliwa amekiri kwamba wamejifunza mengi na kifungu kilichotumika kuwaweka huru kinampa mamlaka DPP kuwashitaki tena kwa kosa lilelile la awali endapo watatenda kosa lolote linaloelekeana na kosa walilokuwa wameshitakiwa nalo.
Ni mapema sana kuanza kuona Kama walionewa na kusingiziwa makosa hayo waliyokuwa nayo. Tusitumie muda na nguvu nyingi kutaka jamii iwaone watakatifu.
Si kila shitaka linaloondolewa mahakamani linakuwa limekosa ushahidi, mengine huondolewa kwa manufaa ya umma hasa linapooneka kutokuwa na madhara tena kwa wakati huo.
Lakini pia tufahamu kuwa hawa walishitakiwa kwa kosa la ugaidi. Kwa serikali makini si rahisi sana kufikia hatua ya kutoa hukumu kwa watu wake kwa kosa Kama hilo hasa ukizingatia ugaidi ni tishio la dunia.
Hapa lazima kuna technicalities zimechezwa ili mzani ubalance kati ya serikali na waliokuwa watuhumiwa.
Tumshukuru Mungu hili swala limefika mwisho maana huku nje presha ilishaanza kuwa kubwa pia hivyo hatujui hii presha na kelele ya nje ingetufikisha wapi.
Lakini pia tumuombe Mungu hayo yaliyokuwa yanaendelea kipindi kile wanakamatwa yasitokee tena. Tuishi kwa amani, upendo na utulivu.