Suala la LUGUMI ni mtihani mgumu kwa Rais Magufuli, akiiweza hii basi tena

Suala la LUGUMI ni mtihani mgumu kwa Rais Magufuli, akiiweza hii basi tena

Kwa uzi wa aina hii nadhani umo njiani kutumbuliwa na sheria ya mtandao. Pole sana, comrade
Unamtisha nani sasa, tutasema tusiposema sisi mawe yatasema
 
Bilioni 5 kwa ajili ya mafunzo ya watu watano,haaaa.Nchi hii bwana,sahivi watu wanasema hizi ni njama za ukawa,Rais akija kuwatumbua wahusika watu hawahawa wanaosema ni njama.za ukawa watashangilia tena.
 
Mh.rais ameishasema serikalini kuna mambo ya ajabu, fikiria imekuwaje walipwe pesa yote na huku kazi hawajamaliza ? Pili kwann pccb wako kimya hadi Leo ? Kwanini wizara yenyewe haijawahilalamika kuhusu hiyo Kampuni kwa kutotekeleza mkataba, 3 waziri mhusika mbona hatokei hadharani kulizungumzia ? Nafkri hapo tuunganishe dot tutapata majibu
 
Unamtisha nani sasa, tutasema tusiposema sisi mawe yatasema

Pale mtakaposhughulikiwa na sheria ndipo mtatambua kama ni vitisho au la. Naomba tubadilike, things are changing very fast in this country. Nadhani yule Ndugu wa Arusha aliyekumbana na mkono wa sheria alikuwa haamini ukali wa sheria hii na inawezekana pengine aliwabeza wengine, kama tunavyofanya baadhi yetu.
 
Hili jambo kwa kweli limewakalia vibaya ndugu zsngu wanaccm. Hamjui km msapoti au mpinge!
 
Hamchoki takataka zinazoiba mnachoka zinazopiga kelele za kuibiwa? Kiburi chenu cha utajiri wa wizi kitaisha tu
Rais aliomba kazi anayoifahamu, hujamfundisha na wala hutoweza kumfundisha afanye kipi na aache kipi
 
0d287a9b64f2f4dc575876e9cf3b4c5a.jpg
 
hebu mwacheni Lugumi afanye kazi, acheni kumuingilia muda si mrefu kazi itakamilika kama mkataba unavyotaka
Ukiwa na kumbukumbu kuwa kazi hiyo ili paswa kukamilika toka 2011 kwanini isinge kamilika mpaka sasa na pia ukijiuliza ni kiasi gani cha fedha kitakuwa kimesalia baada ya mgao, na je bei za mashine bado ni zile zile hapo ndio utajua kama kazi hiyo ya kufikirika ita weza kukamilika au laa.
 
Mimi naamini tingatinga limepanda lenyewe huko kwa umahiri wa dereva wake. kihandisi hili linawezekana. dereva anatumia huo mkononyundo wa tingatinga kulipandisha na kulishusha. kuna klipu nyingi zinazoelezea hili. Kinachofanyika ni kuwa dereva anaanda mazingira mazuri ya kusambazia kifusi cha serious fraud. hataki kifusi kuja kuwa kero baadaye kwa kukosa sehemu ya kukizambaza! Mimi ndivyo nilivyomuelewa kipanya.
 
Ukawa bana lugumi lugumi lugumi...mmekosa kazi ya kufanya mnashupalia tu tutumbua majipu lol!
 
Mimi naamini tingatinga limepanda lenyewe huko kwa umahiri wa dereva wake. kihandisi hili linawezekana. dereva anatumia huo mkononyundo wa tingatinga kulipandisha na kulishusha. kuna klipu nyingi zinazoelezea hili. Kinachofanyika ni kuwa dereva anaanda mazingira mazuri ya kusambazia kifusi cha serious fraud. hataki kifusi kuja kuwa kero baadaye kwa kukosa sehemu ya kukizambaza na baadaye ataleta shindilia mashine iweke sawa sehemu hiyo kabla ya kujenga jengo zuri la Uzalendo, uaminifu, utendaji kazi mzuri kwa manufaa ya watanzania wa sasa na wa vizazi vijavyo ! Mimi ndivyo nilivyomuelewa kipanya.
 
Back
Top Bottom