Man Mvua
JF-Expert Member
- Apr 12, 2016
- 2,183
- 3,521
Amani iwe juu yenu.
Jambo la mishahara ni kitu muhimu sana kwa mtu ndio maisha yake na ndio uhai wake. Kuna mtumishi namba moja aliyepita alipata kusema "Asiyefanya kazi na asile na maana yake afe" hivyo kila mtu hufanya kazi ili aishi yeye na familia yake.
Unyeti wa mshahara ndio umefanya mimi leo niandike hii mada, Nchi yetu bado ina unyonyaji ambao tunafanyiana sisi kwa sisi. Tumejitengenezea matabaka kwenye ofisi na taasisi zote za umma. Tumefanya aina fulani za kazi zikimbiliwe na watu wengi (ubunge) na zingine zikimbiwe (na matajiri) zikimbiliwe na maskini mfano UALIMU.
Ili Nchi yoyote iendelee kwanza jambo la usawa ni muhimu sana na kada za kuendeleza Nchi ndio hupewa kipaumbele Mf: Elimu, viwanda na technology. Nchi hii wanaozalisha hulipwa kiduchu na wafanyamaamuzi hulipwa pesa mlima its contrary the opposite.
Hivi ni kwa nini wanaofanya kazi TRA, BOT, TPA, TASAC na n.k hulipwa zaidi kuliko Walimu na Manesi na Polisi na Majeshi yetu? Bado wana posho, marupurupu na per diem? Hivi kwa nini Mwalimu wa Degree anachukua mshahara laki tano au sita kwa mwezi na hana posho wala per diem mwaka mzima. Halafu mtu mwingine mwenye kiwango sawa cha Elimu anayefanya kazi BOT analipwa 1.8M kwa mwezi? Aiseee!
Mtumishi namba moja aliyepita awamu ya tano alipata kujiuliza kitu ambacho hata mimi najiuliza, "KWANI WALISOMAJE HAWA" mpaka mtu alipwe 25M au 30M kwa mwezi? Mwisho wa kunukuu.
Nchi hii kuna kazi za watoto wa maskini mfano UALIMU, UNESI, UDAKTARI, UFUNDI na n.k pia kuna kazi za watoto wa vigogo (wazee wa kujipangia mishahara yao) na huu mfupa ni mgumu sana kwa sababu hata watoto wa maskini wanaofanikiwa kufika juu kama Magufuli na Samia hushindwa kuuondoa na kuweka usawa ili nchi Iendelee.
Maendeleo ya Nchi tutayasikia kwenye bomba tu kwa aina hii ya unyonyaji isipokuwa mwenye nacho ataongezewa (be rich to get rich)
Kazi njema wajameni nilikuwa na frustrations zangu tu baada ya kupata report ya BOT.
"TUSIDANGANYWE TENA NCHI HII HAKUNA MZALENDO HATA MMOJA LABLA MIAKA 100 IJAYO NDIO WATAZALIWA."