Suala la kuachiwa Mashehe wa Uamsho ni vema wanasiasa wakaliacha kando

Kwa hiyo walikuwa kweli magaidi?.
 
Mbona ushahidi atukupeleka wakafungwa?
 
Wale wahuni walioiba sacrament mbagala walikuwa uamsho ?
 
Mama Samia hapa kahamua kucheza kamari ni either imlipe au isimlipe.... hawa wanaweza kuendelea na hayo mambo au wasiendelee... hakuna anayejua mioyo yao.

Hawa ni magaidi hata Samia mweyewe anajua hilo na dawa ya magaidi huwa ni kuwekwa kizuizini hadi kifo au kutwangwa risasi za kichwa kama majambazi.....

Tumuombe Mungu hawa Magaidi wasianze tena na hali iendelee kuwa shwari.
 

Una ushahidi hao ni magaidi?
Je kuna sehemu wamelipua?

Tunaomba ushahidi
 
Hivi kudai nchi yao iliyoporwa ndio ugaidi ?
 
Hivi wanaozungumzia ugaidi wanaujua kweli ugaidi?
 
Miaka 9 ya Masheikh hao korokoroni, tumeshuhudia Zanzibar yenye Amani. Hatukusikia Kanisa Wala msikiti uliochomwa . Hatukusikia pia Suala la mapadre kutekwa Wala kuuawa.
Siungi mkono suala la wao kukaa rumande miaka yote hiyo bila kuhukumiwa. Hata hivyo, siungi mkono wao kuachiwa kinyemela.
 
Ndugu umeandika cha maana sana. Shukran
 
Hawa siyo mashehe bali ni watuhumiwa wa ugaidi!! Hawakuwa wamekàmatwa kwa ushehe wao bali walikamatwa kwa utuhumiwa wao!!! Vinginevyo mashehe wote wangekuwa wamekamatwa !!!
Mbona masheikh wanakamatwa wengi tu unadhani wamekatwa hao wazanzibari tu?
 
1. Usinifanye nifikiri kuwa unaandika haya bila kuwa na ufahamu wa kutosha namna serikali za kidunia hususani za Ki - Afrika na hususani ya Tanzania chini ya CCM inavyofanya kazi yake ili kujihakikishia inabaki madarakani...

2. Usinifanye nifikiri kuwa hujui kuwa serikali hii chini ya CCM inawatengenezea kesi mbaya, za makosa yasiyo na dhamana watu wote wanaoikosoa kwa ukali na uwazi. Hii ilikuwa mbaya zaidi wakati wa uongozi wa Mwendazake Magufuli kama Rais. Mfano dhahiri ni aina ya viongozi kama Sabaya (aliyekuwa DC wa Hai - Kilimanjaro) na Paulo Makonda (aliyekuwa RC - DSM)

3. Usinifanye niamini kuwa hujui kuwa kuna watu mpaka leo wako mahabusu au jela kwa kesi za namna hii hii, za kubumba kwa watu kutumia mamlaka yao ya kiutawala kuonea na kuwanyanyasa watu na kuwanyima haki zao...

4. Usinifanye niamini kuwa hata hujui kwamba, baadhi ya wakosoaji dhidi ya serikali ya Tanzania na viongozi wake chini ya CCM ambao walishindikana kushitakika mahakamani kwa kubambikizuwa makosa/kesi mbaya, aidha waliteswa na kuuwawa/kupotezwa na wengine kwa kutonywa na watu wema ndani ya serikali hiyohiyo walikimbia nchi na wanaishi uhamishoni nje ya nchi mpaka sasa...!

KWA HIYO;

1. Kwanini wewe unataka wanasiasa wasiseme na kukemea dhambi na tabia hii mbaya toka kwa baadhi ya viongozi/watawala? Wakiacha kufanya hivi, nani apaze sauti kukemea tabia na maovu haya toka kwa watawala waovu hawa...? Je, una maslahi na haya maovu wewe?

2. Kuna maslahi gani ya nchi kutoka kwenye kesi hii iliyowatesa watu wasio na hatia kwa takribani miaka 9 wakiwa gerezani...??

3. Hakuna sababu wala kosa lolote la ugaidi dhidi ya watu hawa (mashekhe) zaidi tu ya kwamba walikuwa na wataendelea kuukosoa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hilo ndilo kosa lao na CCM hawataki na wasingependa mtu alete chokochoko kwenye jambo hili kwa sababu ndiyo uhai wa CCM na serikali yao ulipo. Kujaribu kuukosoa muungano huu haramu ni kutafuta kesi yq ugaidi tu...!!

4. Watu wengine wanasema eti ooh, walisababisha watu kuanza kuuana kwa tundikali nk nk. Sasa mtu unashindwa kuelewa, kwamba, kama ndivyo kwanini walioua ndiyo wasikamatwe na kushitakiwa? Tangu lini kesi ya kuua inageuka kuwa kesi ya ugaidi...??

HAPANA, HAPANA... Uovu huu na kukiukwa kwa haki za watu kwa namna hii lazima kupaziwe sauti popote na kila mtu; kwenye majukwaa ya kisiasa na wanasiasa, makanisani na wachungaji na maaskofu; misikitini na maimamu na mashekhe; wanaharakati na vikundi vya kutetea haki za binadamu.....wote wapaze sauti zao kuupinga uovu...

IMEANDIKWA; "....mpingeni shetani, naye atawakimbia..."

Lazima shetani ----- chanzo cha uovu, kitovu cha uovu apingwe kwa nguvu zote....!!
 
Wajaribu kuomba fidia kama wanataka kumtafutia mama wakati mgumu kwa maamuzi yake ya kuwatoa.

Uamsho ni tatizo la CCM, serikali ya Zanzibar na pro unionists; na wasidhani wazanzibari wote wamepokea kwa shangwe kutoka kwa uamsho hao watu walikuwa wanatengeneza divisions huko visiwani.

As far as bara is concerned can we afford a president anayeweza kuwa influenced by people outside the system so easily? Only in Tanzania, hakuna nchi nyingine duniani civil service yao itakubali.
 

..naipinga hoja yako.

..hawa mashekhe wamekaa kizuizini kwa miaka 9.

..yaani ni sawa na mtu aliyepatikana na hatia na kufungwa miaka 18.

..binafsi sidhani kama serikali iliogopa kuwafunga mashekhe kwa hofu kwamba kutaibuka makundi mabaya.

..badala yake naona kitendo cha serikali kuwashikilia mashekhe bila ushahidi kwa muda mrefu ndio kingesababisha malalamiko na hatimaye makundi yenye chuki.

..Mashehe walipwe FIDIA kutokana na uzembe wa Polisi na DPP.
 
Mie humu ndani naona kuna watu walisahau kuhusu mahakama ya mkazi ambayo walikua wana lazimisha itambulike iwe ndani ya serikali.


Haswa kipindi cha kikwete wanapenda wao waonekane ndio binadamu wengine hakuna kabisaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…