Suala la Machinga, yafanyike haya

Kama suala ni kupata wateja, vp kama wale wenye makampuni ya mabasi nao wakianza kujitafutia maeneo yao binafsi ya maegesho kisa wateja itakuaje??
 
Mabeberu hawatafurahi wakisikia hayo yakifanikiwa
 
Kama unawapenda wanao wajeengee mazingira maalum na mazuri sio kutulea uchafu barabarani mji umekuwa na vibanda kama tuko porini wacheni ushamba huo hapajulikani mjini wala shambani vujo tu.
 
Weweee usicheze na serikali tia vibanda vyote moto mchezo kwisha .Nashauri Serikali iwajengee sehemu rasmi halafu iwahamishe, biashara hizi ndogo ndogo duniani kote zipo lkn si hizi za wamachinga wanavyofanya hawa ni wavamizi wajengewe out of the city maduka au vibanda vidogo vidogo kwa ajili ya biashara zao halafu hamisha kwa nguvu zote
 
Mtaa wa Kongo ulienda kutafuta nini? Nawewe ni mmoja wa waliosababisha idadi kubwa ya watu kariakoo
Mkuu nimesababisha kwa namna ipi?
Mm ni miongoni mwa wanaochukia utaratibu wa biashara za hawa wamachinga na laiti ningekuwa kiongozi ningesafisha majiji yote yenye umachinga.

Jana kuna dada almanusura agongwe na gari kutokana na hawa wanainji.
 
We Acha tu, huyohuyo anayelalamika jioni anapita hapohapo kuhemea nyanya bamia viazi mviringo, eti hamna sehemu za kutembea alijuaje kama hazipo sialipita akitembea alikuwa anatafuta nini kama sio kuhemea

Kukosa utu, roho mbaya na kutowajibika ndio tatizo.
 
Tufike mahali kama Taifa tufuate taratibu zetu kanuni tulizojiwekea,Machinga hana kodi anayolipa pahali popote, kibaya zaidi wanachagua maeneo yale yenye mirija ya watu wengi wanaweka bidhaa zao mbele ya biashara za wanaolipa mamilion ya shilingi kama kodi, Halafu useme eti nao wana familia zao , Je hawa wanaolipa kodi haki yao iko wapi?
 
Sio kwamba hawajui yote hayo ila siasa ndio inaharibu hi nchi.

Wanasiasa wako juu ya kila kitu
 

Tatizo sio machinga, tatizo ni wenye kutakiwa kuwahudumia na kuwasimamia wamekaa maofisini bila kufanya majukumu yao

Unaposema kibaya zaidi wamekaa kwenye maeneo yenye mirija ya watu wengi wewe ulitaka wakauze kusikokua na watu?

Huu Ubinafsi na roho mbaya vinatufanya tushindwe hata kutoa mawazo yanayoweza kujenga nchi na uchumi wetu zaidi ya kubomoa
 
Takataka ni kitu chochote ambacho kipo mahali kisipostahili kuwepo!
Correct!
Hata benz ikiingizwa sebuleni inageuka kuwa takataka, kila mtu atapiga kelele itolewe.

Machinga hawa wanatakiwa kuwekewa njia sahihi na za kufuata taratibu na sheria katika biashara zao.
 
Turudi nyuma kidogo..kabla utawala wa JPM hawa watu walikua kwenye maeneo rasmi katika minada na masoko, Lakini baada ya J PM kuona wafanyabiashara wengi hawakuupenda muelekeo wake akaruhusu hawa Machinga waingie katikati ya miji ili kupata sapoti ya kisiasa.

Maeneo yao yapo wala hahitajiki hata mjumbe kuwaelejeza wanapajua walipokua hapo kabla.
 
Huo ndio ukweriii 100% ndugu zangu
 
Mkuu heko sana, umeandika proposal ambayo imekuwepo akilini kwangu...

Huwa nakosa tu mwamko wa kupoteza nguvu zangu kuandika threads za ushauri hapa...

Tatizo ni kwamba hakuna kiongozi/viongozi wanaochukulia serious mitandao kama hii...

Nchi za wenzetu huwa wanatumia sana wanafunzi waliopo vyuo vikuu kwenye ubunifu wa miradi, mifumo, miundombinu n.k...

Mfano hili la vibanda vya kisasa/mimbari za kisasa n.k vya kimachinga lingeweza pelekwa kama sehemu ya assignment au challenge fupi yenye tunzo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kama ardhi, then wanafunzi wanachora na kusanifu na kuikabidhi kamati maalum. Mwisho wa siku kinapatikana chuo na mshindi anapewa tunzo...

Mchoro unapelekwa kwa wahusika wengine kama JKT kwa ajili ya kuufanya kuwa hai juu ya ardhi...
 

Minada inafanyika mara ngapi kwa wiki? Unataka wakauze kusikokua na wateja ili nani anunue?

Hadi waanze kuanua nguo zako ulizofua ukaanika na kukuchomolea sidemirrors ukiwa unaendesha gari yako ndio utaelewa kwamba wao pia wanatafuta chochote waishi na wao pia wana majukumu na familia kama wewe

Nitaendelea kusema Kinachotakiwa ni kuwapangia na kuwasimamia sio kuwafukuza
 
Pumbav
 
Utamsingizia jpm, hizi siasa zilianzia Zambia, maiko satta alipata support kubwa ya machinga, yule mgombea mwenza yule mzungu alikula sahani moja na machinga tena akitumia bodaboda, baada ya hapo mtizamo wa machinga kisiasa ibadilika.

Pia tukumbuke Lau Masha alipigwa chini na hawahawa machinga baada ya kuwatamkia kuwa akishinda ubunge atawafutilia mbali wakati huo akiwa waziri wa mambo ya ndani sirro akiwa rpc mwanza. Anaijua vizuri nguvu ya machinga.
 

Umeandika kwa kutumia akili za mtafuta kura uchaguzi ukija...

Lakini ungeandika kama mtu wa mipango miji sidhani hata kama ungeandika hivi...

Mpangilio wa mji ni kitu kizuri na faida hata kwa hao wafanyabiashara ndogondogo...

Nitakupa mfano, mji sijui jiji la Mbeya eneo la Kabwe hapo awali lilikuwa eneo wafanyabiashara ndogondogo wanapanga vitu vyao shagalabagala...lakini baadaye kuna kiongozi meenye akili alikuja na utaratibu wa kuwatengenezea meza zilizopangwa vizuri...
 

Sasa wewe unafikiri hao wamachinga wakifa njaa au kuchomwa moto kwa kuwa vibaka kura zitatoshaje😂😂😂

Utaratibu ndio kitu cha msingi, sio kuwadharau wala kuwafukuza. Wao pia wana familia na mahitaji kama wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…