jinsia ya kike ni wa kuwavumilia na kuwasaidia tu. binafsi haikuwa kumkopesha, kuna dada mmoja nadhani kwao alisoma peke yake na akawa tegemeo, mama na baba walishafariki hivyo ni yatima fulani na rundo la mzigo. nilimwonea huruma nikawa naye karibu. nilimpambania kama mdogo wangu, aliolewa na bado akaniona kama mtu wa muhimu kuliko wote ukiondoa mume wake. kumbe mimi sijui, amefanikiwa amepata cheo kikubwa, mwenzangu akawa anatafuta namna gani atanishukuru. awali nilijua utani tu kwa sababu hatujazidiana miaka mingi, though mi namwona kama mdogo wangu na nimeokoka anajua siwezi kuzini. alikuja kufunguka siku moja kwamba anatamani anipe zawadi, ipi? kumbe ya uzinzi, mimi nina mke na watoto anawajua. akahamishwa mkoa, nikaenda kibiashara kwenye mkoa wake, akajua nipo kwenye hotel fulani, aliuliza hadi nikaona anagonga chumbani kwangu, nilifungua tukakaaa tukaongea na hatukufanya kitu, hata baada ya kujibaraguzi mara oohh mi karibu naondoka, mara sijui nataka kurudi nyumbani nikamwambia mdogo wangu wewe unajua mimi nimeokoka, siwezi kuzini pamoja na kwamba nakupenda wewe kama mdogo wangu na upo karibu mno na mimi na ninajua unanipenda, tafadhali tuheshimiane ili mimi nisigombane na Mungu na wewe usigombane na mumeo, mumeo akikuacha mimi sitakuoa, pia mimi nikizini na wewe nitaingia kwenye mgogoro na Mungu utakaonigarimu, jambo ambalo sipo tayari. kwa msimamo wangu ule ndani ya miaka 5, sijawahi kuzini naye.
kitu nilichojiuliza, kwahiyo aliamini akizini na mimi ndio atakuwa amecompensate yale yoote niliyomsaidia maishani? na mumewe ni mtu wa maana tu Phd holder kabisa na wana maisha tu siku hizi wala hakuwa anahitaji pesa, ila penzi langu. shindwa shetani kwa Jina la Yesu.