Suala la Maji: Utawala corrupt unatuletea shida, Mchina akamatwa akichepusha maji mto Ruvu kumwagilia mboga

Mkuu wanasema pale Ruvu kwenye mitambo ya maji yamepungua maji lita milioni 150.Na kuna labda watu sampuli hiyo zaidi ya elfu moja wanachepua maji na labda watu milioni mmoja wanaharibu kingo za mto sababu ya shughuli za binadamu.

Na huo mtambo wa Mchina unachepua lita milioni 1 kwa saa ni wastani wa milioni 24 kwa siku.That is tip in iceberg

Tuseme tu matumizi holela hayajaanza leo,kwanza ni aibu kuwa na mamlaka ya hifadhi kumbe ni dili tu.Hizo wizara za mazingira zingevunjwa ni rushwa tu hamna kitu.Iundwe idara itakayoratibu shughuli za umwagiliaji kwenye wizara ya maji.
 
Mene Mene tekeli na peresi. Hawa wawekezaji wa mboga mboga ndio hangaya alisema wasisumbuliwe vibali sio.
 
Tangu lini wachina wakafata sheria, hawa dawa yao ni kuwakazia kwenye vibali vya uwekezaji sababu hata kazi zao zenyewe hazionekani na ni wezi wakubwa wa kodi.
 
Yaani umuachie mhalifu ambaye most likely kuna wakubwa aliowahonga ili afanye uharamia huo aendelee?
Nimesoma karibu comments zote na kila mtu amecomment kutokana na uelewa wake.

Ni kweli mkulima huyu wa mbogamboga alitumia fursa iliyotangazwa na serikali kukaribisha wawekezaji waje kuwekeza.Akaja kupitia uhamiaji kama alipitia na naamini alipitia kwa sababu anapolima kuna viongozi wa serikali,kuanzia balozi,wenyeviti mbalimbali,mbunge n.k.

Haikutosha,serikali ikawa inahamasisha kulima kilimo cha umwagiliaji,Mchina akajiongeza akakianzia,na wananchi wengine wengi,nao tunawafahamu wanafanya kilimo cha umwagiliaji na mboga zao tunakula kila siku.Imekuwaje leo hii,kilimo cha umwagiliaji kwa mchina kiwe haramu lakini kwa wengine kiwe halali.Au serikali ilikuwa na maana gani kuhamasisha kufanya kilimo cha umwagiliaji,au walikuwa wanamaanisha kumwagilia kwa kutumia ndoo ya mkono.

Huyu Mchina hakuanza kulima leo.Labda mniambie kuwa hakuwa na kibali cha kuishi nchini.Na kama ni hivyo kwa nini hakukamatwa siku zote.Hii tafsiri yake taasisi ya usalama imelala usingizi mzito,inasubiri kuambiwa ya kuwakamata viongozi wa upinzani raia wa nchi hii na kuwapa makesi makubwa makubwa ambayo hayana dhamana.

Na hapa napenda kusema hivi.ni maoni yangu.Kukamatwa kwa Mchina kumetokana na kukatika kwa umeme kitu ambacho sio sahihi.Kama sababu ya umeme kupungua ni Mchina kumwagilia Serikali mnatudanganya.Tafuteni sababu nyingine.

Mmetueleza sababu nyiiiiingi sana za ubabaishaji,mara mashine hazikufanyiwa service kipindi cha JPM.Kwa nini kipindi hicho hizo mashine hazikufa? mara maji yamepungua nk. Nitaendelea tena chai inapoa
 
Duuh kazi ipo kwahio Chalinze wamejaa wachina wengi eeeh?!

Labda bandari ya bagamoyo inawekwa kimkakati kwa ajili ya kusafirisha mazao yao na kulisha nchi yao….
 
We unaona sawa mchina kuja kulima mboga Tanzania? Huo ndio uwekezaji uliomleta
 
Subirini mtakuta ana vibali halali vya uwekezaji kapewa na wizara husika na kwa mbwembwe kabisa hapo ndio mtajua mazuzu wako wengi na sio wa 'kule' tu
 
Huko ni kumuonea..viongozi wako ndio blalifakini .
 
Mkuu,kwa mujibu wa mzee Kasesela hapo hizo ni lita milioni 2 zinatolewa zisilete madhara kwenye mitambo.
Kwa hiyo lita milioni moja ni nusu ya hayo maji uyaonayo hapo.

Tunaambiwa tena mchina anayatumia ndani ya lisaa tu,kumwagilia matembele na mchicha ..maamae bongo tunaonana wajinga sana!😆
 
Kwani hawa wachina walianza lini kuingia nchini?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Nchi hii haiwezi kupata maendeleo chini ya chama cha majambazi na wahudumu uchumi wanaojiita wazalendo, çcm
 
Hiyo bodi ya maji ilipaswa wote wawe wameachishwa kazi baada ya kutangaza hii taarifa. Bodi ilikuwa likizo na sasa ndo wamerudi kazini baada ya madhara kuwa makubwa
Wala sio bodi ya maji, yaani ndani ya wizara ya maji kuna idara inayoshughurika na mabonde, na huo ndio huwa wanatoa vibali vya kutumia maji na sio bure!!huyo mchina ni sarakasi tu, wala hutasikia kitakachoendelea!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…