Suala la kuwakopesha hela wanawake linaharibu urafiki/ukaribu

Suala la kuwakopesha hela wanawake linaharibu urafiki/ukaribu

Wanatisha kama nini
Najua wewe unaweka na riba kabisa wakati wa kurudisha uteni na utwenti 🤣, huna pigo hizo, bana ila sijichanganyi 😂😂 (joking Mis R)
 
Najua wewe unaweka na riba kabisa wakati wa kurudisha uteni na utwenti 🤣, huna pigo hizo, bana ila sijichanganyi 😂😂 (joking Mis R)
Yaani mimi nafanya mara 5 ya ile ulonipa😂
 
jinsia ya kike ni wa kuwavumilia na kuwasaidia tu. binafsi haikuwa kumkopesha, kuna dada mmoja nadhani kwao alisoma peke yake na akawa tegemeo, mama na baba walishafariki hivyo ni yatima fulani na rundo la mzigo. nilimwonea huruma nikawa naye karibu. nilimpambania kama mdogo wangu, aliolewa na bado akaniona kama mtu wa muhimu kuliko wote ukiondoa mume wake. kumbe mimi sijui, amefanikiwa amepata cheo kikubwa, mwenzangu akawa anatafuta namna gani atanishukuru. awali nilijua utani tu kwa sababu hatujazidiana miaka mingi, though mi namwona kama mdogo wangu na nimeokoka anajua siwezi kuzini. alikuja kufunguka siku moja kwamba anatamani anipe zawadi, ipi? kumbe ya uzinzi, mimi nina mke na watoto anawajua. akahamishwa mkoa, nikaenda kibiashara kwenye mkoa wake, akajua nipo kwenye hotel fulani, aliuliza hadi nikaona anagonga chumbani kwangu, nilifungua tukakaaa tukaongea na hatukufanya kitu, hata baada ya kujibaraguzi mara oohh mi karibu naondoka, mara sijui nataka kurudi nyumbani nikamwambia mdogo wangu wewe unajua mimi nimeokoka, siwezi kuzini pamoja na kwamba nakupenda wewe kama mdogo wangu na upo karibu mno na mimi na ninajua unanipenda, tafadhali tuheshimiane ili mimi nisigombane na Mungu na wewe usigombane na mumeo, mumeo akikuacha mimi sitakuoa, pia mimi nikizini na wewe nitaingia kwenye mgogoro na Mungu utakaonigarimu, jambo ambalo sipo tayari. kwa msimamo wangu ule ndani ya miaka 5, sijawahi kuzini naye.

kitu nilichojiuliza, kwahiyo aliamini akizini na mimi ndio atakuwa amecompensate yale yoote niliyomsaidia maishani? na mumewe ni mtu wa maana tu Phd holder kabisa na wana maisha tu siku hizi wala hakuwa anahitaji pesa, ila penzi langu. shindwa shetani kwa Jina la Yesu.
Baada ya msimamo wako hakuendelea kujileta?
 
Wanawake sijui wanatuona sisi wote ni matako zao, mwingine eti aliniambia, sijawahi kula pesa yako hata siku moja. Nikamwangaliaaa, sasa sijui alikuwa anafikiri mi ni muha
Ila wao ukiwaomba wakukopeshe mbususu zao wananuna hao 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mkuu jana kuna ex kanicheki, hello xxxx nina shida, nikajua hii ni hela nikamjibu shida ni za watu wote, akacheka kwa emoji halafu akakaa kimya namimi nikakaa kimya, akanitext tena nina shida nikamwambia nambie lkn isiwe ya hela , akajibu ni ya hela ,nikamjibu siwezi kukukopesha akajibu kwann, nikamwambia siwezi tu, akanijibu nakopa kwa riba, nikamjibu nenda microfinance wanakopesha misikopeshi, akajibu yuko mbali na home, nikamwambia aombee baba au mama ake akope kwa niaba yake akasema hataki kwao wajue ila anataka alipie ada ya mtihani next weeks wanatakiwa kufanya ,nikamwambia mmeo si yupo akasema ndiyo ,nikamwambia mwambie huyo akasema sawa akirudi atamwambia lkn naomba unikopee wewe hapo micro finance kwa niaba[emoji23][emoji23] nikapotea mazima sikumjibu.


Aisee kati ya ex wabahili huyu namba moja, kuna siku tumetoka safari na gari, nikaomba 4k yake nitumie sikuwa na hela ndogo akanipa, nilidaiwa hiyo hela hadi basi wakat mimi amekula zangu sana.

WANAWAKE WABAHILI, WANAWAKE WABINAFSI, HELA YA MWANAMKE INAUMA KULIKO UCHUNGU WANAOPATA WA KUJIFUNGUA
 
wanawake hawakopeshwi na sio wa kuwasaidia kama marafiki maana wao hawasaidii labda uwe kama umetoa sadaka tu.

Kila demu ana jamaa yake, hela akaombe au kukopa anakotoa mzigo.

Mara buku umkopeshe mchizi huwa wanarudisha, hata asiporudisha ukiwa na shida iliyondani ya uwezo wake ukimsanua tu anachinja.
Kitu nilichojifunza hivi karibuni, ukitaka mwanamke asikuombe pesa acha ukaribu naye usio na maana, ukijiroga utupie na voko ,anakuingiza kwenye list ya vichuna wake.
 
Uko sahihi mkuu mi sijapata shida na masela, wanarudisha bila shida akichelewa kidogo atakwambia. Wenzetu hawa siku ya kukulipa ikifika kimya kama humdai yani
Kawaida yako kuna mmoja niliwai mkopa 30k wakati wa kulipa nikamwambia achana nayo, siku kupita akaja nikopa tena umefika wakati wa kulipa mara mikutumie kwa namba ipi nipo kwa wakala, mara oooh wakala kasema hana hela ntaenda badae, badae mara nliacha simu hostel nikaenda discussion . Lengo tu asikie baki nayo.

Ila nilimkomalia akalipa na ikawa mara ya mwisho kukopa kwangu
 
Mimi nilichojifunza sikopeshi mtu yoyote, niliwahi kopesha mtu laki tatu ni mwanaume mpka leo sjamaliziwa kulipwa pesa yangu. Wakiwa na shida wanakuwa wanyonge ukiwasaidia wanasahau hata waliwahi omba msaada kutoka kwako. Kauli yangu ni moja kwa mja yoyote "siko vizuri kwa sasa" hata kama ninayo pesa sikopesh mtu ni heri nikupe tu kuliko kukopeshana watu si waaminifu, syo wanawake syo wanaume. Tunasaidiana si kwa kuwa tunayopesa saaana hapana ni ubinadamu tu kuoneshana.
 
Back
Top Bottom