Suala la Machinga, yafanyike haya

Suala la Machinga, yafanyike haya

Mkuu, nasikitika kukuambia kuwa "maamuzi shirikishi" na machinga (+mama lishe) yanayotaka wasionekane barabarani, chini ya transfoma, nje ya majengo ya ofisi, maduka na masoko, kwenye vituo vya mabasi na kwenye njia za wapita kwa miguu, HAYAWEZEKANI.

Machinga, ni wale wafanyabiashara "dynamic" ambao hawako tayari kwa nidhamu ya kufanyia biashara kwenye masoko na maeneo yaliyotengwa rasmi kwa hizo biashara. Hawako tayari kusubiri wateja wanaofunga safari kutafuta bidhaa kwenye masoko na maduka. Wanataka kumuwahi mteja alipo na kumpatia "door to door service" kwa kadiri inavyowezekana. Hiyo ndiyo "niche" yao. Ndio msingi wa biashara yao.

Serikali haina namna ya kukwepa usimamizi madhubuti wa sheria (law enforcement) dhidi ya machinga kama inataka kurudisha nidhamu, usafi na usalama kwenye miundombinu ya miji nchini. Kama serikali imekubali kuwa haina ubavu wa kushughlikia tatizo hili ni bora iachane nalo. Litajitatua lenyewe huko mbeleni.
Kwani kipindi cha jk, mbona yaliwezekana?meko ndio aliwatia jeuri sana!!walikuwa wakijenga vibanda vinavunjwa, na ukikamtwa ni mahakamani kwani sheria si zipo?serikali ikiamua kwa dhati mbona watakubali tu, mfano kuna masoko yamejengwa yako tupu watu hawaendi huko, eti wanafuata wateja nje!!eti litajitatua lenyewe wakati kila siku ndio linazidi, watu wanajenga mabanda kabisa barabarani, ?!!
 
Jitu katili, think again

Hizi ni bla bla za midomoni tu.

Sheria za uzururaji zipo.

Kila mtu anataka kufanya biashara popote, utaongeaje na mtu huyo.

Hataki kujenga frame wala kulipa kodi, hayo mazungumzo yatakuwa vipi.

This is a mass migration from rural areas to towns /cities.

Chukua hao vijana wote peleka JKT walime na wazalishe, hata wakiwa laki tano.
 
JPM aliwapa jeuri ipi?

Unajua kwamba wamachinga nao ni raia wa nchi hii?

Kama hijui usiongee, JPM alitoa maelekezo sahihi kabisa hata SSH anajua

Ila na wanaozibiwa maduka yao nao ni raia wa nchi hii, tena wenye mchango mkubwa sana kwa taifa hili kuliko hata huyo machinga!!na kwani kupitia kodi anayolipi ndio ina muhudumia huyo machinga, lakini machinga anapomfanya asifanye biashara yake vizuri nalo ni tatizo!!mfano nenda mbagala unakuta mtu amelipia fremu tena iko pembezoni mwa barabara kuu, lakini kwa mbele kuna kama kambi ya wavuvi ni maturubai tu hata chochoro la kuzifikia hizo fremi hakuna!!mwisho wa siku anafunga biashara tu,
 
Siyo kwamba hawaelewi.
waliingia mjini kwa mbio za mwemge na kuajiriwa kimkakati.
 
Machinga leo wanaitwa uchafu takataka.

Kama JPM alikuwa anapata feelings nazosikia nikiwatazama wamachinga mitaa ya kariakoo, basi Mungu ampe pumziko jema yule mzee.

Kuna wanangu sijui wataenda kuishije mtu kamaliza chuo miaka 7 hana kazi kaamua kuwa mlengaji anaanza kuona mwanga mara paap anarudishwa kitaa...

Sijui kama watu wanaona kinachoenda kutokea....all in all maisha ni vita ngumu sana mtu asipojua size ya viatu vyako anaweza fanya lolote tu... poleni sana wanangu kwa sasa hamna chenu.
Biashara holela ni vurugu. Mama hajasema Machinga wafukuzwe bali wawekwe kwenye maeneo rasmi.
 
