Suala la LUGUMI ni mtihani mgumu kwa Rais Magufuli, akiiweza hii basi tena

Suala la LUGUMI ni mtihani mgumu kwa Rais Magufuli, akiiweza hii basi tena

Natamani nisikie rais kasema vyombo husika vimkamate Lugumi
 
Wana bahati sana sababu ya Mpwa wa Rais anaitwa Kitwanga nae yumo n kampuni yake! Akitumbua inabidi abadili na kuvunh baraza lake la mawaziri ndani ya miezi 6 ya kwanza! Hilo kwa sasa ameliacha kama lilivyo na litapita kimya kimya!
 
Kabla ya Ufisadi wa Lugumi kuwekwa peupe watumbua majipu walikuwa wanaendelea vizuri kutumbua majipu yaliyoifisidi nchi.

Lakini sasa baada ya ufisadi wa Lugumi kuwekwa hadharani, watumbua majipu wakabwaga manyanga na zana zao chini.

Tulichoshuhudia ni yule aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ambaye alihusishwa na Lugumi alitenguliwa uwaziri kwa ulevi. Tangu hapo hatujui huyu 'mlevi' yupo wapi.

Baada ya hapo serikali na bunge zikachachamaa kuminya Uhuru wa kujieleza ndani na nje ya bunge.

Hivi hili Lugumi lina nguvu kiasi gani?
 
Pini ya kutumbulia hatujui ilipo msitusumbueeeee.......kwa sasa tupo busy na kucheki usalama wa Nchi wapinzani wasiandamane wala kufanya mikutano.
 
Police+Lugumi+by+FEDE.jpg


swissme
 
Hata muuza madawa ya kulevya mmoja alosemekana kukamatiwa china akaokolewa na fazake.... anatamba tu ati wanakamatwa mateja wa magomeni ndo wahusika wakuu dah
 
Kuna msemo (methali) moja kutoka Africa Magharibi (unofficial translation):
"Ukitaka kujua kuwa sio kila unapong'atwa na mbu unampiga, ni siku atakapong'ata kwenye testicles (korodani)".
 
Uongozi wa kufahamiana, kupeana kishkaji na kulindana kila idara. Kama humjui nani lazima utumbuliwe. Binafsi siamini katika ulevi wa yule waziri bali kuna jambo zito limefichwa kwenye huo ulevi wake. Ni suala la muda tu, siku wakizinguana linaanikwa jukwaani!
 
Back
Top Bottom