holy spirit
JF-Expert Member
- Nov 30, 2020
- 856
- 1,376
Habari za jioni wakuu
Napenda kuwapa taarifa kuwa sikopeshi mwanamke yoyote hela yangu tena. Kusema kweli sijawahi kukutana na shida ya kurudishiwa hela yangu kutoka kwa mwanaume mwenzangu (niliowakopesha mimi) ila kwa wanawake yamenifika kooni. Hadi uwe mkali ndo upewe hela yako.
Nimekopesha kama wanawake sita hivi kwa kujipa moyo huyu atakuwa tofauti. Huyu ananisumbua kulipa akija huyu najifariji kwamba wanawake wote hawafanani tabia natoa tena.
Kwa hawa niliokutana nao mimi nimeona katabia fulani common, unapimwa kwanza akuone utasikia anasema "na wewe nae mwanaume mzima unadai hadi hiyo jamani".
Hii ni dalili kwamba anayo ila kwa kuwa wewe ni mwanaume anaona uzito kurudisha.
Wanawake wenye hii tabia badilikeni bwana, hata sisi wanaume ni binadamu kama nyie tunafanya kazi za kutuchosha akili na mwili, vi hela vyetu tunavyopata ndio vipoozeo.
Pia, siku nyingine unaweza kuwa na shida genuine kabisa umekwama niko kwenye nafasi ya kukusaidia nikaishia tu kukwambia Niko vibaya.