Kwani kipindi cha jk, mbona yaliwezekana?meko ndio aliwatia jeuri sana!!walikuwa wakijenga vibanda vinavunjwa, na ukikamtwa ni mahakamani kwani sheria si zipo?serikali ikiamua kwa dhati mbona watakubali tu, mfano kuna masoko yamejengwa yako tupu watu hawaendi huko, eti wanafuata wateja nje!!eti litajitatua lenyewe wakati kila siku ndio linazidi, watu wanajenga mabanda kabisa barabarani, ?!!
Machinga Complex ilijengwa kipindi cha JK na machinga hawakwenda kwa kifupi waligoma
 
Machinga leo wanaitwa uchafu takataka.

Kama JPM alikuwa anapata feelings nazosikia nikiwatazama wamachinga mitaa ya kariakoo, basi Mungu ampe pumziko jema yule mzee.

Kuna wanangu sijui wataenda kuishije mtu kamaliza chuo miaka 7 hana kazi kaamua kuwa mlengaji anaanza kuona mwanga mara paap anarudishwa kitaa...

Sijui kama watu wanaona kinachoenda kutokea....all in all maisha ni vita ngumu sana mtu asipojua size ya viatu vyako anaweza fanya lolote tu... poleni sana wanangu kwa sasa hamna chenu.
Mimi najua maumivu ya maamuzi kama haya,nakumbuka miaka ile mkapa,naamka asubuhi nasikia redioni Mungai afanya kweli,kafuta masomo ya ufundi,wakati huo ndo masomo nayofundisha watoto wapate chakula
 
Machinga ni jini ambalo CCM walilitoa kwenye chupa halafu JPM akaliweka sebuleni kwao. Halitoki, halifi, halidhibitiki.
Bila kuzingatia misingi ya utawala bora na demokrasia CCM hawawezi kutatua hili tatizo.
The HALLMARKS of bad governance:
1. Arbitrariness
2. Ambiguity
3. Capriciousness
 
Wana haki kama raia, kama ni issue ya kulipa kodi kila hata kwenye salaried employees wapo ambao hawalipi, na wapo wanaolipa kidogo na wanaolipa kubwa pia

Mnatamani msilipe kodi kama wao wakati mnaishi na kumiliki mitaji tofauti kabisa na wao. Kama hutaki kulipa kodi sababu unashindana na mmachinga na wewe kuwa mmachinga ili upate hiyo raha
Your correct, muza nyanza bamia hoho atalipa kodi ipi? Isitoshe kilasiku anapanda daladala linalotumia mafuta yaliyolipiwa kodi, mwingine humu anatumia gari stk ambalo halilipi kodi wala bima
 
Kwanza kabisa napenda kupongeza serikali kwa maamuzi waliyoanza kuyafanya ya kuwaondoa Machinga katika maeneo ambayo hawatakiwi kuwepo Mf Barabarani na kwenye maeneno ya miji yenye shughuli za kiofisi n.k

Tulishauri hapa na tumeshauri hapa kwa miaka mingi sana namna ya kuhandle hili jambo na nashukuru sasa Serikali wameona kuna haja lianze kufanyiwa kazi.

Kwanza napenda kusema wazi Tatizo la mipango mibovu kwenye miji yetu, majiji yetu ikiwemo kuzagaa hovyo kwa machinga ni matokeo ya uvivu, uzembe , kukosa exposure na kutowajibika kwa kipindi kirefu sana Kwa watendaji wetu! Hii ni Kwa sababu suala la machinga lilitakiwa kuanza kufanyiwa kazi kwa kipindi kirefu sana na hata sasa hili kundi lingekuwa linafanya kazi katika maeneo yaliyopangwa vizuri na hata lingekuwa linalipa kodi Kama makundi mengine ya wafanyabiashara.

Napendekeza katika kuangalia mipango ya muda mfupi na mrefu! Suala la machinga lishughulikiwe Kama ifuatavyo

1. Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Watendaji Wao, waande kufanya vikao vya majadiliano na Machinga. Wawaeleze kuhusu umuhimu wa wao kuendelea kufanya biashara ila kwenye maeneo rasmi, yaliyopangwa vizuri na kuwekewa utaratibu mzuri. Vikao hivi Vifanywe kwenye maeneo halisi walipo Machinga/ Wafanyabiashara wadogo wadogo.

2. Wakuu wa Mikoa, Wilaya, waandae maeneo hayo rasmi yenye mzunguko mkubwa wa watu mf. Karibu na vituo vya mabasi au ofisi au masoko na wawape tenda hata vijana wetu wanaosoma chuo cha ardhi wadesign aina ya majengo/ vibanda ambayo vinatakiwa kujengwa kwenye maeneo hayo. Michoro hiyo ikishapitishwa, Uongozi wa Majiji na Miji husika ndo ujenge na kusimamia ujenzi wa hayo structures izo - Ziwe na standard moja zinazofanana na zijengwe kisasa.

