changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Tuzifahamu baadhi ya makampuni yanayomiliki timu zaidi ya moja duniani
1) The City Football club (CFG)
Hawa jamaa wanamiliki timu 13 ambazo ni
- Yokohama F. Marinos (Japan)
-Montevideo City Torque (Uruguay)
-Girona (Spain)
-Mumbai City (India)
-Sichuan Jiuniu (China)
2)New City Capital and Pacific Media Group
Hawa wanamiliki timu 8
3) Red Bull
Wana miliki timu 4
4) King power international
5) Eagle Football Holdings
6) INEOS sports group
Case 1
Kulingana na list inaonesha ni sahihi kampuni au mtu mmoja kumiliki timu zaidi ya moja lakini sio katika taifa moja (ligi moja). Labda kama wajuzi wengine wanaweza kutoa mifano ya timu zinazotokea nchi moja kumilikiwa na kampuni moja au mtu mmoja basi anaweza kuniweka sawa katika hili.
Case 2
Upande wa kampuni au mtu mmoja kumiliki timu huku ikidhamini timu ndani ya ligi moja hapa nimeona case moja pekee ambapo INOES ambao wanamiliki Manchester united ni mmoja wa wadhamini wa Tottenham Hotspur. Hapa wajuzi wengine mnaweza kutoa mifano ya mazingira kama hayo kama yapo makampuni mengineyo yaliyofanya hivyo.
Case 3
Kudhamini timu zaidi ya moja ( main sponsor) katika timu zinazoshiriki ligi moja.
Mdhamini mkuu ndiye anayeonekana mbele ya jezi, hapa kama tuna kumbukumbu hapo awali Simba na Yanga walikuwa na mdhamini mmoja ambaye ni sportspesa. Hili ni wazi kuwa hakuna uvunjifu wa sheria kampuni moja kudhamini timu zaidi ya moja.
Kwa wanaofuatilia soka la uingereza watakumbuka msimu wa 2018/2019 ambapo timu tano za championship zilidhaminiwa na kampuni moja ya online casino inayoitwa 32Red. Timu hizo zilikuwa ni Leeds, Aston villa, Derby, Preston na Middlesbrough hivyo hakuna kosa kisheria kwa kampuni moja kuwa mdhamini mkuu wa klabu zaidi ya moja wanaoshiriki michuano ya ligi moja.
Sasa tuje kwenye soka letu hasa kwenye swala zima linalopigiwa kelele na watu wengi hasa mashabiki wasiokuwa wa Yanga kuhusiana na GSM.
Je GSM ni mdhamini au mmiliki wa Yanga?
GSM ni muendeshaji wa shughuli zote zinazoihusu timu ya Yanga, ni kama kampuni inayowekeza katika timu ya Yanga kinyemela (sio rasmi) kipindi ambacho mfumo wa mabadiliko haujakamilika.
Ili kuitendea haki soka letu, na kuiheshimu ligi yetu kuna haja ya TFF na bodi ya ligi kuangalia swala zima la udhamini wa GSM kwa timu nyingi kiasi hiki katika msimu ujao, ni bora hata ingekuwa ni timu mbili angalau.
Siwezi kusema kama kuna upangaji wa matokeo ila ifikie wakati ligi yetu iwe katika weledi na kuondoa mazingira yakufikirika na mashaka kama ilivyo sasa.
Kwasasa wadau wengi wa soka wanaamini kuwa Yanga ikicheza na timu inayo dhaminiwa na GSM basi ni mechi ya mipango hiyo.
Kuna umuhimu wa wadau wa soka kutoa credit ya ubora wa Yanga kupitia mazingira fair kabisa pasipo kuwa na mashaka ya namna yoyote ile, hii itaipa timu hadhi yake. Pia kama kuna ukweli juu ya upangaji wa matokeo basi hilo jambo halitakuwa na afya kwa timu kwa mashindano ya kimataifa.
1) The City Football club (CFG)
Hawa jamaa wanamiliki timu 13 ambazo ni
- Man city ( Eng)
- New York City fc (USA)
- Yokohama F. Marinos (Japan)
-Montevideo City Torque (Uruguay)
-Girona (Spain)
-Mumbai City (India)
-Sichuan Jiuniu (China)
- Lommel (Belgium)
- Troyes (France)
- Palermo (Italy)
- Bahia (Brazil)
- Club Bolivar (Bolivia)
2)New City Capital and Pacific Media Group
Hawa wanamiliki timu 8
- Barnsley (England)
- Thun (Switzerland)
- Oostende (Belgium)
- Nancy (France)
- Esbjerg (Denmark)
- Den Bosch (Netherlands)
- Kaiserslautern (Germany)
3) Red Bull
Wana miliki timu 4
- RB Leipzig (Germany)
- New York Red Bulls (US)
- RB Bragantino (Brazil)
4) King power international
- Leicester City ( England)
- Leuven (Belgium)
5) Eagle Football Holdings
- Crystal Palace (England)
- Olympique Lyonnais (France)
- Botafogo (Brazil)
- Molenbeek (Belgium)
- Florida (USA
6) INEOS sports group
- Manchester united (England)
- Nice (France)
- FC Lausanne-Sport (Switzerland)