Msisitizo uwekwe kwenye kujengwa structures izo kwenye standard za juu za ubora ambazo haziruhusu miji kuchafuka. Zikishajengwa then wafanyabiashara wadogo wadogo wapangiwe kufanya kazi kwenye maeneo hayo. Kwa utaratibu wa kuzingatia usafi na mpangilio bora.

3. Uwekwe muongozo wa Wafanyabiashara kufanya biashara kwenye maeneo hayo. Ziteuliwe kamati za Wafanyabiashara hao hao katika kusimamia iyo miongozo itakayogusa namna ya kufanya biashara, jinsi ya kuzingatia usafi na mpangilio. Endapo eneo husika litakiuka hiyo miongozo uwajibishwaji uanze kwa kamati husika. Kuwe pia na penalties katika kukiuka iyo miongozo ikiwemo fine na hata kuzuiwa kufanya biashara kwenye eneo hilo.

4. Endapo mfanyabiashara anahitaji kufanya biashara nje ya eneo lililopangwa na kutengwa Kwa ajiri ya yeye kufanya biashara, kuwe na Miongozo maalum ya namna mfanyabiashara huyo anatakiwa kufanya biashara yake kwenye eneo hilo, namna anavyotakiwa kujenga eneo lake la biashara na Pia wawekewe kodi maalum ya kulipia ili afanye biashara kwenye eneo hilo ambalo ni nje ya eneo lililotengwa kwa kufanyiwa biashara. Kiwango cha kodi ambacho mfanyabiashara hiyo anatakiwa kulipa katika kufanya biashara kwenye eneo hilo lazima kiwe juu zaidi kuliko kiwango anachotakiwa kulipia katika maeneo ambayo wenzake wametengewa kufanya biashara.

Mwisho napenda kumpongeza Mama Samia kwa kuruhusu hili lifanyike. Naomba tu haya mawazo yazingatiwe maana tutaweza kumaliza hili Tatizo la uchafuzi wa miji na kuharibika kwa majibu yetu kutokana na ufanyaji wa biashara holela usiozingatia mipango miji na ukusanyaji wa kodi.

Naomba kuwasilisha
Chukua Kariakoo, hilo jengo maalum kufanyia biashara lijengwe mtaa gani? Tupe mfano.
Hayo masoko yaliyojengwa maeneo wanakoishi machinga hao na hawayataki, unataka wapelekewe watu wa aina gani ambao watanunua bidhaa zao.
Nini tofauti ya bidhaa za wamachinga na za wenye maduka?
Hao wamachinga siku zote wanao viongozi wao, hivyo hilo si jipya.
Kigezo cha eti wanatafuta riziki ndicho kinawajengea kiburi, kila mtu mzima mwenye nguvu hutafuta riziki ili aweze kuishi, mwenye duka hauzi sura dukani pake naye anatafuta riziki.
Siasa rahisirahisi ndizo zimetufikisha hapa na zitakuwa mbaya zaidi tuelekeako kwani idsdi yao inazidi kuongezeka kwenye eneo dogo.
 
Haya yote kasababisha yule "nileteeni Gwajima"

Siku hizi ukipita kariakoo umachinga kila kona na hawana wasiwasi.

Jamani eeh hawa wamekupeni kura lakini isiwe sababu ya kusababisha tabu kwa wengine.

Leo nilipita Mtaa wa Kongo machinga wamefunga barabara yote hata pakukanyaga ni mtihani nikajiuliza hv hii nchi ina sheria au tunaishi kama kuku.!!!😎
Makala ondosha machinga usiogope lawama ajali nyingi zinatokea maeneo ya Msimbazi kutokana na uzembe na ujinga huu wa kuwaogopa hawa wamachinga.

Mama Samia hawa wamachinga ni chanzo cha ajali nyingi katikati ya jiji tafadhali fanya jambo mama.
Mtaa wa Kongo ulienda kutafuta nini? Nawewe ni mmoja wa waliosababisha idadi kubwa ya watu kariakoo
 
Wamachinga waliotapakaa ni raia wa wapi?
Kama ni wa Tanzania acha kuwaangalia wao kama tatizo, kaongee na viongozi walioshindwa kuwaongoza na kuwasimamia
Ikiwa tatizo la machinga halijakuathiri ni rahisi kuzungumza jinsi ambavyo unaweza, Lakini ukweli machinga na JPM wameiharibu inchi, Mamia ya biashara zilizokua rasmi zilifungwa kwa sababu ya kadhia hii machinga, Haiwezekani ulipie kodi za TRA,Vibali vya Halmashauri, Ulinzi shirikishi, tozo za usafi halafu mtu ackachonge tu meza ya mbao aiweke mbele ya Biashara yako, HUU NI UPUMBAVU ULIOPITILIZA.
 
Kwani JPM alikua anakubarika? Au alikua analazimisha misifa ya kijinga tu....Mungu Fundi... Ata nyumbani kwako kuna utaratibu huwezi ruhusu watoto wako waweke Viatu kwenye Friji huo ni upumbavu tu...Leo machinga wanapanga nyanya Barabarani kwenye Rami hii uliiona wapi km ulikua sio usen.ge wa JPM? Wakuu WaMikoa baadhi walijaribu kuwatafutia maeneo ya kwenda wakawa hawataki na JPM akawa anawakaripia hao wakuu... Leo pita miji mikubwa yani wamepanga nyanya hadi kwenye Round about kitu ambacho ni ushamba na hatari kwa usalama... Nchi lazima iwe na utaratibu... Samia ndo Rais kwasasa uwe umempigia kura au lah ata JPM hakupendwa na wote
Ulisha jiuliza kwanini machinga hawako masaki wala lugalo?
 
Ikiwa tatizo la machinga halijakuathiri ni rahisi kuzungumza jinsi ambavyo unaweza, Lakini ukweli machinga na JPM wameiharibu inchi, Mamia ya biashara zilizokua rasmi zilifungwa kwa sababu ya kadhia hii machinga, Haiwezekani ulipie kodi za TRA,Vibali vya Halmashauri, Ulinzi shirikishi, tozo za usafi halafu mtu ackachonge tu meza ya mbao aiweke mbele ya Biashara yako, HUU NI UPUMBAVU ULIOPITILIZA.

Wameharibu nchi kwa sababu wanaotakiwa kuwasimamia wamekaa maofisini bila kufanya mipango yoyote? Kwani kulikua na gharama gani wahusika kuwapangia sehemu zisizotakiwa kufanya biashara kama zile njia za waenda kwa miguu na kwingineko?

Wewe unashauri tuwapeleke wapi watakapoweza kuishi na kutunza familia zao ili nchi unayosema wameiharibu itengamae??

Kabla ya kuwaza juujuu na kuishia kuwaona machinga tatizo tafuteni mzizi wa tatizo
 
Ulisha jiuliza kwanini machinga hawako masaki wala lugalo?

Watu wavivu hawataki kutumia akiliza kufikiria kabisaaa, badala yake wanaishia kuwaona binadamu wenzao tatizo
 
Ikiwa tatizo la machinga halijakuathiri ni rahisi kuzungumza jinsi ambavyo unaweza, Lakini ukweli machinga na JPM wameiharibu inchi, Mamia ya biashara zilizokua rasmi zilifungwa kwa sababu ya kadhia hii machinga, Haiwezekani ulipie kodi za TRA,Vibali vya Halmashauri, Ulinzi shirikishi, tozo za usafi halafu mtu ackachonge tu meza ya mbao aiweke mbele ya Biashara yako, HUU NI UPUMBAVU ULIOPITILIZA.
Machinga haendi China, wenye madukq ndio huwapa bidhaa machinga wakauze jioni wapeleke hesabu, eti mtu hauzi mbona hafungi biashara na frem analipia 10m kila mwaka

Ulishawaji kutana na matangazo ya ajira chapchap hebu fuatilia ni ajira gani kama hautaishia kubebeshwa mabeseni vijiko pasi chupi sindiria soksi.
 
Watu wavivu hawataki kutumia akiliza kufikiria kabisaaa, badala yake wanaishia kuwaona binadamu wenzao tatizo
We Acha tu, huyohuyo anayelalamika jioni anapita hapohapo kuhemea nyanya bamia viazi mviringo, eti hamna sehemu za kutembea alijuaje kama hazipo sialipita akitembea alikuwa anatafuta nini kama sio kuhemea
 
Back
Top Bottom